Tafuta

Vatican News
Papa Francisko: Mtoto Yesu ni kiini cha Sherehe za Noeli. Papa Francisko: Mtoto Yesu ni kiini cha Sherehe za Noeli.  (Vatican Media)

Papa Francisko: Kristo Yesu ndiye kiini cha Sherehe za Noeli

Baba Mtakatifu Francisko katika Siku kuu ya Mtakatifu Stefano; Shemasi na Shahidi, 26 Desemba 2018, amewakumbusha waamini kwamba, Mtoto Yesu ndiye kiini cha Sherehe za Noeli, asaidie kukuza na kudumisha udugu, ushirikiano na mshikamano katika familia na jumuiya mbali mbali za waamini!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano, tarehe 26 Desemba, Siku kuu ya Mtakatifu Stefano Shemasi na Shahidi, aliwatakia heri na baraka waamini na mahujaji wote kutoka ndani na nje ya Italia, wakati huu wanapoendelea kumtafakari Mtoto Yesu katika maisha yao! Amewakumbusha waamini kwamba, Mtoto Yesu ndiye kiini cha Sherehe za Noeli, asaidie kukuza na kudumisha udugu, ushirikiano na mshikamano katika familia na jumuiya mbali mbali za waamini!

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwashukuru waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema sehemu mbali mbali za dunia, waliomtumia salam na matashi mema ya Sherehe za Noeli na Mwaka Mpya 2019. Anasema, si rahisi kwake, kuweza kuwajibu watu wote hawa, lakini hawa wote anawahifadhi na kuwakumbatia katika sala na sadaka yake. Anapenda kuwaonesha moyo wake wa shukrani wale wote waliompatia na wale ambao wameahidi kuendelea kumsindikiza kwa njia ya sala katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Papa: Shukrani

 

 

26 December 2018, 15:36