Cerca

Vatican News
Papa: Sala ya Malaika wa Bwana Papa: Sala ya Malaika wa Bwana   (ANSA)

Papa:kipindi cha Majilio ni kusubiri pia Utukufu wa Kristo!

Basi,jiangalieni,mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla. Ndiyo mbiu iliyosikika ya Yesu katika Injili ya Jumapili ya kwanza ya Majilio na ili kuweza kukesha na kuomba katika kusubiri ujio wake Bwana Yesu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Leo tuaanza majilio, kipindi ambacho ni cha kiliturujia kinacho tuandaa katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na kuinua mitazamo yetu tukifungua  mioyo ili kumpokea Yesu. Kipindi cha majilio si kukiishi katika kusubiri kuzaliwa kwa Bwana tu; tunakiishi wakati tunaalikwa  kuwa na matarajio ya Utukufu wa Kristo, yaani  siku ile itakapowadia ya kurudi kwake. Ni kujiandaa ili kukutana na Yeye siku ya mwisho ukiwa na uchagizi wa kweli na ujasiri. Katika kukumbuka siku ya Kuzaliwa kwa Bwana, ni matarajio ya kurudi kwa Utukufu wa Kristo, na hata kwa ajili ya kukutana sisi binafsi; ni katika siku ambayo Bwana anatuita. Katika Wiki nne, sisi tunaalikwa kubadilika kwa namna tunavyoishi na ukawaida  wa kuweza kukuza matumaini na kukuza zile ndoto za wakati endelevu. Huo ndiyo mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji wote waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro, mjini Vatican, siku ya Jumapiliti tarehe 2 Desemba 2018, wakati Mama Makanisa, anaanza kipindi cha Majilio, ikiwa ni Jumapili ya kwanza ili kuweza kujiandaa kumpokea Bwana Yesu.

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari hiyo anasema: Injili ya Jumapili kutoka (Lk 21,25-28.34-36) inajikita katika mwelekeo huo kwa dhati na kuhimiza  kuwa makini  ili kuachilia mbali na ile  mitindo ya maisha ya ubinafsi au ukawaida wa kukimbizana kila siku. Maneno ya Yesu yanajikita hasa kwa namna ya pekee akisema: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla, (...) Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu”, (Lk 21,34.36).

Ni kipindi mwafaka cha kufungua mioyo yetu ili kuweza kujiuliza jinsi gani tunatumia muda wetu kwa ya maisha

Kukesha na kuomba ndiyo njia ya kuishi katika kipindi kinacho anza leo hii hadi siku ya Kuzaliwa kwa Bwana. Usingizi wa kina unazaliwa kutokana na kuzungukia daima sisi binafsi na kujifungia na maisha binafsi kutokana na matatizo, furaha na uchungu, lakini daima ni kujizungukia binafsi. Uchovu huo na kuboa huko ni kutoakana na kujifungia matumaini. Na ndipo inapatikana mizizi ya usingizi mzito na uvivu unaozungumzwa na Injili.  Kipindi cha Majilio kinatualika katika jitihada za kukesha na kutazama nje yetu binafsi kwa kupanua akili na moyo ili kujfungulia mahitaji ya watu, ndugu na matashi ya ulimwengu mpya. Ni matashi ya watu wengi wanaosumbuka kwa njaa, ukosefu wa haki na vita; ni ustashi wa maskini, wadhaifu , na walioachwa peke yao. Hiki ni kipindi mwafaka cha kufungua mioyo yetu ili kuweza kujiuliza kwa dhati juu ya jinsi gani tunatumia muda wetu katika  maisha.

Mtindo wa pili wa kuweza kuishi vema kipindi cha matarajio ya Bwana ni kusali

Tabia ya pili ya kuweza kuishi vema kipindi cha matarajio ya Bwana ni kile cha sala: “Changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia”inaonya Injili ya Mtakatifu Luka. Hiyo ina maana ya kukuamka na kusali, kulekeza mawazo na mioyo ywetu kwake Yesu ambaye anakuja.  Kwa kuwada tunaamka tukiwa tunasubiri jambo au mtu. Tunamsubiri Yes una tunataka kumsubiri kwa sala ambaye inafungamana na kukesha. Ksali na kusubiri Yesu, kujifungia kwa wengine , kukaa na kuesha na siyo kujifungia sisi binafsi, Baba Mtakatifu anahimiza. Akiongeza anasema, lakini iwapo katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ni kufikiria kutumia, na kununua yaani ni kitu gani ninaweza kununua hiki na kile cha ulimwengu, Yesu kwa hakika hatapita na wala hatutampata. Sisi tunasubiri Yes una tunataka kumsubiri kwa sala ambayo inafungamana na kukesha anahimiza Papa!

Upeo matarajio ya sala ni upi?

Baba Mtakatifu ameuliza swali: je upeo wa matarajio ya sala ni upi? Matarajio ya upeo huo yanaelekezwa na Biblia hasa katika sauti ya manabii. Baba Mtakatifu anataja nabii aliyetajwa katika somo la siku, ambaye ni Yeremia, aliyezungumza na watu wakati wa majaribu ya uhamishoni na walio kuwa katika hatari ya kupoteza utambulisho wao binafsi. Hata sisi kama wakristo, japokuwa ni watu wa Mungu, Baba Mtakatifu anabainisha kwakba ipo hatari ya kubobea katika ulimwenfu na kupoteza utambulisho wetu na zaidi kuwa kuwa wapagani.

Kutokana na hilo, tunahitaji Neno la Mungu kwa njia ya nabii anayetangaza: “ Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapolitimiza neno lile jema nililolinena, katika habari za nyumba ya Israeli na katika habari za nyumba ya Yuda. Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii” (Yer. 33:14-15). Baba Mtakatifu anahitimisha tafakari hiyo akithibitisha kuwa: “Chipukizi la haki ni Yesu, ni Yesu anayekuja na ambaye tunamsubiri. Bikira Maria anayetuletea Yesu ni mama wa kukesha na kuomba, anatusaidia kuongeza nguvu ya matumaini yetu katika ahadi ya Mwanaye Yesu, ili tuweze kufanya uzoefu ambao kwa njia ya historia ya mateso Mungu anabaki mwaminifu daima na anasaidia katika makosa ya kibinadamu kwa kuonesha huruma yake.

03 December 2018, 10:23