Tafuta

Urafiki kati ya Wayahudi na Wakristo ni wa muda mrefu Urafiki kati ya Wayahudi na Wakristo ni wa muda mrefu 

Papa Francisko:Tukarabati mpasuko wa kutoelewana kati ya Wayahudi na Wakristo!

Baba Mtakatifu Francisko ameandikia utangulizi wake katika kitabu kilichopewa jina: Biblia ya urafiki.Meneno ya Torah/Pentateuki, tafakari ya kiyahudi na kikristo, kitakachotolewa katika maduka ya vitabu tarehe 18 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika utangulizi wa Kitabu cha Biblia ya urafiki. Maneno ya Torah/Pentateuki tafakari ya Wayahudi na Wakristo. Baba Mtakatifu Fancisko anasititza kuwa nyma ya mabega yetu ya karine ya XIX  ya ubaguzi wakristo wayahudi na ambao kwa miaka kumbi hivi ya mazungumza yalutofanyiika, lakini licha ya hayop kipindi cha miwsho mambo mengio yamebaki hivyo na mengi bado yanahitaji kibadilishwa. Ni kitabu ambacho kitolewa katika maduka ya vitabu tarehe 18 Januari 2018 Kitabu ambacho kipmepea Jina la “Biblia ya urafiki. Maneno ya Torah ana Pentetuko tafakari ya wayahudi na wakristo!

Kitabu hicho kimeandikwa na Marco Cassuto Morselli na Giulio Michelini (Cinisello Balsamo, Toleo la  Mtakatifu Paulo, 2019), kitakachotoka tarehe 18 Januari 2019.  Utangulizi wa Kitabu hicho umetangazwa na Gazeti la Osservatore Romano tarehe 15 Januari 2018 ambapo Baba Mtakatifu anakazia kwamba ni lazima kukarababati nyufa ziliotokana na ukosefu wa uelewa kati ya wayahudi na wakristo. Kadhalika anasisitiza  njia ambayo no bora katika mazungumzo siyo tu kuzungumza na kujadiliana, bali ni kuandaa mipango ya kutimiliza kwa pamoja . Lengo kuu la pamoja ni lile la kuwa mashuhudwa wa upendo wa Baba katika dunia nzima.

Ukarabati wa mpasuko wa uhusiano kutokana na ukosefu wa uelewa

Kwa upande wa Wayahudi kama vile kwa wakristo hakuna wasiwasi ya kwamba kuna upendo wa Mungu na jirani ambao unajikita katika amri ya Mungu. Wayahudi na wakristo wanapaswa kwa dhati kuhisi kwa pamoja undugu kama  kaka na dada daima wanaounganishwa  katika Mungu mmoja mwenye urithi wa utajiri wa kitasaufi wa pamoja na  msingi mmoja ambao unaoendelea kujenga wakati endelevu.

Baba Mtakatifu anathibitisha jinsi gani alivyo na utambuzi wa  karne 19 nyuma yetu ambayo imekuwa na matukio ya ubaguzi wa kiyahudi na hata kwa makumi ya miaka ya mazungumzo ambayo yameweza kufanyika kuhusiana na suala hili. Licha ya hayo kwa nyakati za mwisho, mambo mengi yamekuwa na mabadiliko na mambo mengine bado yanaendelea kuwa na mabadiliko kwa taratibu. Kwa maana hiyo inahitaji kutanya kazi kwa kiasi kikubwa hasa cha kuomba msamaha ili kutoa malipizi ya mabaya yaliyotendeka kutokana na ukosefu wa uelewa. Thamani, utamaduni na mawazo ambayo yanatambulisha uyahudi na Ukristo, lazima yaweze kuwekwa katika huduma ya ubinadamu, bila kusahuliwa kamwe utakatifu wake na udhati wa urafiki. Biblia inatufanya kutambua vema kuwa, ukiukwaji wa thamani hizi unahitaji haraka kukarabatiwa njia ya mazungumzo ya kujenga.

Kujifunza Torah

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua zaidi juu ya mahusiano hayo anasema ni lazima kuwa na jambo la maisha katika umuhimu wa wakristo kwa kugundua na kuhamasisha  ufahamu zaidi wa utamaduni wa kiyahudi ili kuweza kumudu uelewa wa kujielewa sisi wenyewe kwa dhati. Hata mafunzo ya Torah, yaani kitabu kitakatifu cha Wayahudi  ni sehemu msingi na wajibu wa kila mkristo kuelewa. Kutokana na hilo, Baba Mtakatifu Francisko anapendea kukabidhi mchakato wa safari kwa kutafuta maneno katika maombi kwa kila mwamini Myahudi anayosali kila siku baada ya sala ya amidah isemayo: ili iweze kufunguliwa milango ya Toraha , ya hekima , akili na ufahamu, milango ya kumwilishwa na kusaidia, milango ya maisha, ya neema, ya upendo, ya huruma na sifa mbele yao”.

Tujifunze vema Toraha au Pentateuki

Tukumbuke Torah/ Pentateuki inawakilisha vitabu vitano vya kwanza vya Biblia, ikiwa ni kitabu cha Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati.  Vitabu hivyo vinaitwa pia Pentateuki, kutokana na neno la Kigiriki linalomaanisha “buku lenye vitabu vitano.” Torati iliandikwa na Musa, kwa hiyo inaitwa “kitabu cha sheria ya Musa.” (Yoshua 8:31; Nehemia 8:1) Ni wazi kwamba awali kilikuwa kitabu kimoja lakini kikagawanywa baadaye ili iwe rahisi kukitumia. Toh·rahʹ inatumiwa pia kuwakilisha sheria ambazo Waisraeli walipewa kuhusu jambo fulani hususani, kama vile, “sheria ya toleo la dhambi,” “sheria juu ya ukoma,” na “sheria kumhusu Mnadhiri.”​ (Mambo ya Walawi 6:25; 14:57; Hesabu 6:13). Torahʹ nyakati nyingine huwakilisha maagizo na mafundisho, iwe ni kutoka kwa wazazi, watu wenye hekima, au kutoka kwa Mungu mwenyewe.​ ( Rej Methali 1:8; 3:1; 13:14; Isaya 2:3).

Kwa maana hiyo Torati, au Pentateuki inaelezea istoria ya jinsi Mungu alivyoshughulika na wanadamu kuanzia uumbaji hadi kifo cha Musa (Rej Mw1:​27, 28; Kumbukumbu la Torati 34:5). Masharti ya Sheria ya Musa. (Kut 24:3) Sheria hiyo imefanyizwa kwa zaidi ya masharti 600. Inayojulikana zaidi kati ya hizo ni ile inayoitwa Shema, au ungamo la imani ya Wayahudi. Sehemu moja ya Shema inasema: “Lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote.” (Kumb la Torati 6:4-9) Yesu aliifafanua kuwa “amri iliyo kuu na ya kwanza.”​(Mt 22:36-38). Na Jina la Mungu, linapatikana mara 1,800. Badala ya kuwazuia watu wasitumie jina la Mungu, Torati ina amri zilizowataka watu wa Mungu watamke jina hilo. (Hesabu 6:​22-​27); (Kumb la Torati 6:​13; 10:8; 21:5) Kutokana na maelezo hayo machache Wayahudi wanatumia Torah katika mafundisho yao.

 

16 January 2019, 13:29