Tafuta

Vatican News
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana  (ANSA)

Papa:Mama Maria anatuonesha mwanae anayetubariki!

Mama Maria anatuonesha mtoto aliyemkumbatia mikononi mwake, anabariki familia ya kibinadamu na ili wote tujikite katika huduma ya amani. Ni mbiu iliyosikika katika tafakari ya Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 1 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo ni siku ya nane baada ya Noeli, tunaadhimisha Sikukuu ya Mama Matakatifu wa Mungu. Kama wachungaji wa Betlehemu, tubaki bado katika mtazamo wetu kwa mtoto ambaye mama yake amemkumbatia mikononi mwake. Na kwa maana hiyo anatuonesha Yesu Mwokozi wa ulimwengu na kwake yeye anatubariki. Anabariki safari ya kila mtu na kila mwanamke katika mwaka huu inaoanza na ambapo yeye atakuwa mwema kwa kadiri ya kila mtu atakavyopokea wema wa Mungu ulioletwa na Yesu duniani. Kwa dhati ni baraka ya Mungu ambaye katika hizi za sikukuu wanatakiana wote heri. Leo hii liturujia inatupeleka kujikita  katika baraka ya kizamani ambayo makuhani wa Israeli walikuwa wakibariki watu wao. Baraka hiyo inasema kuwa: “Bwana akubarikie na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake na kukupa amani” (Nm 6,24-26).

Kwa mara tatu kuhani alikuwa anarudia jina la Mungu Bwana

Ni mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, kwa waamini na mahujaji wot waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, wakati Mama Kanisa anadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu sambamba na maadhimisho ya Siku ya 52 ya Kuombea Amani Duniani kwa mwaka 2019. Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari yake anasema: “Kwa mara tatu kuhani alikuwa anarudia kwa jina la Mungu, “Bwana”akiwa ameamsha mikono yake juu ya watu waliokuwa wamekusanyika. Katika Biblia, jina linawakilisha hali halisi ambayo inatamkwa na ndiyo maana limewekwa jina la Bwana juu ya mtu na familia au jumuiya ili kuweza kuipa nguvu  za baraka zitokazo kwake.

Maneno hayo kwa mara mbili yanatajwa uso wa Bwana. Kuhani anasali ili Mungu awangazia na kuwa kuwafadhili, wakati huo awainulie uso wake na kuwapa amani. Tunatambua vema kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya kwamba, kuona uso wa Mungu ni vigumu kwa mtu, kwa maana hakuna anayeweza kuona uso wa Mungu akabaki na maisha. Hiyo ni hali halisi inayoelezea juu ya ukuu wa Mungu usioisha katika utukufu wake. Lakini pia utukufu wa Mungu ni upendo wote japokuwa huwezi kuonekana, kwa maana ni kama Jua ambalo huwezi kulitazama kwa karibu sana, Mungu anaangaza neema zake kwa kila kiumbe na kwa namna ya pekee kwa wanaume na wanawake ambao sehemu kubwa wanahusika baba Mtakatifu amesema.

Wakati maalumu ulipotimia, Mungu alionesha uso wake kwa njia ya mtu

Lakini wakati maalumu ulipotimia, Mungu alionesha uso wake kwa njia ya mtu, Yesu aliyezaliwa na mwanamke akaishi chini ya sheria (Gal 4,4). Baba Mtakatifu anafafanua kwamba hapa inarudia ile picha ya siku ya leo tuliyo anza nayo. Picha ya Mama Mtakatifu wa Mungu ambaye anamwonesha Mwanae Yesu Kristo, Mwokozi wa dunia. Yeye ni Baraka ya kila mtu na familia nzima ya kibinadamu; Yeye ni chemi chemi ya neema, ya huruma na amani.

Ni sikukuu ya Bikira Maria mama wa Mungu sambamba na Siku ya Amani duniani

Baba Mtakatifu akiendelea kufafanua sikukuu ya Bikira Maria mama wa Mungu anathibitisha kwamba ndiyo maana “Mtakatifu Paulo VI alipendelea kuwa siku ya kwanza ya mwezi Januari iwe ni Siku ya Amani na leo hii tunaadhimisha Siku ya 52 ya Kuombea Amani Duniani, inayoongozwa na kauli mbiu: “Siasa safi ni huduma ya amani”. Hatuwezi kuridhika na kuona siasa inajihusisha tu kwa watu wa serikali. Watu wote wanapaswa kuwajibika katika maisha ya mji na kwa ajili ya wema wa pamoja na hata siasa safi ni njema kwa kipimo ambacho kila mmoja anashika nafasi ya kujihusisha katika kukuza amani. Mama Matakatifu wa Mungu atusaidiea katika jitahada hizo za kila siku. Baba, Mtakatifu anamependelea kila mmoja aweze kumsalimia mara tatu Maria Mama wa Mungu na ndiyo ilikuwa hitimisho ya tafakari ya malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini waliounganika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro.

 

01 January 2019, 13:47