Tafuta

Vatican News
Tarehe 3 Septemba Papa amekutana mjini Vatican na maaskofu waliomaliza mafungo ya kiroho Tarehe 3 Septemba Papa amekutana mjini Vatican na maaskofu waliomaliza mafungo ya kiroho 

Papa Francisko amekutana na maaskofu waliomaliza mafungo kiroho!

Papa Francisko amekutana na Maaskofu karibia 40 katika nyumba ya Mtakatifu Marta ambao kwa siku hizi wameshiriki Mafungo ya kiroho, yaliyoandaliwa na Baraza la Kipapa la Maaskofu. Mafungo haya ya kiroho yanazingatia utashi wa Baba Mtakatifu Francisko, kwa maaskofu wanao adhimisha miaka mitano na sita tangu kuwekwa wakfu kama maaskofu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 3 Septemba 2018, Papa Francisko amekutana na maaskofu ambao wamefanya Mafungo ya kiroho tangu tarehe 20 Agosti hadi 3 Septemba 2018.  Amekutana nao katika katika nyumba ya Mtakatifu Marta karibia maaskofu 40 ambao kwa siku hizi wameshiriki Mafungo ya kiroho, ambayo yameandaliwa Baraza la Kipapa la Maaskofu.

 Mafungo haya ya kiroho yanazingatia utashi wa Baba Mtakatifu Francisko ambaye alitaka kwamba kila mwaka itolewe fursa ya kukutana na kufanya mafungo ya kiroho ya pamoja kwa ajili ya maaskofu ambao wanaadhimisha miaka mitano na 6 tangu kuwekwa kwakfu kama maaskofu.  Kutokana na suala hilo, tangu tarehe 20 Agosti hadi 3 Septemba , wameunganika kwa pamoja maaskofu waliowekwa wakfu kati ya mwaka 2011  - 2013. Mafungo ya kiroho yalikuwa yamegawanyika katika sehemu mbili, ya kwanza ilinzia eneo la Mji wa Aricia katika nyumba ya Kiroho ya Divino Maestro Roma.

Maaskofu hawa  waliongozwa katika uzoefu wao kwa mada ya  kushirikishana , uzoefu wao, furaha, matatizo na hata changamoto. Sehemu ya pili ya mafungo ilifanyika huko Camaldoli katika Wilaya ya Arezzo nchini Italia kwenye  Monasteri ya wamonaki, pamoja na kwamba  mafungo ya kiroho yaòiendeshwa kwa tasaufi ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola wakiongozwa na mapadre wa Kijesuit.

04 September 2018, 13:14