Tafuta

Jengeni  hadhi ya binadamu na maendeleo yake endelevu Jengeni hadhi ya binadamu na maendeleo yake endelevu 

Ujumbe wa Papa:Jengeni hadhi ya binadamu kwa maendeleo endelevu!

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake katika Jukwaa la G20 la Mazungumzo ya kidini, ulioanza huko Buonos Aires kuanzia tarehe 26-28 Septemba 2018. Papa anawashauri ya kwamba dini zizungumze kwa namna ya kujenga na kuchangia maendeleo endelevu, ambayo yanasimamia juu ya hadhi ya mtu na siyo faida

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Ujumbe wa Papa Faancisko aliowatumia wajumbe wa Jukwa la Mazungumzo ya kidini uitwa G20 unaofanyika katika mji Mkuu wa Argentina, Amerika ya Kusini, ambao umefunguliwa tarehe 26-28 Septemba 2018. Katika kitovu cha meza ya mduara na kazi za makundi zaidi ya washiriki wa Jukwaa hilo wanaongozwa na mada ya “Ujenzi unaoruhusu maendeleo sawa na endelevu:mchango wa dini kwa wakati endelevu na wenye hadhi”.

Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu anasititiza kuwa dini zinaweza kutoa mtazamo mpya wa nini maana ya kuwa mwanadamu, yaani mtamzamo unaozaliwa na imani ya Mungu. Mtazamao ambao unaweza kuchangia kujenga maendeleo ya dhati na siyo wa  wa kutafuta faida binafsi za kichumi.

Mchango wa dini

Baba Mtakatifu katika tafakari yake ni kuanza kutazama hali halisi ya migogoro ambayo inatishia wakati endelevu wa binadamu na ugumu wake, kama vile ndugu wengi kaka na dada wasio kuwa na makazi au kusahuliwa. Kwa maana hiyo anathibitisha kwamba, katika Jukwaa hilo la kidini linaweza kwa namna ya pekee kujikita katika kutafakari kwa kina mchango maalum ambao dini inaweza kutoa maendeleo katika  kuhakikisha wakati endelevu ya hadhi kwa kila mtu, aliyepo duniani kwa maana idadi idadi kubwa inakubwa na changamoto ngumu.

Mazungumzo yenye  tija na siyo kulazimisha mawazo yawe sawa

Akendelea na ujumbe wake anathibisha kuwa Jukwaa hili linaweza kwa mara nyingine kuonesha na kutoa matunda katika mzungumzo yanayojenga na kutafuta suluhisho bora. Mazungumzo ambayo hayaondoi uzalendo, bali yanatambua kuunda uhusianowa kibinadamu ambao unaheshimu, kwa maana ya kusikiliza yule ambaya ana mawazo tofauti, pia ni fursa na utajiri mkubwa. Ni lazima kujenga undugu na si kujenga ukuta  kwa sababu wakati endelevu unahihitaji kuheshimu namna ya kuishi kwa pamoja, mawazo yasiwe ya kinadharia bali matendo.

Bianadamu ndiye kitovu zaidi ya teknolojia

Hata hivyo Papa anaonesha jinsi gani dunia hii inazidi kujiimarisha na mifumo ya kuteknolojia katika manedeleo, lakini akionesha kuwa kwa dhati ni kutaka kutawala, kuthibiti hali halisi katika kukuza masuala binafsi ya kiuchumu na faida. Kila aina ya jaribu la kuunda maendeleo ya dhati. Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa,  kwa mtazamo wa kiuchumi na hata kijamii au kiteknolojia lazima itambue kwanza hadhi ya kuwa binadamu. Binadamu kwa dhati ndiye mdau, ndiye kitovu na ndiye wa mwisho, wa maisha yote ya kiuchumi na kijamii”.

Hadhi ya binadamu na maendeleo endelevu

Katika mtazamo huo Papa Franciskoanahimiza dini kutoa “njia mpya ya kuangalia ukweli na mwanadamu: si kwa tamaa mbaya na madaraka, lakini kwa heshima ya asili ya mtu mwenyewe na wito katika viumbe vyote. Tunapaswa kutekeleza maendeleo endelevu na kulinda nyumba yetu ya pamoja na kutunza familia nzima ya wanadamu. “Tunaweza kufanya kazi pamoja kama vyombo vya Mungu vya kulinda na kutunza viumbe” na kila mmoja anaweza kutoa mchango wake na utamaduni wake na imani yake” amehitimisha Papa Francisko.

 

27 September 2018, 10:29