Tafuta

Papa amewasalimia watoto wote wa Roma ambao kama utamaduni walikuwa na sanamu ndogo za kubarikiwa kabla ya kuziweka katika pango dogo katika nyumba zao Papa amewasalimia watoto wote wa Roma ambao kama utamaduni walikuwa na sanamu ndogo za kubarikiwa kabla ya kuziweka katika pango dogo katika nyumba zao 

Papa anakabidhi kwa Mungu malengo ya mkataba wa uhamiaji!

Baba Mtakatifu anashukuru saini ya mkataba kuhusu uhamiaji, maana chombo hicho kinaweza kufanya kazi kwa uwajibikaji,mshikamano na uhuruma mbele ya yule ambaye kwa sababu moja au nyingine amelazimika kuacha nchi yake. Amebariki pia sanamu ndogo za Yesu zilizoletwa na umati wa watoto wengi kutoka Roma

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wiki iliyopita, umetiwa saini Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhamiaji huko Marrakech Morocco wa usalama na mpangilio kwa ajili ya jumuiya nzima ya kimataifa. Baba Mtakatifu anashukuru kwamba chombo hicho kinaweza kufanya kazi kwa uwajibikaji, mshikamano na uhuruma mbele ya yule ambaye kwa sababu moja au nyingine amelazimika kuancha nchi yake. Baba Mtakatifu anakabidhi malengo hayo yote katika sala za waamini wote.

Kubariki sanamu ndogo za Yesu kwa ajili ya pngo la kila nyumba

Ametamka  maneno hayo  Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Domenika 16 Desemba 2018, kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Mjini Vatican.  Kadhalika Baba Mtakatifu amewasalimia watoto wote wa Roma ambao kama utamaduni walikuwa na sanamu ndogo za kubarikiwa kabla ya kuziweka katika pango dogo katika nyumba zao. Baba Mtakatifu anasema watakapojikusanya pamoja mbele ya pango, kwa kutazama Mtoto Yesu, watahisi mshangao.

Swali nini maana ya mshangao

Lakini swali la kujiuliza, nini maana ya mshangao? Akijibu amesema: Ni hisia ya nguvu na zaidi ya hisia za kawaida. Ni kuona Mungu. Ni mshangao mkubwa wa fumbo la Mungu aliyejifanya mtu; ni Roho wa Mungu ambaye ataweka ndani ya moyo unyenyekevu, huruma na wema wa Yesu. Yesu ni mwema, Yesu ni mpole. Yesu ni mnyenyekevu. Hiyo ndiyo kweli sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana! Amehimiza kwa kusema Msisahau! ….Kwa maana hiyo ameongeza: “iwe kwenu na kwa ajili ya familia”. Baba Mtakatifu amewabariki wote na sanamu ndogo za Yesu na kuwatakia sikukuu njema na Majilio mema.

17 December 2018, 10:29