Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu anawaombea waathirika wa ajili ya ajali ya meli katika Ziwa la Victoria nchini Tanzania Baba Mtakatifu anawaombea waathirika wa ajili ya ajali ya meli katika Ziwa la Victoria nchini Tanzania 

Papa:Salam za pole kufuatia ajali ya Meli nchini Tanzania

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa raia, viongozi wa Kanisa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia na ajali ya meli iliyotokea Alhamis 20 Septemba 2018 katika ufukwe wa Kisiwa cha Ikara. Shughuli za uokaji bado zinaendelea

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake, uliotia saini na Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican tarehe 21 Septemba 2018 kwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania Askofu Marek Solczynsk, kufuatia na Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa raia, viongozi wa Kanisa, na na  Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kufuatia na ajali ya meli iliyotokea, Alhamis 20 Septemba Tanzania.

Baba Mtakatifu Francisko anaelezea masikitiko yake mara baada ya kupata habari ya ajali ya feri ya MV Nyerere ambayo ilipinduka katika Ziwa Victoria, ufukweni mwa Kisiwa cha Ikara tarehe 20 Septemba 2018. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anaonesha kwa masikito moyoni na  mshikamano kwa wale wote wanaoomboleza kwa ajili ya kupoteza wapendwa wao na kwa wale ambao bado wanahofia kuwakuta bado hai wale ambao hawajapatikana. Kwa wote anaomba baraka ya Mungu iwashukie na kuwakumbatia kwa nguvu na faraja kwa wale waliopatwa na mkasa huo. Kadhalika anawatia moyo viongozi wa raia na vikosi vya ukoaji wanaoendelea katika juhudi hiyo ya uokoaji.

Kuhusiana na ajali ya Meli ufukweni Kisiwani  cha Wilya ya Ukerewe Tazania

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bwana Issack Kamwelwe amesema kuwa, zoezi la uokoaji wa miili ya waliofariki linatarajiwa kukamilika jioni ya tarehe 21 Septemba 2018, na tayari maandalzi ya maziko yanaendelea kufanyika ikiwemo kuandaa majeneza. Waziri Kamwelwe ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC), akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara Wilaya ya Ukerewe mkoani Mmwanza, na kuongeza kuwa Shughuli za mazishi zitafanywa kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kuzingatia mila na desturi na kwa kuzingatia taratibu za kidini kwa vile viongozi wote wa dini wapo.

Kufuatia ajali hiyo mbaya na yakusikitisha Rais atuma salam za rambi rambi

Naye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana John Pmombe Magufuli, ametuma salamu za rambirambi na pole kwa familia, ndugu na jamaa kutokana na ajali ya kivuko hicho cha MV Nyerer, na amewaomba Watanzania kuwa watulivu wakati huu ambapo Taifa limepata msiba mkubwa.

Mbali na Rais Magufuli hata viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nao wanaendelea kutoa salamu za pole.Wakati huo huo taarifa zinasema kuwa naye Waziri  Mkuu Kassimu Majaliwa amekatisha ziara yake mkoani  Dodoma na kuelekea Ukerewe Mwanza kuwafariji wananchi waliopatwa na maafa kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere. Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma, ametangaza uamuzi huomchana wa Ijumaa,tarehe 21 Septemba, 2018 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chandama, wilayani Chemba ambao walisimamisha msafara wake ili wamweleze kero kubwa ya maji inayowakabili.

 

21 September 2018, 15:19