Tafuta

Vatican News
Nia ya maombi kwa mwezi ni huduma ya amani Nia ya maombi kwa mwezi ni huduma ya amani 

Papa:nia ya maombi Novemba ni kwa ajili ya huduma ya amani!

Nia ya sala ya Baba Mtakatifu kwa njia ya video kwa mwezi Novemba 2018 ni kwa ajili ya kuombea huduma ya amani, hivyo Papa anasema: “Tusali pamoja ili lugha ya moyo na mazungumzo viweze kushinda daima lugha ya silaha”

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika nia ya maombi ya kila mwezi, hata katika mwezi Novemba 2018, Baba Mtakatifu anawaomba watu wote wajikite kusali kwa ajili ya huduma ya amani, kwa maana watu wote wanahitaji amani na wanatesema kutokana na ukosefu huo.

Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa njia ya video  mwezi huu anasema:  “Wote tunataka amani. Ni jambo ambao linatakiwa zaidi ya kitu kingine na kufanya uteseke kutokana na ukosefu wake”. “Tunaweza kusema maneno mazuri sana, lakini iwapo ndani ya moyo wetu hakuna amani, haitakuwapo hata katika dunia".

Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kusema: "Kwa kusitisha kutumia nguvu hadi kufikia ziro na asilimi 100% ya huruma, tujenge amani ya kiinjili ambayo haibagui hata mmoja" .Na tusali pamoja ili lugha ya moyo na ya mazungumzo viweze ushinda daima lugha ya silaha”.

06 November 2018, 13:43