Tafuta

Vatican News
Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana tarehe 3 Oktoba 2018 Ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana tarehe 3 Oktoba 2018  (Vatican Media)

Sinodi,Papa Francisko: ni vema kuwa upande wa Kanisa kama mama!

Katika hotuba ya Papa Francisko wakati wa ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu tarehe 3 Oktoba 2018, ameanza kutoa shukrani kwa waandaaji wote wa shughuli hiyo, lakini kwa namna ya pekee vijana wote ambao kwa namna nyingi wameonesha kuwa upande wa Kanisa

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya kutoa shukrani kubwa kwa wote waliojikita katika maandalizi ya Sinodi na kwa namna ya pekee vijana wote ambao wamehisi kuwa upande wa Kanisa, wakati wa hotuba yake ya ufunguzi  wa Sinodi ya Maaskofu iliyoanza tarehe 3 Oktoba 2018, hotuba yake ya kina imejikita kutazama Kanisa kama mama, kama Mwalimu, kama nyumba, kama familia yenye uwezo, licha ya udhaifu wa kibinadamu na matatizo, Kanisa linalong’aa na kuonesha ujumbe usiozama wa Kristo!

Baba Mtakatifu amesema: “Ni vema kushikamana na mashua ya Kanisa ambayo licha ya dhoruba isiyokuwa na huruma katika ulimwengu, linaendelea kutoa kimbilio na ukarimu kwa kila mtu; ni muhimu kujiweka katika kusikiliza kila mmoja; ni vema kuogelea na kwenda kinyume dhidi ya upepo wa kisasa na kufungamana na thamani iliyo ya juu yaani, familia, uaminifu, upendo, sadaka, huruma, na uzima wa milele.

Ujasiri wa kuzungumza

Papa Fransisko, akiendelea kuwakumbusha kuwa “Sinodi ni kipindi cha kushirikishana”, amewashauri, “ wote  wazungumze kwa ujasiri na uwazi , na hiyo “ni katika kuunganisha uhuru, ukweli na upendo”. “Ni katika mazungumzo tu, Papa anaongeza, yanaweza kutufanya sisi kukua”. “Ushauri wa ukarimu na wenye uwazi unajenga na husaidia, wakati huo huo hauleti masengenyo yasiyo na maana, udanganyifu au hukumu”. Kwa ujasiri wa kuzungumza Papa Fransisko anaeleza, inatakiwa uendane na unyenyekevu wa kusikiliza.

Uhuru wa kubadili kile unachokishikilia

Sinodi lazima iwe “zoezi la mazungumzo” na matunda ya kwanza ya majadiliano, Papa anabainisha kuwa , “ kila mtu anangua katika mapya na ili kubadilisha maoni binfasi ambayo ni shukrani kutokana na alivyoweza kusikiliza kutoka kwa mwingine”. Kwa maana hiyo, ameongeza kuomba Papa, hebu tujisikie huru kukaribisha na kuelewa wengine na kwa maana hiyo, kubadili maoni yetu na nafasi zetu ni ishara ya ukuaji mkubwa wa kibindamu na kiroho”.

Mang’amuzi, uwazi na kusikiliza

Sinodi ni zoezi la Kanisa katika kung’amua, kwa maana hiyo, “kuwa na uwazi katika kuzungumza na kujifungua wazi katika kusikiliza ni msingi ili Sinodi iweze kuwa na mchakato wa mang’amuzi”. Papa Fransisko anaendelea kufafanua kuwa, “ Mang’amuzi sio kauli mbiu ya matangazo, sio mbinu ya kiufundi ya shirika na wala kuwa mtindo huu wa kipapa, bali ni tabia ya mtazamo wa mambo ya ndani ambayo imesimika mizizi katika tendo la imani. Mang’amuzi ni njia na wakati huo huo ni lengo ambalo sisi tunajiwekea. Hiyo inatoa msingi ambao sisi tunaamini kuwa Mungu yupo katika shughuli yake, katika historia ya dunia, katika matukio ya maisha, katika watu ambao ninakutana nao na ambao wanazungumza nami. Kwa maana hiyo tumealikwa kujiweka katika usikivu na kusikiliza Roho anashauri nini, kwa namna zipi na njia zipi ambazo hazijulikani. Mang’amuzi kwa maana nyingine, yanahitaji nafasi na muda".

