Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu alikutana na wawakilishi wa kikundi cha wanaclub ya pikipiki ndogo aina ya Vespa Baba Mtakatifu alikutana na wawakilishi wa kikundi cha wanaclub ya pikipiki ndogo aina ya Vespa   (ANSA)

Wanaclub ya Vespa wamemzawadia Papa pikipiki ndogo!

Pikipiki ndogo aina ya Vespa kutoka kwa wanaclub ya vespa za kizamani, wamemzadia Papa Francisko ambayo baadaye itawekwa katika matendo ya upendo kwa wahitaji

Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana katika uwanja wa Mtakatifu Marta, Baba Mtakatifu amepokea zawadi ya pikipiki ndogo aina ya Vespa kutoka kwa wanaclub ya vespa za kizamani. Pikipiki hiyo itauzwa na baadaye kuwekwa katika matendo ya upendo kwa wahitaji.

“Ni zawadi ambayo tulikuwa tunashauku ya kuitoa kwa papa”. Hayo ni maneno ya Guliano Ianiro Rais wa club ya pikipiki ya kizamani aina ya Vespa, akisisimulia wakati wa mahojiano na Vatican News na kwamba zawadi hiyo wameipeleka nyumba ya Mtakatifu Marta. Pikipiki ndogo ya Vespa 50R, ni ya mwaka 1971 yenye namba: BF362918 ambayo wameiandika mwaka wa kuzaliwa wa Bergoglio – yaani wa Papa Francisko hadi leo hii. Pia zawadi ya Element yake ikiwa na nembo ya Vatican.

 Fedha itakayo patikana kutokana na mauzo ya pikipiki ndogo  itaingia katika mfuko wa sadaka. Aliyesindikiza zawadi hiyo ni Msimamizi wa Mfuko wa Sadaka ya Papa Kardinali Konrad Krajewski  ambaye ameikabidhi lakini  ambayo badaye itaingia katika matendo ya upendo.

Pikipiki ndogo 600 aina ya vespa ziliegeshwa ndani ya Vatican na wawakilishi walikwenda uwanja wa Mtakatifu Petro ili kuudhuria sala ya Malaika wa Bwana ambapo Baba Mtakatifu mara baada ya sala, aliwasalimia na kuwakaribisha.

Walio jiandikisha ni watu 640 kutoka claub 77 duniani kote, ikiwa ni muunganiko kwa mara ya pili wa kimataifa mjini Roma- Caput Vespa na muuunganiko  umemalizika tarehe 2 Septemba huko Semenzaio ya Mtakatifu Sisto katika Uwanja wa Porta Petronia. Kila Club ya Vespa imezawadia mji wa Roma mmea ili uweze kupandwa katika mji huo.

 

03 September 2018, 10:01