Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu akibariki waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI wakati wa Katekesi yake tarehe 16 Januari 2019 Baba Mtakatifu akibariki waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI wakati wa Katekesi yake tarehe 16 Januari 2019  (ANSA)

Papa Francisko anasisitiza kuwa mkristo asali kama mtoto mdogo!

Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu Jumatano tarehe 16 Januari 2019,katika mwendelezo wa ufafanuzi wa Sala ya BabaYetu, anakumbusha kuwa Mungu siyo Baba Yetu tu, lakini pia ni kama mama hasiyechoka kamwe kupenda kiumbe chake, hivyo ni kusali kama mtoto mdogo anavyomwambia baba yake

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuendelea na katekesi kuhusu Baba Yetu. leo kwa ni  kuanza  kutazama katika Agano la Kale linaonesha kuwa, sala ilikuwa inazama kwa kina  hadi kufikia kufanya neli liwe moja  la Aba yaani Baba.  Tumesikiliza anachoandika Mtakatifu Paulo katika Barua yake kwa Warumi:“Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana ambao kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba  (Rm 8,15).

Ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 16 Januari 2019 wakati wa katekesi yake kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika ukumbi wa  Paulo wa VI, katekesi yake ni mwendelezo wa ufafanuzi wa Sala ya Baba Yetu. Ambapo katika tafakari hii ameongozwa na Neno la Mungu kutoka kwa Mtakatifu Paulo kwa Warumi lisemalo: “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambao kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; (Rm8,14-16. Baba Mtakatifu akiendelea na ufafanuzi huo anasema Mtume Paulo kwa Wagalati pia anasema:” Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, ni kwamba Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. (Gal 4,6).

Maombi ya Mtakatifu Paulo yanarudia mara mbili kuonesha mapya ya Injili

Maombi hayo yanarudiwa mara mbili, ambapo yanajikita kwa kina kusisitiza mapya yote ya Injili. Mara baada ya kumjua Yesu na kumsikiliza mahubiri yake, Mkristo hawezi kufikiria tena Mungu kama mtu wa kuogopa, hana hofu tena, bali nahisi kuchanua katika moyo wake ile imani kwake. Na kwa uthibitisho ya kwamba inawezakana kuzungumza na Muumba na kumwita “Baba”. Hiyo ni tafsiri muhimu sana kwa wakristo ambao daima wahifadhi mtindo wa asili yaani wa kusema  Aba, Baba, Mtakatifu amethibitisha! Ni nadra kuona kwamba katika maneno ya Aramaiki kwenye Agano Jipya hayatafsiriwa kwa lugha ya Kigiriki. Tunapaswa kufikiria kuwa maneno hayo ya kiaramaiki yamebaki kama yalivyorekodiwa sauti ya Yesu mwenyewe. Na kwa maana hiyo waliheshimu lugha ya Yesu. Katika neno la kwanaza la Baba Yetu tunakutana kwa haraka na mzizi wa mapya ya sala ya kikristo.

Hiyo haihusu lakini kutumia ishara moja, kwa maana ya kwamba sura ya baba ifungamane na fumbo la Mungu; badala yake ni kujaribu kupata ile  sura kamili  ya dunia ya Yesu aliyokuwa anapitia ndani ya moyo wake. Iwapo tutatimiza operesheni hiyo, Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba, tunaweza kusali kwa dhati sala ya “Baba Yetu”. Na ndiyo tazama mwingine alitoa ushauri wa kutafasiri neno la kiaramaiki asili ya Aba na Baba. Kwa maana hiyo sisi sote tunaendelea kusema Baba yetu, lakini katika moyo tunaalikwa kusema Aba kwa maana ya kuendelea kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu kama ule wa mtoto mdogo na baba yake anayemwita aba. Kwa hakika kielelelezo hicho kinaonesha ule upendo na joto, jambo ambalo linaonesha mantiki ya umri wa uchanga.

Sura ya mtoto mdogo aliyepakatwa na baba yake

Sura ya mtoto mdogo aliyepakatwa katika mikono ya baba ambaye anahisi upendo mkuu kwa ajili mwanae. Na ndiyo Baba Mtakatifu anashauri kwamba ili kuweza kusali vema ni lazima kufikia hatua ya kuwa na moyo kitoto. Siyo kuwa na moyo wa kujitosheleza, kwa maana huo hauwezi kusali vema bali ni kuwa kama kweli mtoto akiwa katika mikono ya baba yake. Hata hivyo Baba Mtakatifu anasema  kwamba ni Injili unayoonesha vema maana ya neno hili. Je ina maana gani neno hili kwa Yesu ? Baba Yetu inachukua maana kamili kutiwa joto iwapo tunajifunza kusali mara baada ya kusoma, kwa mfano  kuhusu simulizi la baba mwenye huruma katika sura ya 15 ya Mwinjili Luka (Lk 15,11-32). Tufikirie sala hii aliyosema mwana mpotevu, mara baada ya kufanya uzoefu wa kukumbatiwa na Baba yake aliyekuwa akimsubiri kwa muda mrefu, baba ambaye hakukukumbuka tena maneno ya kukatisha tamaa aliyokuwa ameelezwa na mwanae, ni Baba ambaye  sasa anamfanya atambue ni kwa jinsi gani amemkosa sana.

