Cerca

Vatican News
Sala ya Papa mbele ya picha ya Mama Maria kukabidhi ziara yake ya kitume Sala ya Papa mbele ya picha ya Mama Maria kukabidhi ziara yake ya kitume  (Vatican Media)

Ireland inamsubiri Papa Francisko katika ziara hii ya upyaisho!

Tendo la Baba Mtakatifu ambalo analifanya kila wakati kabla ya kuanza ziara yake, iliyo yoyote ya kitume ni desturi ya kwenda katika Kanisa Kuu la Mama afya ya watu wa Roma ili kukabidhi ziara yake kwa Mama Maria, hivyo tarehe 24 Agosti 2018 jioni alikwenda katika Kanisa Kuu na kuingia katika Kikanisa Kidogo na kupiga magoti kwa kusali na kuweka ua.

Sr Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ameondoka asubuhi hii  kuelekea katika Ziara yake ya 24 ya Kitume asubuhi ya leo ya tarehe 25 Agosti kuelekea nchini Ireland. Huko anasubiriwa na waamini wa Ireland,  maelfu na maelfu ya familia kutoka mabara matano katika Mkutano ambao ni kwa ajili yao.

Francesco asali katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria

Tendo la Baba Mtakatifu ambalo analifanya kila wakati kabla ya kuanza ziara yake, iliyo yoyote ya kitume ni ile desturi ya kwenda katika Kanisa Kuu la Mama afya ya watu wa Roma, ili kukabidhi ziara yake kwa Mama Maria, ni desturi yake kwa muda mrefu  na hivyo tarehe 24 Agosti 2018 jioni  alikwenda  katika Kanisa Kuu na kuingia katika  Kikanisa Kidogo mahali ambapo ipo picha ya Mama Maria  akiwa na ua mkononi, alipiga  magoti mbele ya Picha ya Bikira Maria na kusali.

Katika tweet na baadhi ya picha zilizowekwa na Msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Greg Burke, zinaonesha Papa katika ziara hiyo mchana Katika Madhabahu ya Bikira Maria, ikiwa ni katika mkesha wa ziara ya  kitume ya siku mbili 25-26 Agosti nchini Ireland!

Baba Mtakatifu ataadhimisha hitimisho la Mkutano wa familia  duniani ambao umefunguliwa tangu 21 Agosti 2018.

Kadhalika wanamsubiri kwa hamu kubwa katika Tamasha la Familia 25 Agosti  jioni katika Uwanja wa Crocke, wakati huohuo hata kumsikiliza msaniii maarufu Andrea Bocelli ambaye ataweza kutumbuiza mbele ya Baba Mtakatifu na Familia nzima iliyounganika katika Mkutano huo wa kipekee kwa ajili ya familia nzima duniani. Jukwaa la Misa Takatifu Jumapili 26 Agosti katika Uwanja wa Phoenix umeandaliwa tayari, ambao unakadiliwa watu milioni moja kuudhuria Misa Kuu Takatifu hya itimisho la  Mkutano wa Familia Duniani ambao unaongozwa na kauli mbiu Injili ya Familia isema Injili ya Familia: Furaha ya uUlimwengu ambayo imekuwa na mwangwi wa Wosia wa Kitume wa Papa Francisko wa Amoris Laetitia yaani Furaha ya upendo ndani ya familia.

25 August 2018, 09:08