Tafuta

Vatican News
utano wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Wakristo Mkutano wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Wakristo  (Vatican Media)

Papa:kujenga mahusiano ya dhati ya kindugu na wapentekoste!

Papa Francisko, amekutana na washiriki karibia 60 ya Mkutano wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa umoja wa Wakristo. Mada ya mkutano huo ilikuwa juu ya “Makanisa ya Kipentekoste, Karismatiki na Kiinjili: dhana ya umoja”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican News

Kujenga mahusiano ya dhati kindugu na jumuiya za kipentekoste,karismatiki na wainjili ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko alio utoa  kwa washiriki karibia 60 wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha umoja wa wakristo, aliokutana nao m jini Vatican Ijumaa 28 Septemba 2018. Papa Francisko anasema juitihada katika kumasisha umoja wa Wakrito ni muhimu hasa kwa mtazamao wa matukio ya kuongeza kwa makundi ya kipentekeoste , na wakarismatiki, na hivyo ametoa wito wa kujenga mahusiano ya dhati.

Ulazima wa mang'amuzi ya Roho Mtakatifu

Akiendelea na hotuba yake, amesema hawali ya yote  kuna ulazima wa kufanya mang’amuzi na kutambua uwepo wa Roho Mtakatifu katika jumuiya hizo na kutafuta kila njia ya kujenga mahusiano ya dhati kindugu. Na hiyo itawezekana tu iwapo kutakuwapo fursa za kukutana nao  na kushinda ile hali ya kutoaminiana, inayozidishwa na ujinga au ukosefu wa uwelewa wa pamoja kwa sehemu zote mbili.

Ni lazima kufanya mchakato ili kuweza kufikia,kwa maana hiyo Papa Francisko anatoa uzoefu wake binafsi ambao anajihukumu. Kwani amesema akiwa kama mkuu wa Shirika la Wajesuit, alikuwa amewakataza wanashirika wake wasiwe na mahusiano na Chama cha Huuisho Roho katoliki wa Roho, kwa sababu katika muungano wao sala, ulifanana kama vile shule ya samba yaani muziki wa samba.  Lakini baadaye amesema kuwa, aliwaomba samahani na kama askofu amekiri kwamba alikuwa na mahusiano mema  katika Misa kwenye Kanisa Kuu.

Kutembeleana

Baba Mtakatifu akiendela amesema inahitaji undugu wa kutembeleana ambao ni kwa njia ya sala, kutangaza Injili na huduma kwa wenye shida. Kwa namna hiyo wakatoliki wanaweza kutoa sifa kwa uzoefu wa jumuiya nyingi zinazoishi imani ambayo kwa namna nyingine ni tofauti na ile ambayo wamezoe. Kwa upande mwingine wao wanaweza hata kusaidiwa ili kushinda hukumu juu ya Kanisa Katoliki na kutambua kuwa katika tunu msingi ya utamaduni , ambayo waliipokea Mitume, ni Roho Mtakatifu ambaye anaendelea kufanya kazi kwa uthabiti.

Hata hivyo ameelezea juu vikwazo ambavyo vinasababisha  wakati mwingine mahusiano yasiwe  rahisi  kati ya wakatoliki, wapentekoste, wakarismatiki na wainjili, kwamba ni pamoja sababu za kihisia, katik auzoefu huu wa kidini. Vikwazo hivyo anavitaja kuwa ni mwonekano wa ghafla wa jumuiya mpya, ambayo inajihusisha mtu au kwa baadhi ya wahubiri wengine, kutofautiana  na misingi ya kanuni za kidini  na uzoefu wa Makanisa ya kihistoria, kwa maana hiyo ,Papa amesisitiza, hali hiyo inaweza kujificha hatari ya kuchukuliwa na mawimbi ya kihisia ya wakati huo. Kutokana na ukweli kwamba si waamini wachache wakatoliki   wanavutiwa na jumuiya  hizo  na hivyo basi, “ni sababu ya malumbani lakini,hata hivyo Papa anaongeza kusema, kwa upande wetu, inaweza kuwa suala la uchunguzi binafsi na upyaisho wa shughuli za kichungaji”.

Hakuna nafasi isiyobadilika. Roho hujenga habari mpya

Kwa hakika, kuna jumuiya nyingi ambazo zimeongozwa na harakati hizi, zinaishi kwa dhati uzoefu wa Kikristo na Wakatoliki wanaweza kukubali utajiri huo: Kanisa linakua kwa uaminifu kwa njia ya Roho Mtakatifu hasa zaidi linapojifunza kujifungia kwa ndani, lakini kukubali bila hofu na wakati huo huo, kuwa na ufahamu mkubwa habari zake mpya. Roho Mtakatifu daima ni mpya. Kila wakati. Na tunapaswa kuzoea. Ni habari mpya ambayo inatufanya sisi kuelewa mambo,  kwa undani zaidi, kwa mwanga zaidi na kubadili tabia nyingi pia! Au hapana? pia tabia za nidhamu. Lakini Yeye ndiye Bwana wa habari. Amethibitisha Baba Mtakatifu!

Kwa hiyo, hatupaswi kupumzika juu ya “nafasi za kimya na zisizowezekana” lakini “kukubali hatari ya kujikita katika kuendeleza umoja: pamoja na utii wa mwaminifu wa Kanisa na bila kuzima Roho”. Kwa dhati, Roho hujenga mapya na huongoza kila kitu katika umoja wa kweli, ambao sio sawa. Ufunguzi wa moyo, hutafutaji wa  muungano  na mang’amuzi, ni mitazamo ambayo lazima iwe ndiyo tabia ya “mahusiano yetu”, amehitimisha Papa.

 

 

 

28 September 2018, 14:37