Tafuta

Vatican News
Mkutano wa wajumbe kimataifa  wa wajane walio wekwa wakfu Mkutano wa wajumbe kimataifa wa wajane walio wekwa wakfu  (Vatican Media)

Papa:Ujane ni uzoefu kwa namna ya pekee mgumu!

Baba Mtakatifu Francisko,tarehe 6 Septemba 2018, amekutana na vikundi viwili vya wajane ambao wamejisadaka maisha yao kwa Bwana, wakiwa katika hija yao ya kiroho mjini Roma kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Wajane waliofunga nadhiri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Marafiki wapendwa, kwa furaha kubwa ninawakaribisheni katika fursa yenu ya hija ya Roma. Ninawashukuru kwa hotuba yenu na ninatoa salam kwa wanajumuiya ya Ndugu wa Mama wa Yesu wa ufufuko na Jumuia ya Nabii Anna ambao mmetawanyika katika nchi nyingi za dunia , kama vile hata mapadre ambao wamewasindikiza na kwa njia yetu, hata watu wote ambao wamepata majaribu kutokana na vifo vya wenza wao”.

Hayo ni maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 6 Septemba 2018, alipokutana na vikundi viwili  vya wanawake wajane  ambao wamejisadaka maisha yao kwa Bwana,  na kufunga nathiri wakiwa katika hija yao  ya kiroho mjini Roma kwenye Mkutano wa Kimatafa wa Wajane wenye nadhiri. Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake anasema, “ujane ni uzoefu kwa namna ya pekee mgumu…. Kwa wengine unajieleza kwa namna kutambua kuonesha nguvu yao zaidi katika kutunza watoto na wajukuu na kupata kielelezo hiki cha upendo wa utume mpya wa elimu” ( Wosia wa kitume Amoris laetitia 254)

Wameitwa kuishi ushauri wa kiinjili

Kama hiyo ni kweli, sehemu kubwa, vifo vya waume zao, vimewapelekea hata kujua wito mwingine kwa namna ya pekee ule wa Bwana na kujibu kwa kufunga nadhiri kwake kwa ajili ya upendo na kwa upendo. Pamoja na wao, Baba Mtakatifu anashukuru Mungu kwa ajili ya uaminifu wa upendo ambao unawunganisha kila mmoja wao, licha ya kifo na mchumba wao ambaye amewachagua kwa kufunga nadhiri kwa ajili ya kuishi leo hii, kumfuasa Kristo kwa njia ya usafi, utii na ufukara. Hata hivyo anaongeza kusema, wakati mwingine maisha  hayo yanawakilisha changamoto kubwa na kwa njia ya hizo, Bwana anawaalika katika uongofu mpya ambao unawawezesha kwa neema na kujionesha vema katika kuishi, kwa lengo la kufikia na kushiriki utakatifu wake ( Eb 12,10), Wosia. Gaudete et Exsultate – furahini na kushangilia, 17).

Kuitwa kwao ni neema

Kwa namna hiyo kuitwa kwao, wao wanathibitisha kuwa inawezakana kwa neema ya Mungu na msaada katika kusindikizwa na wachungaji  na watu wengine wa Kanisa kuishi, ushauri wa Kiinjili na kujikita katika uwajibikaji binafsi wa familia, taaluma na kijamii. Kujisadaka kwao katika ujane ni zawadi ambayo Bwana anafanya kwa Kanisa kwa kuwaalika wote wabatizwa kwamba, nguvu ya upendo wa huruma yake ndiyo njia ya maisha na utakatifu ambayo inatuwezesha kushinda majaribu na kuzaliwa kwa matumaini na furaha ya Injili. Baba Mtakatifu anawaalika zaidi kuendelea kuwa na mtazamo usio na kikomo kwa Yesu Kristo na kukuza mahusiano kwa namna ya pekee yanayo waunganisha na Yeye. Kwa maana anasema,  yeye yuko pale katika moyo na Moyo wa Bwana, kwa usikivu wa Neno lake, ambalo tunachota ujasiri na kuvumilia akitupatia mwili na roho ili kujimwilisha vema kwa njia ya kujiweka wakfu na katika shughuli zetu

Wawe taa kwa wanaotembea katika giza na kivuli cha mauti

Kwa kujitoa wakfu Baba Mtakatifu anasema wanaweza kupeleka ushuhuda wa upendo wa Mungu ambaye kwa kila mtu anaitwa kujua uzuri na furaha ya kuitwa na Yeye. Waungane na Yesu Kristo na kuwa chachu katikakati ya dunia hii, wawe mwanga kwa wale wanaotembea katika giza na kivuli cha mauti. Katika ubora wa maisha yao kindugu, katika umbu la jumuiya zao, wajitunze kwa njia ya uzoefu wao wa binafsi wa na udhaifu,  kuwa karibu na wadogo na maskini, kwa kuwaonjesha huruma ya Mungu na ukaribu wake wa upendo. Kwa mantiki hiyo, Baba Mtakatifu amewatia moyo ili waishi nadhiri zao kila siki kwa urahisi na unyenyekevu, wakiomba Roho Mtakatifu ili anawasaidie kushuhudia, kwa dhana ya kanisa na duniani ambayo Mungu naweza kutenda wakati wowota , hata katikati ya kushindwa na ambaye anajitoa kwa Mungu kwa ajili ya upendo, kwa hakika atazaa matunda” (Wosia Evangelii gaudium 279).

Amehitimisha hotuba yake na kusema: “ kwa matumaini hayo, ninawakabidhi kwa Bwana na kwa maombezi ya Bikira Maria na kuwabariki kwa baraka ya kutume , kwa wote, familia ya jumuiya hizi mbili ya ndugu wa Mama Yetu wa Ufufuko (Fraternité Notre Dame de la Résurrection) na Jumuiya ya Nabii Anna” (Communauté Anne la Prophetesse).

06 September 2018, 15:26