Tafuta

Vatican News
Papa Francisko ametuma ujumbe wa matashi mema kwa ajili ya Sikukuu ya Mwaka mpya wa Kiyahudi Papa Francisko ametuma ujumbe wa matashi mema kwa ajili ya Sikukuu ya Mwaka mpya wa Kiyahudi 

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Jumuiya ya Kiyahudi Roma!

Papa Francisko amemtumia ujumbe Mkuu wa Jumuiya ya Kiyahudi Roma, Rav Riccardo Di Segni na Jumuiya ya kiyahudi katika fursa ya kuadhimisha sikukukuu ya Rosh Ha Shana, yaani sikukuu ya Mwaka mpya wa Kiyahudi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Bwana atubariki kwa zawadi ya amani na kutuongezea nguvu kwa wingi katika juhudi ya kuihamasisha bila kuchoka. Ndiyo ujumbe wa Papa Francisko aliomtumia Mkuu wa Jumuiya ya Kiyahudi Roma, Rav Riccardo Di Segni na Jumuiya ya kiyahudi katika fursa ya kuadhimisha sikukukuu ya Rosh Ha Shana, yaani sikukuu ya Mwaka mpya wa Kiyahudi ; Yom Kippur na Sukkot na Sikukuu ya Mavuno.

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake anasema “ Katika fursa ya Sikukuu ya Rosh Ha- Shanah, Yom Kipuur na Sukkot, ninayo furaha kuwatumia matashi mema ya dhati wewe na jumuiya ya Kiyahudi mjini Roma. Anawatakia sikukuu njema kwa kukumbuka mema mengi waliyoopokea kutoka kwa mwenyezi Mungu na iwe kwa Jumuiya ya wayahudi wa dunia nzima neema ya kina na utulivu kiroho.

Kwa wema wake usio kuwa na kifani, uweze kuwatia nguvu kila mahali palipo na muungano wa urafiki na utashi wa kuhamasisha daima mazungumzo kwa ajili ya wema wa wote. Shalo Alechem” . Amehitimisha!

19 September 2018, 13:42