Tafuta

Vatican News
Papa akiwa na vijana wa Grenoble-Vienne wakati wa mkutano wao mjini Vatican Papa akiwa na vijana wa Grenoble-Vienne wakati wa mkutano wao mjini Vatican  (ANSA)

Papa:Vijana fuata Yesu wakati Kanisa likichanua na katika kipeo!

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na kikundi karibia cha vijana 20, tarehe 17 Septemba 2018 wa jimbo la Grenoble – Vienne. Mkutano wao umetangazwa tarehe 18 Septemba ukiwa na mada mbalimbali hasa zinazohusu juhudi za wakristo katika jamii ,miito, kushuhudia, huduma kwa maskini na mengineyo. Vijana wajifunze kutoa huduma

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mabaya yanayoikumba Kanisa, ukaribu wa maskini, miito, unyanyasaji na juhudi ya wakristo katika Jamii ndiyo mada zilizoguswa tarehe 17 Septemba 2018, katika mkutano wa faragha wa Baba Mtakatifu Francisko na vijana wa Jimbo la Grenobal – Vienne, ambapo habari hiyo ikatolewa rasmi na vyombo vya habari tarehe 18 Septemba 2018 . Katika maongezi yao, wanasema yamejikita katika nafasi kubwa ya mazungumzo ya wazi, lakini zaidi ya ubaba na bila kuwa na wasiwasi, Baba Mtakatifu ameweza kujibu maswali ya vijana kuanzia umri wa miaka 14 na  kuendelea mbele. Baba Mtakatifu amethibiisha kuwa wao ni wakweli na hivyo kwa huruma na mifano ya dhati amewajibu kwa dhati maswali yao mengi.

Kushuhudia kabla ya kunena

Baba Mtakatifu kwa vijana hao ameomba wasikose kuzungumza, lakini wawe na utayari wa kusikiliza na kuwa tayari kutembea katika njia ya ukaribu. Hiyo ndiyo kanuni ya kwanza kwa mujibu wa Papa FRancisko kama siri ya kuonesha ujumbe wa kikristo, hata kwa wale ambao wanapenda kushutumu Kanisa au kuinyoshea kidole dhidi yake katika suala la sasa la unyanyasaji kingono na kijinsia. Kwa maana hiyo amesema kuwa, kushuhudia kabla ya kunena ndiyo picha ya ujumbe wa Kikristo kwa wote . Kusikiliza, kutenda ndiyo hapo unaweza kusema. Pamoja na hayo ujumbe wa kikristo hauwezi kutangazwa ukiwa umekaa katika sofa, kwa maana daima ni katika mwendo. Huko kuna maana ya kuiga Yesu ambaye kwa miaka mitatu alitembea tu, unaweza kufikiria kuwa maisha yake yote yalikuwa ni barabarani, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Kuinama kwa maskini.

Akiendelea kujibu maswali ya vijana hawa, Baba Mtakatifu pia ameweza kuwashauri juu mzizi wa Injili ya kwamba, huo unajikita katika moyo wa maskini na ndiyo picha ya Kristo. Kuhudumia maskini siyo uharibifu, lakini ni Injili. Kwa maana hiyo vijana lazima wajifunze kuwa mstari wa mbele katikati ya huduma bila kutazama juu kuelekea chini, badala yake ni kupiga magoti ili kuweza kugusa magonjwa ya maskini, kugusa madonda ya Kristo na kuweza kuishi upendo wa dhati. Na anaongeza: anaposema maskini, maana yake ni hata wa afya, wagonjwa; maskini wa ukosefu wa fedha; maskini wa utamaduni; maskini ambao wameangukia katika raha, hata madawa ya kulevya. Ni vijana wenzao wangapi ambao wameangukia katika janga la madawa ya kulevya, hao kwa mfano ni masikini na  masikini wa Injili.

Wajibu wa Kikristo:  Baadaye Baba Mtakatifu Francisko ameelezea juu ya masuala ya uwajibu wa kikristo katika jamii: kwa maana hiyo amewambia wajifunza kuwa walinzi wa ndugu zao, ili  wasiishi na upweke , badala yake watengeneze jumuiya, wawe mwili ambao unasaida katika safari na kuwa tayari kuchafua mikono yao. Amekumbusha hata historia ya Biblia kuhusu Caino kwa maana hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa ajili ya wengine, familia, nchi ya na dunia kwa ujumla.  Na daima wafanye hivyo lakini wakiwa kinyume na matendo ya Caino. Baba Mtakatifu anathibitisha Caino alinawa mikono, Pilato alinawa mikono na Mkristo anachafua mikono ili kufanya mema kwa wengine, Baba Mtakatifu amesisitiza.

Kadhalika ametoa onyo kwa mambo mawili ambayo amekiri ni adui mbaya wa juhudi ya Mkristo: mambo hayo ni ubinafsi hasa ule wa kujitazama  mwenyewe binafsi, kama vile ufisadi, na pia adui mwingine ni  kuwa na mali  kwa maana ya yule anayeshikilia mambo ya fedha, ambayo inayochoma na kukatiza moyo wa mawazo ya wote, hadi kifikia mipka ya moyo na katika mifuko.

Kuwasindikiza mapadre na watawa

Kuhusiana na swali la miito, Baba Mtakatifu amesisitiza juu ya ulazima wa kusindikiza vijana wanao chagua njia ya kuweka wakfu: mapadre, watawa na waseminari… kwa maana wito ni zawadi kutoka kwa Mungu, hivyo kuna haja ya kuhifadhi kwa njia zozote amesisitiza na kusema, jambo msingi ni kuwalelimisha juu ya ubaba, umama katika jumuiya ya kindugu. Kuwasaidia wakue na kuwasindikiza!

 

 

19 September 2018, 13:22