Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu katika Picha ya Mama wa Mungu huko Aglona mara baada ya Misa Takatifu Baba Mtakatifu katika Picha ya Mama wa Mungu huko Aglona mara baada ya Misa Takatifu  (Vatican Media)

Papa huko Aglona:Karibisha bila ubaguzi,hakuna matumaini katika ubinafsi!

Kukaribisha bila ubaguzi, bila kufikiria kuwa tunaweza kuwa na matarajio na usalama. Ndiyo mambo msingi ambayo yamesikika katika mahubiri ya Papa Francisko wakati wa Misa katika eneo la Madhabahu ya Maria Mama wa Mungu huko Aglona, mji mdogo wa Latvia. Baada ya Misa aliondoka na Helikopta kuelekea mjini Vilnius

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Moja ya hatua msingi ya ziara ya Papa Francisko nchini Latvia ilikuwa ni Misa Takatifu iliyo adhimishwa katika Madhabahu ya Maria, Mama wa Mungu wa Aglona, mji mdogo unaojulikana kutokana na uwepo wa Kanisa Kuu ndogo, lilojengwa kunako mwaka 1700, na maftareli wa kidomenikani na ambapo Mkatifu Yohane Paulo II aliweza kuipa heshima ya kutakaja kama Kanisa Kuu ndogo. Madhabahu hiyo wanatoa ibada ya Picha ya Maria Mama wa Mungu wa Aglona.

Maria yuko karibu na waliobaguliwa

Katika mahubiri yake, Baba Mtakatifu amejikita kukafanua kuwa Maria amesimama wima chini ya msalaba alipowambwa miguu na karibu na Mwanae,  ambapo ni kama vile yupo  karibu na wale ambao dunia ya leo inawakimbia, hata wale ambao wako katika  mchakato, wamehukumiwa wote na kuchukuliwa.

Ni ukaribu ambao siyo mfupi kama matembezi au kufanya safari ya utalii ya mshikamano. Hiyo ina  maana ya  kuteseka na wale wanaoteseka, hali halisi ya uchungu na ili wao wahisi kweli ukaribu, kwa maana wote waliobaguliwa katika jamii wanaweza kufanya uzoefu huo wa Mama ambaye yuko karibu,na ili anayeteseka hasibaki na madonda yaliyofunguliwa ya Mwanae Yesu.

Ushuhuda wa msamaha wa Askofu Sloskans

Maria anajionesha hata kama mama aliye wazi katika msamaha, na anayekataa ubaguzi. Hata hivyo Papa anaonesha kuwam katika hali halisi ya sera za kisiasa, historia za malumbano kati ya watu, bado ni ya uchungu, lakini anasisitiza kuwa mahusiano ambayo yamepanuka, ndiyo yanayofungua undugu na wengine. Papa anatoa mfano wa sura muhimu y Kanisa la Latvia, kwa kutazama hasa Askofu Boleslavs Sloskans, aliyeishi miaka kati ya 1927-1993 katika magereza ya Kisovietiki, kwa kushutumiwa uongo kama mpelelezi.

Kadhalika, Papa amekumbuka maneno yake yanayogusa ya askofu wa Latvia aliyo waandikia wazazi wake: “Ninaombwa kwa moyo wa kina; msiache kutawaliwa na chuki au kuhangaika ndani ya mioyo yenu. Iwapo tunaruhusu hiyo, hatutakuwa wakristo, bali harara”. Mama Maria na mitume wa ardhi hiyo awanawalika wakaribishe na kutoa ahadi mpya juu ya ndugu, na undugu wa ulimwengu katika kipindi ambacho utafikiri kinarudi nyuma hasa tabia ya kutoamini wengine”.

Kukaa karibu na wengine lakini bila kushirikishana

Hata hiyo ameonya juu ya hatari ambayo inaweza kujitokeza wakati unakaa karibu bila kuwa na ushirikishwaji, kwa mfano anasema, inawezekana wanandoa na vijana au watu wazima au wazee wakahisi  ukosefu wa kutazamwa kuwa na mawasiliano baridi.

Baada ya Misa ametoa shukrani kwa wote, katika madhabahu ya Aglona

“Ndugu wapendwa, baada ya kumaliza maadhimisho haya, ninamshukuru Askofu wenu kwa maneno yake aliyo yake aliyonilenga. Ninataka kusema asnte kwa moyo wote kwa wote ambao kwa namna moja au nyingine wamshiriki kuandaa ziara hii. Kwa namna ya pekee, utambuzi wa Rais wa Jamhuri hii na viongozi wote wa nchi kwa makaribisho”. "Ninatoa zawadi kwa Mtakatifu Mama wa Mungu wa Ardhi hii ya Maria , kwa namna ya pekee Rosari maalum: Bikira awalinde na kuwasindikiza daima".

25 September 2018, 10:33