Tafuta

 24.11.2018 Papa Francisko amekutana na washiriki wa mkutano wa III Kimataifa wa Tamasha la kwaya mjini Vatican 24.11.2018 Papa Francisko amekutana na washiriki wa mkutano wa III Kimataifa wa Tamasha la kwaya mjini Vatican 

Wimbo na muziki ni nyenzo za uinjilishaji na siyo kujionesha!

Katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, tarehe 24 Novemba, Baba Mtakatifu Francisko,amekutana na washiriki wa Mkutano wa III kimataifa wa Tamasaha la Kwaya, amewashauri wawe karibu na watu daima katika kipindi cha furaha na uchungu, wakati huo huo wajiangalie ili wasiangukie katika kishawishi cha kujionesha badala ya kuinjilisha

Sr. Angela Rwezaula

Uwepo wenu katika Ukumbi huu umewezesha kupiga vyombo vya  muziki na nyimbo na ambao kwa namna nyingine vimekwenda zaidi ya kuta hizi, na kweli Mmeamsha Vatican! Ni vema kusiliza sauti zenu mzuni na kuonja furaha na jitihada zenu katika sauti ya pamoja wakati wa sala zetu. Ninamshukuru Askofu Mkuu Rino Fisichella kwa ubunifu wake, hotuba yake na kuruhusu kugusa kwa dhati njia nyingi za uinjilishaji. Ni mwanzo wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa kukutana na washiriki wa mkutano uliounganisha wanamuziki, kwaya za majimbo na maparokia kutoka pande za  duniani kote katika mkutano ulioanza tarehe 23-25 Novemba 2018 kwenye ukumbi wa Paulo VI , ikiwa ni toleo la III tangu kuazana Mkutano wa Kimataifa wa tamasha la kwaya katika fursa ya kuadhimisha Siku kuu ya Mtakatifu Cecilia, iliyo andaliwa na Baraza la Kipapa la uinjilishaji mpya kwa ushirikiano wa Chama cha Nova Opera, ambapo imeona washiriki zaidi 8,000 kutoka mabara yote duniani.

Sinodi ya vijana ilizungumzia juu ya wimbo katika liturujia

Baba Mtakatifu amesema katuka siku zilizopita kama wajuavyo imefanyika Sinodi ya Maakofu kwa ajili ya vijana na mada hiyo imekuwa muhumu hasa kwa kujita katika suala la muziki. Umuhimu wa muziki unawakilishwa na mazingira ya kweli ambayo vijana mara nyingi wamejikita na  kweli, kama vila utamaduni na lugha ambayo inaweza kuboresha liturujia  hata kuwa rasimlia ya kichungaji inayowaalika kwa namna ya pekee katika liturujia na upyaishowake. (Hati n 47). Muziki wao na nyimbo zao ni zana za kweli za uinjilishaji  katika kipimo ambacho wanatoa ushuhuda wa kina wa Neno la Mungu linalogusa moyo wa mtu, na kuruhusu maadhimisho ya sakramenti, kwa namna ya pekee wa Ekaristi Takatifu, ambayo inafanya uonje na kutambua uzuri wa Mbingu, Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha.

Katika kipindi cha furaha na uchungu, Kanisa linaalika kuwa karibu na watu

Baba Mtakatifu anatoa ushauri kwa washiriki hao kuwa:“kamwe msisimame katika shughuli hii muhimu kwa ajili ya maisha ya jumuiya zenu; kwa namna hiyo katika nyimbo  mnatoa msisimko ambao kwa kina umo ndani ya kila mtu. Katika kipindi cha furaha na uchungu, Kanisa linaalika kuwa karibu na watu daima ili kuweza kuwasindikiza katika imani. Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ni mara ngapi muziki na nyimbo vinasaitia katika kipindi  maalum cha maisha ya watu, ili waweza kuendelea kuhifadhi kama kumbukumbu msingi ambayo imejitokeza katika maisha yao.

Mtaguso wa Vatican II ulipokuwa katika mchakato wa upyaisho  wa liturujia  ulisema kuwa “muziki wa utamaduni wa Kanisa inaunda urithi wa thamani ya juu” (Cost. Sacrosanctum Concilium, 112). Na hiyo ni kweli, Baba Mtakatifu anabainisha na kuongeza kusema, kwa namna ya pekee tamaduni nyingi za jumuiya zilizo katika dunia nzima, ambao wanafanya kuonesha mtindo na ambao umesimikwa mzizi wake katika utamaduni wa watu na kugeuka kuwa sala ya kweli. Ibada hizo za watu, zinatambua kusali kwa ubunifu na kutambua kuimba kwa ubiunifu, kama alivyosema Askofu mmoja wa Italia kuwa ni mfumo wa jumuiya ya Kanisa. Wimbo unasaidia katika toba. Kwa njia ya muziki na nyimbo, vinatoa sauti ya sala na kwa namna ya pamoja kuunda kwaya ya kimataifa mahali ambapo sauti moja inakwenda kwa Baba, katika sifa na utukufu wa watu wake.

Muungano wao unafanya Kanisa la ulimwengu na tamaduni zake

Baba  Mtakatifu amebainisha kuwa uwepo wao na muungano huo wa kimataifa, unapokelewa kama Kanisa la ulimwengu na tamaduni zake. Nyimbo zao na muziki wao kwa namna ya pekee katika maadhimisho ya Ekaristi yanafanya  mwili na katika kuimba sauti moja ya imani yetu. Hata kama wanazungumza lugha tofauti, lakini wanaweza kuelewa muziki ambao wanaimba na imani wanayosadiki na matumaini yanayotarajiwa. Aidha Baba Mtakatifu amesema wao wanasoma na kijiandaa katika wimbo na sauti ambazo zinasaidia katika sala na maadhimisho ya liturujia, lakini zaidi wasiangukie katika vishashi vya kujiona na ambavyo vinazima shughuli yao na kuwanyanyasa ambao wanashiriki sala. Kwa kusisitiza zaidi, Baba Mtakatifu anahimiza wasifanya hivyo. Wawe viongozi wa nyimbo kwa mkutano mzima na wasiwakoseshe watu wa Mungu kuimba na wao na kutoa ushuhuda wa sala ya Kanisa na ya jumuiya.

Thamanisha urithi wa dini na ibada za nyimbo za kizamani

Katika hilo, Baba Mtakatifu ameonesha juu ya masikitiko yake kwa baadhi ya maadhimisho, kwamba inawezekana kuona wengine  wanaimba vizuri, lakini watu hawawezi kuimba kile ambacho wanakwaya wanaimba, kutokana na hili anathibitisha,  kwa kuwa wao wametambua umuhimu wa wimbo  na muziki wasidharau tafsiri nyingine za roho ya watu, katika sikukuu ya wasimamizi, maandamano, muziki na nyimbo za dini za watu wa kizamani ambazo ni urithi wa dini ambayo inastahili kuhamasishwa na kusaidiwa kwa sababu daima ni matendo ya Roho Mtakatifu katika moyo wa Kanisa. Na Roho katika wimbo atusaidie kwenda mbele. Kwa njia hiyo, muziki ni chombo cha umoja ili kuifanya Injili iwe ya dhati katika dunia ya leo, kwa njia ya uzuri ambao bado unavutia na unafanya uwezekano wa kuamini kwa kutegemea  msaada wa upendo wa Baba. Baba Mtakatifu anahitimisha: “ninawasindikiza kwa baraka yangu na kuwakabidhi kwa Mtakatifu Cecilia, msimamizi wenu, lakini zaidi msisahau kusali kwa ajili yangu hata kwa njia ya wimbo wenu”.

24 November 2018, 15:00