Cerca

Vatican News
Papa Francisko akiwa na Rais wa Estonia Bi, Kersti Kaljulaid, Papa Francisko akiwa na Rais wa Estonia Bi, Kersti Kaljulaid,  (ANSA)

Papa Francisko yuko nchini Estonia!

Hatua ya mwisho ya ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu ni nchi ya Estonia, mahali ambapo amefika asubuhi ya tarehe 25 Septemba 2018, katika ndege ya kipapa kutokea mjini Vilnius na ametelemka katika Uwanja wa Kimataifa wa Tallinn na kupokelewa na viongozi wa serikali ya nchi, pia kutembelea Rais wa nchi Bi, Kersti Kaljulaid

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kituo chake cha mwisho wa ziara yake ya Kitume ya siku nne katika Jamhuri za nchi za Kibaltiki (Lithunainia Latvia na hatimaye Estonia) kimetimia. Baba Mtakatifu amefika katika nchi ya Estonia, mahali ambapo amefika  asubuhi ya tarehe 25 Septemba 2018, saa 3.43 masaa mahalia akiwa katika ndege ya kipapa kutokea mjini Vilnius na ametelemka katika Uwanja wa Kimataifa wa Tallinn.

Mara baada ya kupokelewa rasmi katika uwanja wa ndege wa Tallini imefuatia sherehe fupi, katika uwanja wa Ikulu. Na baadaye ametembelea kwa faragha Rais wa nchi ya  Estonia Bi, Kersti Kaljulaid, katika Bustani ya mawaridi ya Nyumba ya Rais.

Ratiba ya siku yake kabla ya kurudi Roma

Baba Mtakatifu baadaye anatarajiwa kuwa na mkutano wa kiekumene na Vijana, katika Kanisa la Kulutheri la Kaarli, na kufuatia chakula cha mchana katika Konventi ya watawa wa Mtakatifu Brigida huko Pirita.

Mchana atakuwa na mikutano ya mwisho: saa 9.15 alasiri anatarajiwa kukutana na watu wanaosaidiwa na  Matendo ya Upendo ya kitume katika Kanisa watakatifu Petro na Paulo; saa 10.30 jini Misa Takatifu katika uwanja wa Uhuru; saa 12.30 jioni,  sherehe za kuagana katika Uwanja wa ndege na tayari kuanza safari ya kurudi Roma, mahali ambapo anatazamiwa kuwasiri Uwanja wa Champino majira ya saa 2.20 za usiku masaa ya Italia.

Kuanza safari kutokea Vilnius

Asubuhi  tarehe 25 Septemba kabla ya kuacha ubalozi wa Vatican huko Vilnis , Baba Mtakatifu amependelea kutoa zawadi ya kipapa, ambayo  ni sanamu ya mti kuchongwa unaowakilisha“ Kristo anayewaza”, sanamu iliyotengeneza na msanii wa Kilithuania Andriaus Kaziukonio. Ni kazi ambayo inahusianana kuwakilisha  utamaduni wa picha za ibada ya watu wa kibaltiki.

Uwanja wa Kimataifa Vilnius

Katika uwanja wa ndege wa Vilnius kumekuwa na sherehe fupi ya kuaga. Papa amepokelewa na Rais wa nchi, Bi Dalia Grybauskaité na kabla ya kuagana amekutana naye kwa faragha dakika chache mahalia ambapo walikuwa wameandaa sehemu hiyo ndani ya ndege. Baba Mtakatifu Francisko ameagwa pia na watu wa kujitolea karibia 200,000 ambao wametumbuiza nyimbo. Na wawili kati yao wamemzawadia Baba Mtakatifu zawadi ya kukumbumbu ya ziara yake.

Telegram kwa Marais wa Lithuania na Latvia

Hata hivyo akiacha mji mkuu wa Vilnius, kwenye ndege iliyo kuwa inampelekea nchini Estonia, Papa Francisko ametuma Telegram mbili  kwa marais wa  Lithuania na Latvia, Bi Dalia Grybauskaité na Raimond Vejonis, ambapo katika telegram hiso anawakikishia baraka ya Mungu ya amani na furaha.

 

 

 

 

25 September 2018, 11:33