Cerca

Vatican News
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana  (ANSA)

Papa: Kuamini ni kuweka kitovu cha upendo wa kweli katika maisha

Katika kukiri imani katika Yesu Kristo auwezi kuishia katika maneno tu. Papa katika tafakari yake wakati wa sala ya Malaika wa Bwana amethibitisha hayo juu ya kumfuasa Yesu maana yake ni kama kuweka mhuri wa maisha binafsi katika upendo wa Mungu na jirani. Amekumbuka ziara ya Palermo na kutangaza zawadi ya msalaba mdogo kwa waliokuwa uwanjani.

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

“Yesu ni nani? Hilo ndilo swali linalojikita ndani ya Injili nzima ya Marko na leo katika Liturujia inapendekezwa kwenye Somo ambalo Yesu mwenyewe anawauliza juu ya utambulisho wake kwa mitume wake”. Ni mwanzo wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotoa tarehe 16 Septemba 2018, kwa waamini na mahujaji waliofika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro kusali naye sala ya Malaika wa Bwana. Akiendelea na tafakari hiyo anasema, “Yesu anataka kujua ni kitu gani watu wanamfikiri! Lakini kabla ya Yesu kutaka kujua wanafikiria nini juu yake, Yeye tayari alikuwa anatambua kuwa wafuasi wake wanao uelewa makini kuwa watu  wanamamjua Mwalimu!”, Francisko amethibitisha.

“Inajulikana kuwa, Yesu anafikiriwa na watu kuwa yeye ni nabii mkubwa. Lakini kwa uhakika yeye hana wasiwasi juu ya hilo kwa kutaka kujua kiasi gani wanamfahamu na hata mazungumzo ya watu wanayosema juu yake. Na wala Yeye hakubali hata mitume wake wajibu maswali yake kwa mantiki ya mtindo wa wakati ule, au kwa kutaja watu maarufu wa Biblia Takatifu, kwa maana imani thabiti ikiinamia katika mantiki ya ukawaida, hiyo ni imani kipofu”, anathibitisha Papa.

Yesu ni kitovu cha maisha ya anayesadiki

Baba Mtakatifu akifafanua zaidi anasema: “Hiyo haitoshi kwa Yesu kwa maana anataka jambo jingine; anatamani kwamba, kati yake na mitume wake wajenge ule uhusiano binafsi. Na ndiyo maana anauliza: “ Je ninyi mnasema mimi ni nani? Na hilo Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa: hilo  ni swali analouliza kila mmoja wetu, na “labda,“inawezakana nasi tunathibitisha kwa shauku kuwa,“Wewe ni Kristo”. Francisko amethibitisha: “Lakini Yesu anapotwambia kwa uwazi, kile ambacho aliwaeleza mitume wake yaani kwamba, utume wake unatimizwa, si katika njia pana ya mafanikio, bali ni katika njia nyembamba ya kuwa  mtumishi mteswa, mtiifu, aliyekataliwa na kusulibiwa, hapo ndipo inawezekana tukawa kama  Petro na kupinga jambo hilo kwa maana linakwenda kinyume na matarajio yetu ambayo ni ya kiulimwengu”, Baba Mtakatifu amekazia!

Kukukiri imani na maisha ya dhati

Kutokana na hiyo katika kuamini Yesu haiwezekani kamwe  kuwa suala la maneno tu, kwa maana  inahitaji“ kuchagua na kwa matendo ya dhati”, yaliyotiwa mhuri wa upendo wa Mungu na jirani. Ili kumfuasa Kristo inahitaji kujikana binafsi na kuchukua msalaba. Anayetaka kujiokoa maisha yake binafsi atayapoteza”, kama isomekavyo katika Injili. “Mara nyingi katika maisha na kwa sababu nyingi, tunakosea njia ,kwa kutafuta furaha katika mambo au kwa watu ambao tunawageuza kama vitu. Lakini furaha ya kweli tunaipata tu, iwapo upendo wa kweli tuna kutana nao, unatia mshangao na unatubadili. Upendo unabadili kila kitu. Upendo ndiyo kila kitu na upendo unaweza kubadili hata sisi ! na kila mmoja wetu”, Papa Mesisitiza.

 

17 September 2018, 10:53