Tafuta

Vatican News
Papa Francisko nchini Latvia Papa Francisko nchini Latvia  (ANSA)

Papa:Ninyi ni mizizi ya watu, msipoteze matumaini na upole!

“Mara nyingi wahanga ambao wamejitoa miili yao na roho yao kutetea uhuru wa nchi zo, wametupiliwa mbali katika upweke wao, ukosefu wa rasilimali na kubaguliwa hadi kufikia umaskini wa kukithiri”. Ndiyo tafakari ya Baba Mtakatifu aliyoitoa katika Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Yakobo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kutembelea Kanisa Kuu la Mtakatifu Yakobo, Kanisa lililojengwa Karne ya XIII, na leo hii limejumuishwa katika orodha ya thamani ya Urithi wa Dunia kwenye  Umoja wa Mataifa (Unesco). Baba Mtakatifu amekaribishwa katika lango kuu na Paroko, wakati huo karibu na altare akakaribishwa na wanadoa wawili wazee ambao wamempatia maua,na Papa akayaweka katika picha ya Bikira Maria.

“Mara nyingi wahanga  ambao wamejitoa miili yao na roho yao kutetea uhuru wa nchi zo, wametupiliwa mbali katika upweke wao, ukosefu wa rasilimali na kubaguliwa hadi kufikia umaskini wa kukithiri”. Ndiyo tafakari ya Baba Mtakatifu aliyoitoa katika Kanisa Kuu Katoliki la Mtakatifu Yakobo. Mara baada ya salam ya makaribisho kutoka kwa Askofu Mkuu wa Riga Zbignevs Stankeviès, Baba Mtakatifu ameendelea na hotuba yake kufuatia hotuba ya askofu Mkuu, iliyokuwa inajikita katazama wazee waliopo. Katika Hotuba hiyo anakumbusha kuwa: “ wanaume na wanawake ambao wameishi katika vita ya pili ya dunia, na baadaye katika kipindi kilichofuata, cha kuzuka kwa itikadi za kukana Mungu, na hatari zote zilizo kuwapo wakati ule; wanaume na wanawake walisongwa vikali  na kupata mateso kwa njia ya sera za siasa hadi wengine wakaacha imani yao katika Kristo”.

Treni ya uhuru bila kumbukumbu

“Ninyi mliopo hata mmepata mmjaribiwa,  Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza, hofu ya vita, na baadaye mateso ya sera za kisiasa na hata kukimbia nchi zenu(…) Lakini mmekuwa imara na kuhifadhi imani. Vichwa vingi vilivypamba shaba ndani ya   Kanisa la Mtakatifu Yakobo, kwa hakika wamevumilia kwa ujasiri utawala wa kidikteta, na ule wa kisovietiki bila kuzima imani katika mioyo na kufikia wengine kuweka wakfu katika maisha ya ukleri,, kitawa, makatekista na hata huduma mbalimbali za Kanisa ambazo zilikuwa zinawaweka katika hatari ya maisha”.

Ingawa inaonekana  leo, kwa jina la uhuru, watu wanawashughulikia wazee, wasiwe na upweke, ukosefu wa rasilimali na kutengwa, hata huzuni. Lakini ikiwa ndivyo, hivyo, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, kinachojulikana kama treni ya uhuru na maendeleo huishia kwa wale ambao wamejitahidi kupambania haki, wakiwa behewa lao katika msululu wa mwisho kwa  watazamaji wakati wa sikukuu, wanaheshimiwa na kupewa sifa, lakini wakiwa wamesahauliwa katika maisha ya kila siku ".

Moyo kijana uliofunguliwa katika mapya ya Mungu

Kadhalika katika hotuba yake, wamewatia moyo wote na kuwaalika wasiangukie kuta tamaa , huzuni au kukosa upole na matumaini. Kwa kukumbusha Barua ya Mtume Uakoba anayeomba kubeba kwa uvumilivu na matumaini yasiyoisha, wakati huo kutunza mouo ubaki kina na wala usiwe mgumu bila furaha ya mamo mapya kutoka kwa Mungu. Wao anasema wamepitia kipindi cha nyakati mbalimbali , na ni mashuhuda hai wa dhti katika matatizo mbalimbali , lakini hata wakiwa na zawadi ya unabii, ambao unakumbusha ujana wa kizazi ambacho kinalinda wale waliotanguliwa na ambao wamependezwa na kusifiwa na Mungu, na ambao wanaombolezwa kwa Mungu iwapo yeye amewasahau. Kwa maana hiyo amewaomba wasisahau miziz ya watu , miziz ya vijana chipukiza ambao lazima wachanue na kutoa matunda ,: walinde miziz hiyo na kuhifadhi uhai wake.

 

24 September 2018, 14:15