Kanisa kusikiliza na kutembea

Njia ya maandalizi kwa muda huu wa Sinodi - Papa amekumbusha kuwa alikuwa  amesisitiza kuwa  "Kanisa lina  deni la kusikiliza hata mbele ya vijana, ambao mara nyingi huhisi  kuwa kanisa haliwaelewi undani wa asili yao na kwamba hawapokelewi kwa kile ambacho wao wanajionesha kweli na wakati mwingine hata kukataliwa: “Sinodi hii ina fursa, zoezi na wajibu wa kuwa ishara ya Kanisa ambalo kweli linajiweka kitete kusikiliza, ambayo linaacha liulizwe na  wale ambao linakutana nao , na ambao daima halina jibu tayari lililofungwa na kuwapatia.. Kanisa lisilosikiliza linaonyesha kuwa limefungwa kwa mapya, limefungwa kwa mshangao wa Mungu, na haliwezi kuaminika, kwa namna ya pekee  kwa vijana, ambao bila kizuizi wanakwenda mbali badala ya kukaribia.

Kuondokana na hukumu na desturi

Hatua ya kwanza katika mwelekeo wa kusikiliza ni kutoa uhuru katika akili na mioyo  "kutokana na kuhukumu  na desturi": "tunapofikiri tunajua tayari ni nani yule  na anataka nini Papa  Fransisko anafafanua -basi ni shida kumsikiliza mwingine kwa dhati. Vijana hujaribiwa kuzingatia watu wazima waliopitwa na wakati ; na watu wazima wanajaribiwa kuona kuwa ni vijana wasio na ujuzi, kujua jinsi wao walivyo na hasa,  jinsi gani wanapaswa kuwa na kuishi. Yote hii inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha mazungumzo na kukutana kati ya vizazi.

Wazee ni mapigo ya ustaarabu

Watu wazima - anaelezea papa - "wanapaswa kushinda vishawishi vya  kudharau uwezo wa vijana na kuwahukumu vibaya". Vijana, kwa upande wao mwingine, wanapaswa kuondokana na vishawishi  vya kutosikiliza watu wazima na kuwafikiria  wazee  watu wa mambo ya kale, ya zamani na kukera". Wazee, "licha ya udhaifu wao wa kimwili, daima hubaki kumbukumbu ya ubinadamu wetu, mizizi ya jamii yetu, pigo la ustaarabu wetu".Kuwadharau, kuwafungia kwao, kuwafunga katika hifadhi ya upekee au kuwafuta ni dalili ya kuanguka kwa mawazo ya ulimwengu ambayo yanararua nyumba zetu kwa ndani. Kupuuza hazina ya uzoefu ambayo kila kizazi hurithi na kuieneza kwa mwingine ni tendo la kuharibu.

Janga la ukikuhani

Papa anatoa ushauri "kushinda kwa uamzui juu ya  janga la ukikuhani".Kwa dhati  anasema, kusikiliza na kuondokana na desturi pia ni dawa kali dhidi ya  hatari ya ukikuhani, ambayo mkutano kama huu haiwezekani kukosekana. : Ukikuhani ni upotoshaji na ni mzizi wa maovu mengi katika Kanisa kwa maana hiyo anasema Papa, tunapaswa kuomba msamaha kwa unyenyekevu na zaidi  kuunda masharti na ili  kutokurudiwa tena.

Kuchanua matumaini

Sinodi itawafufua mioyo yetu!" Francesco anatualika "tusijiruhusu tujaribiwe na unabii wa bahati mbaya," kukaza "macho juu ya mema ambayo mara nyingi hayafanyi kelele, sio kichwa cha blogu au hufika kwenye kurasa za mbele". Hatimaye, Papa anatuhimiza "tujaribu kuhudhuria siku zijazo, na kutoka nje ya Sinodi si hati tu, ambayo mara nyingi huwa inasomwa na wachache na kuhukumiwa na wengi ", bali inabidi hasa kutoka nje ya sinodi  na mapendekezo halisi ya kichungaji kiasi cha kuweza "kutekeleza kazi ya Sinodi yenyewe" yaani: kuchipusha ndoto, kuamsha unabii na maono, kustawisha matumaini na uaminifu, kuboresha mahusiano, kujifunza kutoka kwa wengine, na kuweka mtazamo chanya unaoangaza akili, unaowasha mioyo, unaoipa nguvu mikono na kuwavuta vijana wote bila kumwacha hata mmoja kuwa na maono yajayo yaliyojaa furaha ya Injili.

04 October 2018, 10:14