Tafuta

Vatican News
Baraza la Maaskofu India wameandaa mkutano wa kwanza wa vijana Katoliki huko News Delhi Baraza la Maaskofu India wameandaa mkutano wa kwanza wa vijana Katoliki huko News Delhi 

Papa kwa vijana wa India:kuweni jasiri na matumaini endelevu!

“Shukuruni Mungu kwa ajili ya maisha yenu mema na kwa faida ya wengine, msisahau kuwa, ujana ni utajiri unatoa matunda”. Ndiyo ujumbe kwa njia ya video wa Papa kwa washiriki wa Mkutano wa kwanza wa vijana Katoliki nchini India kuanzia tarehe 21-25 Oktoba 2018, unaofanyika mjini New Dalhi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 21 Okotaba 2018, mjini New Delhi India, wameanza Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa vijana katoliki. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video akiwatia moyo wote kutoa matunda ya maisha. Baba Mtakatifu anasema, “Shukuru Mungu kwa maisha yenu mema na kwa ajili ya faida ya wengine. Msisahau kuwa ujana ni utajiri unatoa matunda. Na mnao wakati endelevu uliopo na katika mikono yenu na endeleni mbele bila kukata tamaa”.

Taarifa kutoka shirika la habari za kimisionari Fides, linathibithisha mkutano huo kuanza tarehe 21 Okotaba huko New Delh na walio andaa ni Tume ya vijana wa Baraza la Maaskofu wa India. Hata hivyo tarehe 18 Oktoba, Percival Holt, Rais wa kitaifa wa chama cha vojana katoliki nchini India akiwa mwalilishi katika Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana alimzawadia Papa Francisko, msalaba wa Mchungaji mwema uliotenengezwa kwa mkono kutoka kwenye aina ya mti ulichorwa kandambili na ua moja.

Wakiwa wanakwenda sambamba na mkutano wa Sinodi, zaidi ya wawakilishi 500 kutoka katika majimbo 132 katoliki ya India wanaudhuria maadhimisha yaya ya maana hadi tarehe 25 Okotba 2018. Kuanzia sasa mkutano huo utakuwa unafanyika kila mwaka amesema msemaji Manoj Mathew, kati ya waandaaji wa chama hicho cha vojana katoliki na kwamba wanafikiria kuwa ni muhimu kuweza kuwasaidia vijana kuwa na fursa ya kuudhuria vipindi vya mafunzo ya kitaifa.

23 October 2018, 13:56