Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake, Jumatano tarehe 8.8.2018 Baba Mtakatifu Francisko wakati wa katekesi yake, Jumatano tarehe 8.8.2018  (Vatican Media)

Mtakatifu Theresa Bernadetha wa Msalaba, liombee Bara la Ulaya!

Tarehe 9 Agosti ya kila mwaka, Kanisa linaadhimisha kumbu kumbu ya Mtakatifu Theresa Bernadetha wa Msalaba, maarufu kama Edith Stein. Shuhuda wa imani na mwanamke wa shoka, aliyejibidisha kumtafuta Mungu katika uaminifu na upendo; shuhuda wa ndugu zake Wayahudi na Wakristo, daraja la majadiliano ya kidini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, mwishoni mwa katekesi yake kuhusu Amri za Mungu na kishawishi cha binadamu kutaka kuabudu miungu vitu na watu, Jumatano tarehe 8 Agosti 2018, amewakumbusha waamini kwamba, tarehe 8 Agosti 2018, Kanisa limefanya kumbu kumbu ya Mtakatifu Dominico Guzman, Mwanzilishi wa Shirika la Wadominican, maarufu sana kwa kuhubiri. Mtakatifu Dominico alikuwa mtumishi mwaminifu wa Kristo na Kanisa lake, mfano bora wa kuigwa na waamini, na hasa zaidi, wale wote wanaoitwa kwa jina la Dominico.

Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba, tarehe 9 Agosti 2018, Kanisa linaadhimisha kumbu kumbu ya Mtakatifu Theresa Bernadetha wa Msalaba, maarufu kama Edith Stein. Shuhuda wa imani na mwanamke wa shoka, aliyejibidisha kumtafuta Mungu katika uaminifu na upendo; shuhuda wa ndugu zake Wayahudi na Wakristo, daraja la majadiliano ya kidini. Baba Mtakatifu anamwomba, Mtakatifu Theresa Bernadetha wa Msalaba, aliombee Bara la Ulaya ili lisikumbwe na ubaridi. Mwenyezi Mungu apewe sifa na mwanadamu na akombolewe!

Sikiliza kwa raha zako mwenyewe!

 

08 August 2018, 15:13