Tafuta

Vatican News
Katekesi ya Papa Francisko 22 Agosti 2018 Katekesi ya Papa Francisko 22 Agosti 2018  (Vatican Media)

Papa:Wapo wenye uhusiano na jina la Mungu kinafiki !

Baba Mtakatifu katika katekesi yake anasema ni vema kusikiliza. Neno, usilitaje jina, linajieleza maana yake katika lugha ya kiyahudi na kama ilivyo katika lugha ya kigiriki tafsiri yake ni kwamba utalibeba, japokuwa bila kuelemewa. Tusitumie jina hilo kinafik na desturi kwasababu ni desturi na si kwa moyo na ulaghai

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wapendwa ndugu na kaka habari za asubuhi! Tuendelee na Katekesi kuhusu amri za Mungu na leo hii kwa kujikita katika amri isemayo “usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako ( Kut 20, 7) Kwa hakika tunasema neno hili kama mwaliko wa wa kuacha kudharau jina la Mungu na kuzuia kilitumia bila sababu yoyote. Hiyo ina maana wazi ambapo inatuandaa kwa kina zaidi katika maneno msingi hasa ya kutolitumia jina la Mungu bure na  bila sababu yoyote.

Ni utangulizi wa tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake ya kila Jumatano tarehe 22 Agosti katika ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI mjini Vatican kwa waamini na mahujaji wote. Baba Mtakatifu anaendelea kusema ni vema kusikiliza. Neno: usilitaje jina, linajieleza maana yake katika lugha ya kiyahudi na kama ilivyo  katika lugha ya kigiriki tafsiri yake ni kwamba  utalibeba, japokuwa bila kuelemewa.

Maelezo ya usilitaje bure, linajieleza bayana na linataka kusema kuwa: ni utupu, na ubatili” Ni kutaka kujifafanua zaidi katika kuelezea juu ya kitu fulani ambacho kiko wazi, na mfano wa ukosefu wa jambo fulani. Ndiyo tabia ya unafiki, ya desturi kwasababu ni desturi na si kwa moyo … na ulaghai. Hiyo ina maana ya  kutumia maneno au kutumia jina la Mungu lakini kwa utupu bila ukweli ndani yake.

Jina katika Biblia ni ukweli wa kina wa mambo hasa ya watu na jina linawakilisha utume; kwa mfano Ibahimu katika kitabu cha Mwanzo (7,5) na Simoni Petro katika Injili  ya Yohane (1,42) , walipokea jina jipya ili kuwaelekeza mabadiliko ya mwelekeo wa maisha yao. Na kutambua vema jina la Mungu linapelekea mabadiliko ya maisha binafsi: kwa maana tangu wakati huo Musa alipotambua jina la Mungu katika historia alibadilika ( taz Kut 3,13-15). Jina la Mungu katika liturujia za kiyahudi, lilikuwa likitamkwa kwa  sikukuu  ya  Siku ya Toba  kubwa  na watu walikuwa wanasehemewa kwa  sababu, ilikuwa ni kwa njia ya jina, walikuwa wanawasiliana na maisha yenyewe na Mungu ambaye ni huruma.

Kwa maana hiyo kutumia jina binafsi la Mungu, ina maana ya kuchukua sisi binafsi hali halisi na kuingia katika mahusiano ya nguvu, katika uhusiano wa dhati na yeye. Kwa wakristo, Baba Mtakatifu anaongeza: amri hiyo ni wito wa kukumbusha kuwa tumebatizwa, lakini je namna gani?   ni kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu , kama inavyothibitisha kila mara tunapofanya ishala ya msalaba, ili kuweza kuishi matendo yetu ya kila siku katika muungano wa kina na wa kweli na Mungu yaani katika upendo wake.

Wafundishe watoto wafanye isala ya msalaba vizuri

Kwa upande wa ishala ya Msalaba, Baba Mtakatifu Francisko amependa  kwa mara nyingine tena kusisitiza juu ya kuwafundisha watoto wafanye ishala ya msalabavevama kwa maana anasema,ukimwambia mtoto afanye ishala ya msalaba, yeye ataonesha kwa matendo (wanaigiza kufanya ishala ya msalaba kwa ishara). Wao wanafanya jambo ambalo hawajuhi ni kitu gani. Kwa maana hawajuhi kufanya ishala ya msalaba!

