Tafuta

Vatican News
Tarehe 10.11.2018 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa Tarehe 10.11.2018 Papa alikutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa  (ANSA)

Kuelekea Budapest 2020. Papa: Enezeni utamaduni wa ekaristi!

Baba Mtakatifu amekutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kongamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa wakiwa katika maandalizi ya Kongamano hilo litakalo fanyika mjini Budapest tarehe 13-20 Septemba 2020. Amesisitiza juu ya wokovu kuwa ni kisima cha Ekaristi, lazima kuigwa mfano na waamini

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 10 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Kongamano ya Ekaristi Takatifu Kimataifa. Akianza hotuba yake, anawashukuru kufika kwao, wakati wanamalizia mkutano wao Mkuu na kumshukuru Askofu Piero Maein kwa maneno ya hotuba yake.  Kadhalika amewasalimu wawakilishi wa Kimataifa kutoka katika Mabaraza ya Maaskofu duniani kwa namna ya pekee, Wawakilishi wa Kamati ya Hungury walioongozwa na Kardinali Peter Erdő. Baba Mtakatifu anasema, tukio hilo litaadhimishwa katika eneo la Mji Mkuu wa Ulaya, mahali ambapo jumuiya za Kikristo zinasubiri kwa hamu uinjilishi mpya na wenye uwezo wa kukabiliana na mitindo mipya ya kidunia na utandawazi ambao unahatarisha kufuta  historia yenye utajiri na ukuu zaidi.

Je ni ni maana ya kuadhimisha Kongamo la Ekaristi katika mji wa kisasa

Akiendelea na hotuba yake, Baba Mtakatrifu anasema ndipo linajitokeza swali la kujiuliza: je ni ni maana ya kuadhimisha Kongamo la Ekaristi katika mji wa kisasa na wenye tamaduni nyingi ambako Injili na mitindo yake ya kidini imeweka pembeni? Katika kujibu hili swali  amebainisha kuwa: Ina maana ya kushirikishana na neema ya Mungu ili kuendeleza kwa njia ya sala, matendo na utamaduni wa Ekaristi, kwa  maana ya kufikiria na kutenda inayoanzia juu ya Sakramenti, lakini pia inayotambuliwa hata zaidi  ya mipaka yake ya kuhusika katika Kanisa. Katika Ulaya iliyo na ugonjwa wa utofauti na kwa kupitia kipindi cha migawanyiko na kujifungia binafsi, Baba Mtakatifu anasema, wakristo wanapyaishwa hawali ya yote  na  dominika baada ya dominika, ambayo ni ishala rahisi na imani yenye nguvu. Hawa wanakusanyika kwa jina la Bwana kwa kujitambua kuwa ndugu. Na ndipo hapo inarudia miujiza katika kusikiliza Neno na ishala ya Mkate uliomegeka hata ule  ulio mdogo na mnyenyekevu, katika mkutano wa waamini ambao wanageuka kuwa mwili wa Bwana, katika tabernakulo yake duniani. Maaadhimisho ya Ekaristi yanageuka kuwa kama chombo cha kuatamia ile mitindo ambayo inazaa utamaduni wa ekaristi, kwa sababu inatia chachu  na  kusukuma ili kuunda ishara na mtindo wa maisha ya neema ya Kristo ambaye alijitoa yeye binafsi bila kujibakiza!

Tabia ya kwanza ni muungano

Baba Mtakatifu  Francisko akifafanua juu ya tabia za Ekaristi amesema: tabia ya kwanza ni muungano. Katika Karamu ya mwisho, Yesu alichagua Mkate na kikombe cha ndugu kama  ishala ya zawadi yake. Inafuata maadhimisho ya kumbukumbu ya Bwana ambayo yanamwilishwa katika Mwili wake na damu yake ambayo ni muhimu na kujenga muungano na Yeye na muungano na waamini kati yao. Kwa dhati ni changamoto ya  muungano wa Kristo katika uchungaji wa ekaristi, kwa sababu hiyo ni kutaka kusaidia waamini waungane na Yeye ambaye yup  katika maumbo ya  Sakramenti ili kuweza kuishi na Yeye na Yeye katika utume. Hili linachangia kwa nguvu hata utamaduni wa Ekariste, nje ya Misa na kujengwa tangu zamani kipindi muhimu katika shughuli za Kanisa. Sala ya kuabudu, inafundisha kutotengenisha Kristo kiongozi mkuu na Mwili wake, yaani umoja wa sakaramenti na Yeye na ile ya mwili wake na matokeo ya jitihada za kimisionari.

