Tafuta

Vatican News
Papa amewaonya Jumuiya ya Wajesuit kuwa makini ya roho ya  malimwengu ambayo ni jambo baya sana Papa amewaonya Jumuiya ya Wajesuit kuwa makini ya roho ya malimwengu ambayo ni jambo baya sana  (ANSA)

Papa:Matunda hayakomai ndani ya mizizi, ni nje yake!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na jumuiya ya Taasisi ya kimataifa ya Yesu (Wajesuit) wakati wanaadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwake na Padre Arrupe, ambapo amewaeleza kuwa jubilei hiyo ni fursa ya neema kwa ajili ya kufanya kumbukumbu. Kadhalika amewaonya kuhepuka na roho ya malimwengu ambayo ni jambo baya sana!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuundwa, kukua na kukomaa ndiyo maneno matatu aliyotumia Baba Mtakatifu Francisko na kuwakabidha hotuba aliyokuwa ameiandaa kwa ajili ya jumuiya ya Taasisi ya kimataifa ya Yesu ( Wajesut) mjini Roma aliokutana nao katika ukumbi wa mkutano mjini Vatican tarehe 3 Desemba 2018. Baba Mtakatifu na wanajumuiya hao amezungumzia juu ya historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, iliyoundwa kunako mwaka 1958 na Padre Arrupe mjesuit na ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika kuanzia mwaka 1965 hadi 1983. Amezungumzia juu ya utume wa Shirika la Wajesuit,na kuthibitisha kuwa Jumuiya ni mahali pa kukuza vichipukizi ambavyo vinaletwa kutoka ulimwenguni kuja Roma na kutoka Roma kupeleka vichipukizi hivyo katika dunia, kwa maana hiyo ni shirika katika moyo wa Kanisa na Kanisa katika moyo wa shirika.

Kujifunza na kuunda

Ili kuweza kufanya kumbukumbu ya taasisi hiyo, Papa Francisko anakumbusha kuanzia katika mizizi yenye msimamo na ambayo matokeo ni kuweza kukua, kwa njia hiyo amewambia kwamana, wao wanaishi katika nyumba ambayo mtakatifu Ignatius aliishi, aliandika kanuni na kuwatuma wafuasi wake wa kwanza katika utume duniani, na kwa jinsi hiyo wao wanakaa katika asili hiyo. Ni neema kwa miaka hii katika mji wa Roma, ni neema na msingi wake wa asili (…), na anawaalika katika miaka hii ili  kukua na kusimika mizizi yao (…) Kuwa na mizizi maana yake ni  kuwa na moyo wa ukarimu ambao Mungu anawajalia na kuweza kuupanua.

Hakuna ukomavu bila majaribu

Baba Mtakatifu akiendela kutazama majaribu ya maisha na ndipo amekuwa na mtazamo wa hatari ambao unaweza kugusa mchakato wa kukua. Ameelekeza ubaya wa hatari kwamba; kukua na kusimika  mizizi maana yake ni kupambana bila mwisho dhidi ya malimwengu yanayoshambulia roho na ndiyo kwa upande wake kwamba ni mbaya sana kwa mujibu wa Padre Lubac. Iwapo malimwengu yanashambuli mizizi, matunda na mti wake wenyewe unanyauka. Kwa maana hiyo  anathibitisha, hiyo ndiyo hatari yenye nguvu katika nyakati hizi, ulimwengu u naoshambuliaroho na kupelekea kujiona katika hali ya ukuhani ukuhani. Na iwapo ukuaji huo utateklezwa  katika kupambana dhidi ya ubinafsi, ndipo matunda yanaweza kutokea.

Uhuru na utii ni ishara za kukua vema kiroho

Ishara mbili chanya za makuzi mema ni uhuru na utii. Hizi ni fadhila nzuri iwapo zinatembea pamoja, uhuru unotokana na Roho Mtakatifu ni uhuru binafsi. Ni uhuru ambao unafuata mfano wa Yesu, Baba Mtakatifu amesisitiza. Roho wa Mungu anazungumza kwa kila mmoja katika uhuru kwa njia ya hisia na mawazo; huwezi kujifungik binafsi, bali kujiundia ndani ya moyo na kutembea kama wana walio huru na si watumwa. Baba Mtakatifu anawawatakia matashi mema ya kwamba wawe  na uhuru na ambaoo wanaungana pamoja japokuwa ni tofauti na kila siku wakipambania kupata huru ulio mkubwa zaidi hasa wa kuondokana na ubinafsi (…) “Kama alivyokuwa Yesu, hata sisi chakula cha maisha ni kufanya mapenzi ya Baba na mababa  wa Kanisa anaotupatia.

Kukomaa ni kuweza kukaa kila mahali, hata katika makambi magumu

Kukomaa kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko maana yake ni kufanya umisionari. Amekumbusha hotuba ya Mtakatifu Paulo VI kunako mwaka 1973 ambapo Baba Mtakatifu ametaja kwamba ni ujumbe wa kina zaidi kwa ajili ya Shirika la Wajesuit. Ujumbe huo unaisisitizia wanashirika wa kijesuit kuwapo kila mahali katika Kanisa hata katika katika makambi magumu. Matunda hayakomai katika mizizi na  katika kisiki, bali yanapotoa matunda yake nje na kufanya mbegu mpya ipandwe tena ardhini. Na ndipo hapo kuna kazi ya kimisionari, kwenda moja kwa moja kwenye hali halisi ya leo hii na kutoa huduma katika dunia ambayo Mungu anapenda.

Msiwe na hofu ya matatizo

Baba Mtakatifu anawaalika wapelembele mbele Msalaba na Ekaristi ya mateso ambayo ni ushuhuda pamoja na huduma ya Neno la kama hatua muhimu ya kitulizo. Anawaalika kuchukua mizigo ya wengine, lakini  si kubeba mizigo ya wadhaifu tu,  lakini hata historia mbalimbali za utamaduni na kumbu kumbu za watu.

03 December 2018, 14:40