Kutokana na suala hilo amesisitiza wawafundishe kufanya ishala ya msalaba vizuri, kwa manaa hiyo ndiyo tendo la imani kwa watoto. Na ndiyo zoezi lao kwao alilowakabidhi kwa mara nyingine tena! Kadhalika Baba Mtakatifu ameendelea, je inawezakana kijichulia jina la Mungu kwa namna ya unafiki na kama desturi na utupu? Jibu lake  amesema, kwa bahati mbaya ni chanya, kwa maana ni ndiyo inawezekana. Inawazekana kuishi uhusiano ana uongo na Mungu.

Walimu wa sheria wa uongo.

Katika kusisitiza hili na mifano hai amesema: Yesu aliwambia walimu wa sheria, kwa maana walikuwa wanafanya mambo lakini hakuwa wanatenda yale ambayo Mungu alikuwa anataka. Walikuwa wanazungumza mambo ya Mungu lakini walikuwa hawatendi mapenzi ya Mungu. Na Yesu aliwapa  ushauri watu wake kuwa fanyeni kile wanacho wambia lakini wasifanye  kile ambacho wanatenda. Kwa maana hiyo inaonesha jinsi gani inaweza kushi uhusiano wa uongo na unafiki na Mungu kama watu wale. Neno  la amri Kumi za Mungu ndiyo mwaliko hasa wa kuwa na uhusiano na Mungu ambaye siyo mlaghai, hana unafiki, na ambaye anaweza kuamini yeye kwa namna jinsi tulivyo. Na hiyo kwa kichini chini utaimbua siku  ambayo utafanya uzoefu wa kuguswa na mkono wa Mungu, lakini kinyume na hiyo ni kufanya nadharia tu anathibitisha Baba Mtakatifu.

Huo ndiyo ukristo ambao unagusa mioyo, yaani kukutana na Mungu kwa dhati. Je ni kwanini watakatifu wamekuwa na uwezo wa kugusa mioyo?  kwa nini watakatifu hawazungumzi tu bali wanavuta mioyo! Mtu mtakatifu anavutia moyo unapozungumza naye na kueleza jambo. Wao wanao  uwezo kwasababu ni katika watakatifu wanaona kile ambacho moyo kwa kina unatamani; uwazi, uhusiano wa kweli na shina. Hao wanaonekana watakatifu katika mlango wa karibu jinsi walivyo kwa mfano, wazazi wengi ambao wanatoa mfano bora  kwa watoto wao, kuwaonesha katika maisha ya dhati na kweli, urahisi, ukarimu na uadilifu

Iwapo wakristo wanaongezeka na ambao wanachukua jina la Mungu bila unafiki na kujikita katika matendo ya ombi la kwanza la Baba Yetu Jina la lako litukuzwe, tangazo la Kanisa kwa dhati linasikilizwa na matokeo ya kuaminiwa. Iwapo maisha yetu ya dhati yanajionesha katika Jina la Mungu, ni kuonesha jinsi gani Ubatizo ulivyo mzurii na zawadi kubwa ya Ekaristi!  Jinsi gani ulivyo mzuri umoja ambao upo kati ya mwili wetu na mwili wa Kristo: Kristo ndani yetu na yeye ndani mwetu na sisi ndani mwake! Wote ni kuungana ! Huo si unafiki ni ukweli . Huko si kuzungumza au kusali kama kasuku, huko ni kusali kwa moyo, na kupenda Bwana.

Tangu msalaba wa Kristo na kuendelea, hakuna yoyote anaweza kujidharau na kuwa na hisia mbaya  uwepo wake, hakuna na kamwe! Kwa kila chochote alichotenda. Kwasababu Jina la kila mmoja wetu ni juu ya mabega ya Kristo. Yeye anatubeba. Hatuna budi kuchukua juu yetu jina la Mungu kwasababiu yeye alibeba jina letu hadi mwisho, hata katika mabaya yaliyopo ndani mwetu;

Yeye alijitwisha ili kutusamehe, na kutuwezesha kuweka mioyo yetu upendo wake. Kwa njia hiyo Mungu anatangaza amri hiyo nibebe juu yako, kwasababu mimi nimekubeba juu yangu. Yoyote atakaye taja jina Takatifu la Bwana ambaye ni upendo mwaminifu na huruma, katika hali yoyote anayojikuta nayo, Mungu hawezi kamwe kusema hapana kwa moyo ambao unamtaja na kumwomba kwa dhati. Basi turudi katika zoezi la kufanya nyumbani: kufundisha watoto kufanya ishala ya msalaba vizuri Je mtafanya? Ifanyike vizuri. Asante.

22 August 2018, 16:22