Tafuta

Papa akisungumza na waandishi wa habari wakati wa kurudi Roma Papa akisungumza na waandishi wa habari wakati wa kurudi Roma 

Papa kuhusu Mkataba na China: njia ni mazungumzo!

Makubaliano kati ya China, ndiyo ilikuwa jibu mojawapo la Papa Francisko lililokuwa linasubiriwa na waandishi wa habari wakati wa safari ya kurudi kutoka nchi za Kibaltiki. Na kati ya mada zilizogusiwa na Papa ni zile za kulinda utambulisho wa Jamhuri tatu za Kibaltiki, shutumu dhidi ya silaha, na manyanyaso kwa upande wa wakleri

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko kwa  siku nne na ambapo amejikuta kukabiliana na majeraha ya kumbukumbu inayo wajumuisha nchi za Lithuania, Latvia na Estonia, sera zao za kisiasa ambazo zinaelekeza magharibi na mizizi ambayo inawaunganisha kwa upande, kujikita katika kutazama wakati endelevu, ndiyo mara nyingi Papa  ameweza kuwatakia matarajio mema katika ishara ya matumaini na udhati wa mapatano. Amethibitisha hayo, akiwajibu wahandishi wa habari, wakati wa kurudi kutoka katika ziara yake ya kitume nchi za kilabaltiki tarehe 25 Septemba 2018.

Utambulisho wa kuhifadhi

Katika nchi tatu alizotembelea, Baba Mtakatifu amezidi kusisitiza katika  kila safari juu ya kuhifadhi utambulisho wa nchi za kibaltiki, mahali ambapo mara nyingi zimekanyagwa chini na maingilio ya ukatili, na kulindwa na wale ambao jana walikuwa wanajifanya kama ngazo ya udikteta,lakini leo hii ni wazee ambao wana jukumu la kuonesha kwa kizazi kipya utamaduni, imani na sanaa. Baba Mtakatifu pia akizungumza na wandishi akifikria Jumba la Makumbusho ya waathirika huko Vilnius, na kushutumu vikali juu ya vurugu au kashfa  ya biashara haramu ya silaha ambazo zinaendelea kutengenezwa. Baba Mtakatifu amesema, ndiyo inaruhusiwa na kutoa sifa, kusaidia na kulinda uzalendo, lakini hata Serikali lazima zichukue hatua madhuti kwa kufikiria kwa maamuzi bora  na sio kwa ukatili katika zoezi la kiulinzi.

China, busara katika makubaliano

Baba Mtakatifu katika kuelezea juu ya makubaliano yaliyotiwa saini hivi karibuni kunako tarehe 22 Septemba 2018, kati ta Vatican na Jamhuri ya watu wa China. Makubaliano ya muda na China ni suala ambalo baada ya kufika Lithuania, yalibadili mtazamo zaidi kutoka mashariki na kuweka umakini wa wataalam wa mambo ya vatican. Swali: Uchambuzi juu ya  hatua ya mchakato uliokomaa kwa mara nyingine Jumamosi iliyopita, ambao Vatican  wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka kumi, imejulikana kwamba, Vatican walikuwa  "kuuza" Kanisa huko Beijing.

Baba Mtakatifu kwa utulivu amesema: Mkataba nilisaini mimi; mimi ndiye mhusika, na pia kuongeza kuomba “ kusali” kwa ajili ya wale ambao kwa miaka mingi wameishi nyuma ya Kanisa mafichoni, na leo hii hawaelewi wigo wao“.  “Kila makubaliano ya amani”, anakumbusha, “ sehemu zote mbili wanapoteza jambo”,  lakini wakati huo sasa  “ Ni Papa atateua Maaskofu wa China”. Papa Francisko amesifu “ uvumilivu” na  “busara” ya wanamichakato wa Vatican, kuanzia kwa Kardinali Pietro Parolin, Monsinyo Celli na Padre Rota Graziosi na wote ambao wamewezesha  kufanya  tathmini za "hati" zote za Maaskofu ambao walikuwa bado hawajapata kutambuliwa na Vatican na ambao wanaomba kuwa  sasa sehemu ya kipapa, na ambao watawezeshwa kwa siku ambazo siyo mbali.

 Imani kubwa ya watu wa China

Hata hivyo Papa Francisko ameonesha kuwa watu wa china ni wenye mchango mkubwa wa imani ya wakatoliki ambao wamejaribiwa kwa kipindi kirefu. Kwa maana hiyo katika “makubaliano hayo anao utambuzi wa mateso  yao na kuonesha kuwa : katika fursa ya habari kutoka kwa Balozi mstaafu wa Vatican , alikuwa wametoa msukumo kwa maaskofu wengi kujieleza na kuwa karibu hata waamini wa China ambao wametia saini kwa namna ya kipekee, katika Kanisa la kiutamaduni na lisilo la kiutamandi, kwa barua moja ya pamoja kumtumia Papa kwa kumweleza mshikamano wao. Kutokana na barua hiyo Papa amethibitisha ilikuwa “kama ishara”.

 

26 September 2018, 10:29