Tafuta

Vatican News
Ziara ya Papa nchini Estonia Ziara ya Papa nchini Estonia  (ANSA)

Papa na Vijana wa ekumene:Alipo Yesu ipo radha ya Roho Mtakatifu

Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka juu ya kuweka Kristo kama kitovu: Mahali ambapo Yesu yupo, daima kuna upyaisho, kuna fursa ya uongofu na kuacha yote nyuma yanayo tengenisha kuwa na Yesu na Ndugu. Ndiyo amesisitiza kwa vijana wa kiekumene

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika hotoba ya Papa Francisko kwenye Kanisa Kuu la Kuluteri la Tallini, kwa vijana  amezungumzia juu ya changamoto zinazoikabili safari ya kiekumene na kizazi kipya. Amezungumza hayo mara baada ya kusikiliza wawakilishi wa imani tofauti a kikristo zilizoko nchini Estonia na ushuhuda wa baadhi ya vijana, mahali ambao Papa amesisitiza: “ jinsi gani ilivyo vema kuishi kwa pamoja”.

Akiendelea na hotuba yake anasema, iwapo tunatia bidii ya kutazama jinsi gani wote tuko safarini na  ambao wanafanya safari ya pamoja, tunaweza kujifunza kumfungulia moyo wa imnai mwenzako katika njia bila kumshuku, bila wasiwasi na kutazama tu kile tunachotakiwa kutafuta,yaani amani na uso wa Mungu aliye mmoja. Amani ni shughuli ya fundi wa kiselemala na kuwa na imani kwa wengine kwa maana hata wao wanalo jambo lolote la ufundi. Njia hii inakumbusha kuwa hatutakiwi kutembea peke yetu waamini, lakini kutembea wote kwa pamoja.

Kuishi kwa kumfuasa Kristo

Akiendelea kuwalenga vijana, Papa Francisko amethibitisha kuwa, Makanisa ya Kikristo wakati mwingine wanakumbuka tabia za nyuma ambazo zilikuwa ni  kuzungumza, kushauri tu , badala ya kusikiliza na kwa kujiuliza na kuangazwa na kile ambacho kizazi kipya kinaishi.“Tunatambua kuwa ninyi mtaka na mnasubiri kusindikizwa na siyo kuhukumiwa, iwe kwa mzazi  ambao wanao hofu kubwa na wanazidi kuwalinda sana na kuwazuia sana, wakati ninyi mnahitaji mtu ambaye haogopi udhaifu na kufanya aangazwe na tunu msingi  ambayo ni kama udongo wa mfinyanzi, kuwalinda kwa undani zaidi”. Pamoja na hayo Papa amesema: “ Leo hii ninataka kuwaeleza kuwa tunataka kulia na nyinyi, iwapo nanyi mnalia, kuwasindikiza kwa makofi na vichekesho vya furaha, na kuwasaidia katika kumfuasa Bwana”.

Mahali palipo na Yesu kuna upyaisho

Baba Mtakatifu pia ameongeza kusema kuwa “mahali ambapo kuna ukristo wa kweli, hakuna haja ya kufanya propaganda. Kwa maana jumuiya hiyo inasikiliza, inapokea na kusindikiza”. Ili kuwa karibu na vijana, “ ni lazima kuwapatia majibu, kwa kubadili hali nyingi zinazowafanya waende mbali”. Ni lazima kuwa jumuiya iliyo wazi , inayokaribisha, yenye ikarimu na mvutio, inayojieleza, inyaowezesha, yenye furaha na na ubunifu, kwa maana ya jumuiya isiyokuwa na hofu”.

Kadhalika amesema, “ tunatambua kama mlivyosema kuwa, vijana wengi amwombi lolote zaidi ya kutaka kusikilizwa uwepo wenu”. Lakini anaongeza Baba Mtakatifu,  baadhi wanaomba waachwe kwa amani, kwa maana wanahisi uwepo wa Kanisa unawasumbua hadi kufikia kukera”. Wanachukizwana kashfa za manyanyaso na uchumi,ambapo wanahukumiwa vikali; lakini hivyo ni kutoakana na ukosefu wa uwezo wa kutafsiri vema maisha na utambuzi wa maisha ya vijana katika maandalizi yao; au nafasi nyanu pia  ambayo Kanisa linajikita kuwasaidia vijana”.   “Papa Franciskio amethibitisha kwa vijana ya kwamba, “licha ya ukosefu wa ushuhuda wetu, lakini ninyi endelea  kugundua Yesu katika umbu la jumuiya zake”.”  Kwa maana, tambueni ya kwamba mahali alipo Yesu, daima kuna upyaisho, daima kuna furaha ya uongofu na ili kuweza kuacha nyuma ya mabega kile ambacho kinaleta utenganisho kati ya Yeye na ndugu zake.  Mahali ambapo Yesu yupo, daima kuna maisha na radha ya Roho Mtakatifu. Ninyi leo hii, mnaonja kwa sasa maajabu ya Yesu”.

Upendo haujafa

 “Upendo haujafa, Baba Mtakatifu anabainisha, na kwamba, na unatuita na kututuma”. “Yeye anaomba kufungua moyo tu”. Vijana wengi “ wanatazama upendo unaoisha kati ya wazazi wao, wanaotengua ndoa muda kidogo mara baada ya kuoana; wanafanya uzoefu wa uchungu wa kina wanapoona hakuna anayewajali katika kulazimika  kuhamia nchi nyingine ili kutafuta ajira, au wanatazamwa kwa kushukiwa  sababu ni wageni”. Utafikiri upendo umekwisha, baba Mtakatifu anaendele,  lakini tunatambua kuwa siyo hivyo na tunalo neno la kueleza; jambo la kutanagaza; kwa hotuba ndogo na ishara nyingi”.

Baba Mtakatifu Francisko akimaliza hotuba yake anasema, “hilo ndilo ambalo Yesu anataka kwa maana yeye alipita njia akitenda mema na alipokuwa karibia ya kufa alipendelea maneno ya ishara kubwa ya msalaba: “Tuombe kwa nguvu ya kupelekea Injili kwa wengine, kuitangaza na si kulazimisha, au kwa kutengeneza maisha yetu ya kikristo kama jumba la makumbusho. Maisha ya kikristo ni maisha, ni wakati ujao ni matumani: Siyo jumba la makumbusho. Tuache Roho Mtakatifu atufanye tutafakari historia katika matarajio ya Yesu mfufuka, hivyo Kanisa na katika Makanisa yote yatakuwa na uweo wa kwenda mbele kwa kupokea mshangao wa Bwana!

 

 

 

25 September 2018, 14:47