Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anapokelewa na mtawa wa kimisionari wa upendo na familia ya watoto tisa huko Tallin Papa Francisko anapokelewa na mtawa wa kimisionari wa upendo na familia ya watoto tisa huko Tallin  (ANSA)

Papa:Bwana hachoki kutoa fursa ya kuzaliwa upya:tafuteni mahusiano!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wahudumu wa matendo ya upendo ya Kanisa, Wanashirika wa Wamisionari wa Upendo na wahudumu wa Caritas mahalia. Mkutano huo umefanyika katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo mjini Tallin

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Imani ya wamisionari ndiyo inakwenda njiani, ili furaha kubwa ya Mungu iweze kuzaliwa na kutoa fursa mpya”. Ndiyo maneno yaliyosikika ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa kukutana na wahudumu wa matendo ya upendo ya Kanisa, Wanashirika  wa Wamisionari wa Upendo na wahudumu wa Caritas mahalia. Mkutano huo umefanyika katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo mjini Tallin, tarehe 25 Septemba 2018.

Tengenezeni mahusiano na kutoka nje ya mitaa

Akiendelea na hotuba yake, Papa amesema, “ endeleeni kutengeneza mahusuano na kutoka nje katika mitaa ya miji , ili kuwaambia wote: hata wewe ni sehemu ya familia yetu”. Kwa maana furaha kubwa ya Bwana ni kutuona tunazaliwa kwa upya na kwa maana, yeye hachoki kwamwe kutoa  fursa mpya”. Baba Mtakatifu amesisitiza   hayo kwa wakatoliki ambao wanajikita katika matendo ya Upendo chini Estonia, ambao ni wahudumu wa Caritas, watawa wa mama Teresa wa Kalukuta ambao kwa dhati wanahudumia mamia elfu ya mama vijana waliozaa nje ya ndoa, watu wenye matatizo ya ulevi na wasio kuwa na hali nzuri kimaisha.

Kusikiliza ndugu tisa na watawa

Mkutano wa Baba Mtakatifu umefanyika kabla ya misa ya hitimisho ya ziara yake nchini Estonia, katika Uwanjawa Uhuru wa mji. Baba Mtakatifu amekaribishwa na Paroko wa Kanisa Kuu, Monsinyo Philippe Jourdan, mama mkuu wa Nyumba ya watawa wamisionari wa Upendo na familia moja yenye watoto 9 wanaosaidiwa na watawa hao.

Yesu anahesabu mikono yao

Akiendela na hotua  yake, Baba Mtakatifu amewaaalika waendelee kutafuta mahusiano, na ndiyo wito wake wa mwisho  wa Papa Francisko hasa akihimizai kutoka nje kwenda katika mitaa na kuwambia wote ya kuwa, wanafanya sehemu ya familia kubwa. “ Kama wafuasi ninyi mnaitwa na Yesu ili kuendelea kupanda mbegu na kuonesha ufalme wake. Yeye anahesabu historia yenu, juu ya maisha yenu, mikono yenu kwa ajili ya kwenda katika mji mzima na kushirikishana hali halisi ambayo ninyi mnaishi”.  Swali je Mungu anaweza kuwategemea? Amehitimisha kwa Baraka takatifu akiomba Bwana aweze kutenda miujiza kwa njia ya mikono yao.

26 September 2018, 09:00