Cerca

Vatican News
Misa ya Papa Francisko kwa waamini wa huko Palermo, Sicilia Misa ya Papa Francisko kwa waamini wa huko Palermo, Sicilia   (ANSA)

Misa ya Papa Palermo:Enyi Mafia,ongokeni kwa Mungu wa kweli na wa Yesu Kristo!

Katika siku ya ziara yake huko Sicilia katika fursa ya miaka 25 tangu kuwawa kwa Mwenyeheri Padre Pino Puglisi katika mikono ya uhalifu wa kupangwa uitwao Mafia, Baba Mtakatifu ametoa wito kwa watu hao waache tabia ya kuogopesha watu: “Hacheni kufijifikiria ninyi wenyewe binafsi na fedha zenu, ongokeni kwa Mungu wa kweli na wa Yesu Kristo”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Anayemchukia ndugu yake na kusema anampenda Mungu, ni muongo “kwa sababu ya uongo wa imani anayokiri kuwa nayo kwa Mungu wa upendo”. Baba Mtakatifu ameanza mahubiri yake na maneno hayo wakati wa kuadhimisha Misa Takatifu huko Foro Italia, katika liturujia kumbukumbu ya Mwenyeheri Padre Pino Puglisi, ambapo Papa amelaani vikali juu ya uhalifu wa kupangwa uitwa Mafia. “Neno chuki linapaswa kufutwa katika maisha ya wakristo. Haiwezekani kuamini Mungu wakati unachukia ndugu”.

“Huwezi kuamini Mungu wakati wewe ni mafia. Anayeishi maisha ya umafya haishi ukristo kwani anakufuru maisha katika jina la Mungu upendo. Leo hii tunahitaji wanaume na wanawake wa upendo na siyo wanaume na wanawake wenye kutaka heshima; wenye kuhudumu na siyo wenye kujiingiza katika shughuli zisizo stahili,  wanaotembea pamoja na siyo wanaokimbilia kwenye uwezo. Na safari hiyo inahitaji uongofu wa kweli ambao unazuiwa na hatari ya wamafya wa kweli na mabao kweli inabidi kuwakabidhi kwa Bwana.

Baba Mtakatifu anasema: Iwapo misemo ya wamafya ni :“ wewe hujuhi mimi ni nani,” na msemo wa wakristo ni ule usemao “ mimi ninahitaji wewe. Iwapo hatari ya wamafya ni: wewe utakipata”,  na maombi ya kikrito ni: Bwana nisaidie niweze kupenda”. Kwa maana hiyo  Baba Mtakatifu ameongeza kwa wanamafya “ninawambia: badilika ndugu kaka na dada! Hacheni kujifikiria ninyi binafsi na fedha zenu. Ninyi mnajua kuwa kinachotoka jasho hakitoki mfukoni.  Ninyi hamwezi kupeleke lolote. Ongokeni kwa Mungu wa kweli wa Yesu Kristo, kaka na dada, na iwapo hamfanyi hivyo, maisha yenu wenyewe yatapotea na kushindwa vibaya sana”. Baba Mtakatifu amethibitisha.

Ushuhuda wa Padre Pino Puglisi: Aliyeish maisha yake ya dhati  kati ya maskini wa ardhi yake na kwa muda mrefu katika zawadi na huduma alikuwa na padre Pino: Yeye hakuishi ili aweze kuonekana, bali aliishi Akitoa wito na kupinga umafya na hata hakutosheka zaidi ya kusikia kuwa hawanyi lolote baya, bali alikuwa akipanda wema. Katika dhana ya kupotelea katika miungu fedha, Papa Francisko anasisitiza kuwa, Padre Pino alikuwa kinyume na hilo kwa kuzidi kupendekeza uzuri wa Mungu –upendo.

Kwa maana hiyo upendo wa Padre Pino ulikuwa wa maisha ya ushindi kwa tabasabu, hata wakati wa kifo chake: “Miaka 25 iliyopita kama siku hii, alipofariki wakati wa siku ya kuzaliwa kwake, aliweka taji la ushindi wake na tabasamu. Kwa  tabasamu lile haliishi na halikumfanya hata halale usingizi  usiku  yule aliye muua padre huyo, kwa maana yeye alisema; “kuna aina ya mwanga wa tabasamu”. Padre Pino hakuwa na silaha ya kujilinda, lakini tabasamu lake lilikuwa likionesha nguvu ya Mungu. Halikuwa linapumbaza, lakini likiangaza kwa ukarimu, ambao ulikuwa ukichimba kwa kina  na kuangazia moyo.