Kwa kufanya hivyo, tutaweza kugundua kwa jinnsi gani maneno hayo yanakuwa ni maisha na kutoa nguvu kwa kujiuliza, je inawezekana kweli Mungu kujua  tu upendo peke yake? Je wewe unajua chuki? Lakini Mungu angeweze kujibu hapana, mimi ninatambua upendo tu. Je  mahali ambapo ndani kuna kulipiza kisasi, kiburi cha kutaka haki, hasira kwa ajili kudharauliwa sifa? Na Mungu angeweza kujibu: mimi nitambua upendo tu. Baba Mtakatifu Francisko akifafanua zaidi anasema, katika historia hiyo kuna aina nyingi za kuweza kufanya jambo lolote ambalo linakumbusha moyo wa mama. Ni mama mara nyingi wanaowaomba msamaha watoto wao, wanaofunika ili wasivunje uhusino wao na kuendelea kuwatakia mema hata kama hawastahili lolote. Ni kutamka neno kama ili tu, Aba ili uweze kuendeleza sala ya kikristo. Mtakatifu Paulo katika barua zake anafuata njia hiyo hiyo na haiwezekani kuwa tofauti kwa sababu ni njia aliyofundisha Yesu na katika maombi hayo kuna nguvu inayovutia mambo mengine katika maombi.

Mungu anakutafuta hata kama wewe humtafuti

Mungu anakutafuta hata kama wewe humtafuti. Mungu anakupenda hata kama wewe unamsahau. Mungu anaelewa uzuri uliopo kwako hata kama wewe unafikiri kwamba umeweza kutumia talanta zako zote hovyo. Mungu siyo baba peke yake bali ni kama mama ambaye haishi kamwe kupenda kiumbe chake. Kwa upande mwingine kuna hata kipindi cha kuchukua mimba kinachodumu daima zaidi ya miezi tisa ya kawaida; Ni kipindi cha kuchukua mimba na ambacho kinatoa mzunguko wa upendo usioisha.  Kwa mkristo kusali ni kama kusema kwa urahisi Aba, yaani Baba, lakini kwa imani kama ya mtoto mdogo.

Hata kama tumepoteza njia na kwenda mbali na Mungu tunaweza kuanza upya

Inawezekana sisi haya ikatokea kutembea katika njia za mbali na Mungu, kama ilivyomtokea mtoto mpotevu; vilevile hata kuanguka katika upweke ambao utufanya tuhisi kuachwa peke yetu katika dunia, au zaidi kukosea  na kubaki na dhamiri mbaya ya makosa. Katika kipindi hicho kigumu, tunaweza kupata nguvu mpya kwa  kusali na kuanza na neno la Baba, lakini kwa kulitamka na maana kuu, kama ile ya mtoto mchanga amwitaye aba, yaani Baba. Yeye hataficha uso wake.

Vile vile Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba, ni kukumbuka vizuri, labda kuna mwingine amejazwa na mambo mabaya rohoni mwake, mamoa ambayo hajuhi namna ya kupata suluhisho, au  uchungu mwingi wa kutenda  jambo hilo na lile. Lakini Mungu hafichi uso wake. Yeye hatajifungia  kamwe katika ukimya. Wewe mwambie Baba na Yeye atakujibu.  Akitoa mfano amesema, Je wewe unaye baba. Ndiyo lakini ni mbaya, huyo ni baba anayekupenda na hivyo mwambie Baba na uanze kusali namna hiyo katika ukimya, atakwambia ni kwa jinsi gani amekuwa nawe daima. Ndiyo umefanya hili na lile …lakini Yeye atakueleza kuwa, hakupeteza matumaini, na alikuwa anaona kila kitu na kwa maana hiyo atakwamba; “nilibaki daima pale  karibu nawe mwaminifu wa upendo kwa ajili yako”. Ndilo jibu ambalo atatoa, baba Mtakatifu amesisitiza na kumalizia akiomba wasisahau kamwe ili la kusema Baba!

16 January 2019, 15:33