Cerca

Vatican News
Pope Francis Baba Mtakatifu amekutana na uwakilishi wa kiekumene kutoka nchini Finland   (ANSA)

Papa:Njia ya uekumene ni ya dharura na msingi wa imani!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 19 Januari 2019 amekutana na mahujaji wa kiekumene mjini Roma kutoka nchini Finland wakiwa katika fursa ya Sikukuu ya Mtakatifu Henrik ambapo katika hotuba yake amehimiza juu ya kutembea pamoja katika hija ili kuweza kufikia umoja, kwani ni safari yenye kuanzia katika chemchemi inayobubujika kutoka ubavu wa Kristo msalabani

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 19 Januari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na mahujaji wa kiekumene mjini Roma  kutoka nchini Finland wakiwa katika fursa ya Sikukuu ya Mtakatifu Henrik na kuwaruhusu  kuwa na mkutano wao kindugu ambao unachangia uhamasishaji wa umoja wa wakristo.Akiendendelea na hotuba yake anasema,wajibu wa pamoja kwa ajili ya kuendeleza uekumene ni dharura msingi wa imani ambayo sisi sote tunakita, ni suala ambalo linazaliwa na asili yenyewe ya utambulisho wa wafuasi wa Yesu. Kwa kuwa mitume wote ni kufuata Bwana mwenyewe kwa kutambua daima kuwa uekeumene ni mwendo, mwendo ambao kama walivyokuwa wanasisitiza mapapa mbalimbali tangu Mtaguso wa Vatican II na kuendelea kwa maana haiwezekani kuwa tofauti na wala uchaguzi. Umoja kati yetu unazidi kukua katika mwendo huu mrefu na kwa maana hiyo, hija yao ya mwaka mjini Roma, Baba Mtakatifu amebainisha ni ishara kwa namna ya pekee ya ufasaha ambapo anawashukuru.

Hija yao ni kwa neema ya Roho Mtakatifu anayeongoza kufika kwa Kristo

Hija hiyo inawaalika kutembea pamoja katika njia ya umoja ambayo ni kwa neema ya Roho Mtakatifu anayeongoza pamoja ili kufika  kwake Kristo Bwana wetu kama wana wapendwa wa Bwana, kwa maana nyingine ni kaka na dada kati yetu. Baba Mtakatifu anampongeza hata Askofu wa Kiluteri wa Kuopio wa Finland, kwani zaidi ya maneno yake aliyotoa  yenye thamani ya sala, lakini  hata kwa ajili kuweka umakini, kwamba sisi sote awali ya yote tuko katika huduma ya upendo na ushuhuda wa imani ya pamoja ambayo inatakiwa kuifanyia kazi. Shughuli hiyo inajikita katika msingi wa Ubatizo wa kuwa wakristo na ndiyo kitovu cha kweli kama ilivyokuwa inakumbusha katika mfumo wa elimu jamii ambayo mara nyingi inachangia kijujuu kwa wakristo katika mantiki hiyo kwa upande au pia kutokuwa na maana. Iwapo tunasali pamoja na kutangaza Injili na kuhudumia maskini na wahitaji ndipo njia ya kujitafuta katika mwendo hai, na ni mwendo kamili  wa maendeleo kueleka katika upeo unaonekana wa umoja.

Hata katika masuala ya kitaalimungu na kikanisa ambayo bado yanatutofautisha Baba Mtakatifu anakazia ya kuwa, yanaweza kupata suluhisho tu, katika mchakato wa hatua za pamoja na haiwezekani kamwe kubaki zimesimama; bila kutoa juhudi kwa njia ya mikono yetu na bila kutazama kwa  jinsi gani itatokea. Lakini tunaweza kuwa na uhakika iwapo tutakuwa wapole katika Roho Mtakatifu, naye  atatuongoza namna ambazo leo hii hatufikiri. Tunaalikwa kufanya kile tuwezacho kwa ajili ya kusaidia makutano  ili kupata suluhisho la upendo ulisoalitiwa, wenye vizingiti, hukumu za karne nyingi ambazo zimeendelezwa katika mahusiano yetu.  Katika hatua za kupelekea taalimungu, imechangia hata kwa Tamko la pamoja la hivi karibuni la Tume ya mazungumzo kati ya Wakristo Waluteri, nchini Finland kuhusu Kanisa, Ekaristi na huduma za kichungaji, tamko linaitwa Umoja unaokua. Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa ufuatwe na kuendelezwa mbele kwa kile kilichoanzishwa!

Katika hija hatutembei peke yetu, tunaongozwa pia na utamaduni

Katika safari, ni kukumbuka kuwa hatupo peke yetu Baba Mtakatifu anathibitisha. Kuna mashuhuda wa pamoja ambao kama Mtakatifu Henrik alionesha katika safari, kwa namna hiyo ni kweli kwamba ni neema  kabla ya kumkumbuka na utamaduni siyo mchezo ni zawadai. Utamaduni unakumbushwa katika neno la kilatino kwamba ni kukabidhi. Utamaduni siyo kitu cha binafsi ili kitengenishe, badala yake ni utamaduni ni kukakabidhi ili kutajirishana sisi kwa sisi.

Wote wanaalikwa daima kurudi katika chemchemi ambapo mifereji inabubujika utamaduni. Ni katika ubavu uliofunguka wa Kristo msalabani. Yeye alijitoa binafsi na kutupatia hata Roho wake (Rej Yh 19,30.43). Kutokana hapo, ndipo yapo maisha yetu, na ya kila mwamini; pale kuna hata upyaisho wa milele. Pale tunapata nguvu ya kubeba uzito na misalaba ya mmoja na mwingine. Kwa kutanguliwa na kusaidiwa wale ambao walitoa maisha yao kwa ajili ya upendo wa Bwana na ndugu, sisi sote tunaalikwa tusichoke kamwe katika safari.

Maadhimisho ya kuombea amani kila mwaka

Kila mwaka wakristo duniani kote wamejiwekea siku maalum kwa ajili ya kuomba kwa Bwana umoja. Ni Wiki ya kuombea Umoja wa Wakristo ambapo mwaka huu unajikita kwa kina katika neno la kibiblia: “tafute kuwa wenye haki kweli ( Kumb 16,18-20.) Ni upamoja na kutukumbusha kuwa hatuwezi kutenda haki pekee yetu. Haki kwa ajili ya wote inahitahi kutafuta kwa pamoja, Baba Mtakatifu amekazia.  Katika dunia iliyojaa mipasuko ya vita, chuki, utaifa na migawanyiko, maombi na juhudi ya pamoja ajili ya haki , kwa kiasi kikubwa siyo ya kuacha na wala siyo uchaguzi. Ni dhambi ya kutotimiza wajibu ambayo hatuwezi kuruhusu. Baba Mtakatifu anayo matumaini kwamba ushuhuda wa pamoja katika sala na imani unaweza kuleta matunda hata ziara yao itatiwa nguvu na uthabiti wa ushirikiano kati ya waluteri, waorthodox na wakatoliki nchini Finland. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amehitimisha kwa kuwabariki kila mmoja ili neema ya Mungu iweze kuwashukia na kuwaomba waendelee kusali kwa ajili yake.

19 January 2019, 15:07