Mapadre wa tabasamu: Baba Mtakatifu akikumbuka mfano wa Padre Pino, ameelekeza hata dharura maalum iliyopo kwa sasa  kwamba: “ Tunayo haja ya kuwa na mapadre wenye tabasamu, wakristo wa tabasamu ambao hawachukulii mambo kwa urahisi, badala yake  ni matajiri pekee  ya furaha ya Mungu, kwa maana  ya kuwa na wanaamini katika upendo na kuishi kwa kuhudumia. Padre Pino alitambua jinsi gani alikuwa hatarini, lakini zaidi alitambua kwamba  hatari ya kweli ya maisha ilikuwa ni ile ya kuogopa kutojihatarisha; ni ile ya kuzeekea mahali pazuri, katikati na kwa kutafuta njia fupi.

Sala ya Baba Mtakatifu: Bwana aweze kutuokoa dhidi ya  kuishi namna hiyo , katika kufurahia nusu ukweli. Mungu atuokoe na maisha madogo ambayo yanazungukia vitu vidogo vidogo. Atuokoe kufikiria kuwa kila kitu kinakwenda vizuri, iwapo mimi mambo yangu ni vizuri.  Atuokoe dhidi ya kujiamini wenye kuwa na haki wakati hatujihusishi na  kupinga ukosefu wa usawa. Atuokoe na kujiamini kwamba ni wema  kwakuwa eti hatufanyi lolote lililo baya. Bwana tupatie shauku ya kufanya mema: kutafuta ukweli na kupinga uongo: wa kuchagua sadaka, badala ya uvivu; wa upendo badala ya chuki; wa msamaha badala ya kulipiza visasi.

Kupoteza maisha: Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza  hata kama tumealikwa kuchagua: kuishi binafsi au kutoa maisha, upendo au ubinafsi. Maisha yenye ushindi si yale ambaye anaishi kibinafsi. Si yule anayejitosheleza mahitaji yake binafsi, hata kama anaonekana kijuu juu kushinda mbele ya macho ya dunia”. Unapoishi mtindo wa kibinafsi ambao unashikilia  mambo, katika fedha, madaraka na raha, hayo yote yataishia  kwa namna moja kushindwa: shetani ana milango iliyo wazi na moyo unabobea ndani ya ubinafsi mwisho wake ni kubaki na upweke na utupu ndani mwako. Ili kuweza kutoa suluhisho la mabaya ya ulimwengu, ahitajiki fedha na madaraka, kwani Baba Mtakatifu anathibitisha, “ fedha na madaraka havitoi uhuru wa mwanadamu, badala yake vinamfanya kuwa mtumwa.

Maisha yenye ushindi: Maisha yenye ushindi, ni yale ambayo yameelekezwa na Yesu,kwa maana ya yule  ambaye anabadili mantiki yenye makosa na mitindo inayopendekezwa hata na matangazo ya kibiashara. Kwa maana hiyo maisha ya ushindi siyo yale yeye mafanikio, kwa yule anayepata faidha zake na hundi zake.  Njia aliyo ionesha Yesu ni ile ya upendo mnyenyekevu , kwa maana “ ni pendo tu unaokoa ndani moyo na yenye kuleta amani na furaha” anathibitisha Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza: Madaraka ya kweli ni huduma. Na sauti yenye nguvu zaidi si ya yule anayepiga kelele zaidi, bali sala. Na mafanikio makubwa si yale ya kujulikana zaidi, bali ni ushuhuda wa dhati”. Moja ya njia ya  kujulikana  haraka iwezekanavyo kikristo, Papa Francisko anasisitizza ni kuhisi na kuhudumia watu bila kupiga kelele, bila kushutumu na kusababisa ugomvi.

Kutoa maisha: “Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” Yh 15, 13). Maneno hayo ya Yesu yameandikwa katika Kaburi la Padre Puglisi. Baba Mtakatifu akimalizia amekumba maneno hayo “ yanakumbusha wote ya kuwa, kutoa maisha ndiyo siri ya ushindi wake, siri ya maisha mazuri. Kwa maana hiyo leo hii tuchague hata sisi maisha mazuri!

15 September 2018, 14:00