Tabia ya pili ya Ekaristi ni huduma

Baba Mtakatifu akifafananua tabia ya pili  ya Ekaristi anaseama, ni ile ya huduma. Jumuiya ya Ekaristi ikitangaza hatima ya Yesu Mtumishi, inageuka kuwa yenyewe mtumishi, wakati wa kula Mwili uliopewa, hugeuka mwili ulitolewa kwa ajili ya wengi.   Kuendelea kurudi katika chumba juu kbaisa  (Mdo 1,13) umbu la Kanisa , mahali ambapo Yesu waliwaosha miguu mitume wake, wakristo wanatoa huduma kwa sababu ya Injili na kuingia ndani, mahali pa udhaifu na msalaba ili kushirikishana na kuponya. Zipo hali nyingi katika Kanisa na katika jamii, ambazo inawezekana kutia manukato ya huruma kwa matendo ya kiroho na kimwili.  Baba Mtakatifu anazitaja sehemu hizo kuwa: Ni katika familia zenye matatizo, vijana, watu wazima bila ajira, wagonjwa na wazee walio na upweke, wahamiaji wenye shida, na hata umasikini wa aina nyingi. Katika maendeleo hata ya binadamu aliye na majeraha, wakristo wanaadhimisha kumbukumbu ya Msalaba na kufanya Injili  ya mtumishi Yesu ili  iwe hai iliyotolewa kwa upendo. Wabatizwa wanapanda kwa namna hiyo ule utamaduni wa Ekaristi kwa kujifanya watumishi wa maskini, , si kwa jina la itikadi za mawazo, anaonya Papa,  bali kwa ajili ya Injili yenyewe ambayo inakuwa ni kanuni ya maisha binafsi na ya jumuiya. Na huo ni kama ushuhuda usiomegeka wa wimbi la watakatifu wote wa upendo.

Misa hugeuka kuwa maisha ya ekaristi

Na hatimaye baba Mtakatifu anaongeza:  Misa inageuka kuwa maisha ya ekaristi na kupelekwa katika hali ya juu ya Neno la Injili  ambalo katika miji yetu mara nyingi wamesahahu. Anatoa mfano Baba Mtakatifu kuwa: tufikirie tu neno la huruma. Wengi wanalalamikia hata mito iliyojaa umasikini ambao unjikita katika uzoefu wa jamii zetu. Hiyo ni mito mingi ya woga, harara, maneno mengi, ubaya, chuki, kujifungia binafsi, kutojali mazingira na mengine. Wakati huo huo lakini wakristo wanafanya uzoefu wa kila dominika ya kwamba mto huo hauwezi kujaa na kuzidi bahari ya huruma inayoshuka katika dunia. Ekaristi ni kisima cha bahari ya huruma kwa sababu katika hili ni Mwanakondoo wa Mungu aliyechinjwa sadaka  lakini ambaye amesimama na katika ubavu wake uliochomwa mkuki unatoka maji hai na kuendeleza kutoa kwa njia ya mishale ya Roho Mtakatifu  katika uumbaji mpya na unatoa chakula kwenye karamu ya moja ya Bwana (taz barua. ap. Misericordiae vultus, 7). Huruma inaingia hivyo katika ulimwengu na kujenga picha na mjengo wa watu wa Mungu ambao wanafaa katika nyakati za kisasa.

Ekaristi  ni kisima na uwezo wa kujikita hata katika utamaduni wa Ekaristi yenye uwezo wa kuigwa  na watu wenye mapenzi mema

Baba Mtakatifu Francisko anasema: Kongamano lijalo la Ekaristi Takatifu Kimataifa katika kupeleka mbele historia ya makumi sasa, linaalika kuelekeza mchakato wa njia hiyo ya uongofu mpya  na kukumbusha kuwa, kiini cha maisha ya Kanisa ni Ekaristi. Ndiyo Pasaka yake na yenye uwezo wa kueneneza uchanya, si tu kwa kwa ajili ya wabatizwa, bali hata katika mji wa nchi mahali ambapo wanaishi na kufanya kazi. Kwa maana hiyo tukio la Ekaristi Takatifu huko Budapest, linaweza kukuza jumuiya ya kikristo katika mchakato wa upyaisho, kwa sababu ya wokovu ambao katika  Ekaristi  ni kisima na uwezo wa kujikita hata katika utamaduni wa Ekaristi yenye uwezo wa kuigwa  na watu  wenye kuwa na mapenzi mema kwenye  makambi za upendo, mshikamano, amani, familia na utunzaji wa mazingira. Baba Mtakatifu amehitimisha: “Tangu sasa ninalikabidhi Kongamano lijalo la Ekaristi Takatifu  Kimataifa kwa Bikira Maria na ili awasindikize kila mmoja na jumuiya zenu na kufanya kazi zenu ili ziweze kuzaa matunda!

 

10 November 2018, 14:21