Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemwandikia barua Mama Filomena Lamberti barua ya kuomba msamaha baada ya kumwagiwa tindikali na mumewe! Papa Francisko amemwandikia barua Mama Filomena Lamberti barua ya kuomba msamaha baada ya kumwagiwa tindikali na mumewe!  (ANSA)

Barua ya Papa Francisko kwa Filomena aliyemwagiwa tindikali na mumewe!

Mama Filomena Lamberti alimwagiwa tindikali na mumewe Vittorio Giordano, akafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kupatikana na hatia! Baada ya kutumikia adhabu yake kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu, sasa ameachiwa huru, lakini madhara kwa Mama Lamberti bado ni makubwa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemwandikia barua Mama Filomena Lamberti, aliyemwagiwa tindikali na mumewe, akiomba samahani na msamaha kwa niaba ya wale wote wasiokuwa na ujasiri wa kuomba msamaha kutokana na kuelemewa sana na utamaduni wa kutowajali na kuwathamini watu wengine. Baba Mtakatifu alikua anatoa shukrani kwa Mama Filomena Lamberti baada ya kumtumia kitabu “Maisha mapya. Si hadithi ya kusisimua bali ni ujasiri wa ushuhuda, kilichochapishwa mwaka 2017. Sehemu ya kitabu hiki imesomwa kwenye matangazo ya Kituo cha Televisheni cha taifa la Italia, Rai Uno, Jumapili, tarehe 25 Novemba 2018, Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake.

Ukatili unasababisha simanzi isiyoelezeka, huumiza familia kutoka kizazi kimoja hadi kingine na kushusha kiwango cha maisha ya familia. Ukatili huo husababisha wanawake washindwe kufikia viwango vya juu vya utendaji wao, unadhibiti ukuaji wa uchumi na kudumaza maendeleo endelevu na fungamani. Mama Filomena Lamberti alimwagiwa tindikali na mumewe Vittorio Giordano, akafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kupatikana na hatia! Baada ya kutumikia adhabu yake kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitatu, sasa ameachiwa huru, lakini madhara kwa Mama Lamberti bado ni makubwa!

Baba Mtakatifu anapenda kumhakikishia Mama huyu kwamba anasali na kumwombea, ili ujasiri wa ushuhuda ambao ameuonesha uwe ni fundisho kwa watu wasiojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengine. Kwa miaka 35 Filomena alijinyenyekesha chini ya ulinzi na tunza ya mumewe! Lakini kutokana na wivu akamnyanyasa na kumdharau, kiasi cha kumkandamiza kama soli ya kiatu na kuona maisha yake kama “mahabusu”. Kutokana na mateso haya makali, wakatengana na tarehe 28 Aprili 2012 akamwagia tindikali kiasi cha kumfanya achungulie kaburi!

Papa: Barua
27 November 2018, 09:51