Tafuta

Vatican News
Katekesi ya Papa Francisko tarehe 29 Agosti 2018 imehusu Ziara yake ya Kitume nchini Ireland Katekesi ya Papa Francisko tarehe 29 Agosti 2018 imehusu Ziara yake ya Kitume nchini Ireland  (Vatican Media)

Papa:Tambua ndoto ya Mungu ni umoja, maelewano na amani!

Baba Mtakatifu amesema kuwa uwepo wake Ireland ulikuwa unataka hasa kuimarisha familia za Kikristo katika wito na utume wake. Maelfu ya familia, wanandoa, bibi, babu na watoto walifika mjini Dublin kwa lugha mbalimbali, utamaduni na uzoefu, ambavyo vilikuwa ni ishara madhubuti ya uzuri wa ndoto ya Mungu kwa ajili ya familia nzima ya binadamu.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican News

“Kaka na dada habari za asubuhi…. Mwishoni mwa wiki iliyopita nilitimiza ziara yangu nchini Ireland ili kushiriki Mkutano wa Familia Duniani. Nina uhakika hata ninyi mmeona na kufuatilia kwa njia ya Televisheni. Uwepo wangu ulikuwa unataka hasa kuimarisha familia za Kikristo katika wito na utume wake. Maelfu ya familia, wanandoa, bibi, babu na watoto walifika mjini Dublin kwa lugha mbalimbali, utamaduni na uzoefu, ambavyo vilikuwa ni ishara mathubuti ya uzuri wa ndoto ya Mungu kwa ajili ya familia nzima ya binadamu”

Ndiyo utangulizi wa Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 29 Agosti 2018, wakati wa kuanza katekesi yake katika viwanja vya Mtakatifu Petro Mjini Vatican kwa waamini na mahijaji wengi kutoka pande za dunia. Katekesi ya siku imejikita kwa kina kuelezea juu ya ziara yake ambayo amehitimisha nchini Ireland na kwa maana hiyo anasema: Sisi tunatambua kuwa, ndoto ya Mungu ni umoja, maelewano na amani.

zawadi ya msamaha na mapatano

Katika familia na duniani, tunda la uaminifu, msamaha, la mapatano ambayo yeye alituzawadia kwa njia ya Kristo. Yeye anaalika Familia kushiriki ndoto hiyo na kuifanya katika dunia ambayo ni nyumba mahali ambapo hakuna anayehisi upweke, hakuna anayehisi kutopendwa na hakuna yeyote anayebaguliwa. Fikirieni vizuri hilo, Baba Mtakatifu anasisitiza pia kwamba: Kile ambacho Mungu anataka ni kwamba hakuna yoyote awe peke yake na wala asiwepo yoyote hasiyetakiwa na kubaguliwa! Kutokana na hili ndiyo maana kwa dhati kauli mbiu ya Mkutano wa dunia ilikuwa inasema: Injili ya Familia, furaha ya ulimwengu!

shukrani na kiini cha ziara

Ninatoa shurakani kubwa kwa Rais wa Ireland, Waziri Mkuu na viongozi mbalimbali wa Serikali, raia na dini, kama pia watu wengi kwa kila ngazi ambao wameshiriki kuandaa na kufanikisha tukio hili la Mkutano. Asante sana Maaskofu ambao wamefanya kazi sana! Aidha Baba Mtakatifu amesema kwamba” Nikihutubia kwa viongozi wa nchi katika nyumba ya kifalme huko Dublin, nimesisitiza kuwa, Kanisa ni familia ya familia na jinsi gani mwili na viungo vyake kwa pamoja ni muhimu katika nafasi ya maendeleo ya jamii moja ya kindugu na mshikamano.

Hata hivyo, kiini cha kweli na chenye mwanga, katika siku hizo kilikuwa ni ushuhuda wa upendo wa wanafamilia uliotolewa na wanandoa wa kila rika. Historia zao zimekumbusha kuwa, upendo wa ndoa ni moja ya zawadi maalum ya Mungu ambayo inatakiwa kuiimarisha kila siku katika “Kanisa la nyumbani” ambalo ni familia. Jinsi gani dunia hii inahitaji mapinduzi ya upendo, Baba Mtakatifu anathibitisha na kusema, hayo ni mapinduzi ya utu wema, ambao unaokoa utamaduni wa sasa wa muda mfupi! Na mapinduzi haya yanaanzia katika moyo wa familia.

Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria mjini Dublin

Katika Kanisa Kuu la mjini Dublin, nilikutana na wanandoa wanaojikita katika Kanisa na wanandoa vijana na watoto wadogo wengi. Nilikutana na baadhi ya familia nyingine zinazokabiliana na changamoto na matatizo maalum. Asante sana Mafrateli wakapuchini ambao wako karibu na watu daima na familia kubwa ya Kanisa wakifanya uzoefu wa mshikamano na usaidizi ambao ni tunda la upendo.

Tamasha la familia na ushuhuda

Kipindi mwafaka cha ziara yake, Baba Mtakatifu anathibitisha ilikuwa ni tamasha kubwa la familia lililofanyika Jumamosi usiku. Katika mkesha walisikiliza ushuhuda wenye mguso wa familia ambazo zimeteseka na vita; familia ambazo zimepyaishwa kwa njia ya msamaha; familia ambazo upendo umeokoa ile tabia ya madawa ya kulevya; familia ambazo zimejifunza jinsi gani ya kutumia simu za mkono, tablet na kuweza kutoa kipaumbele cha kukaa kwa pamoja. Hapo imeonesha hata thamani ya mawasiliano kati ya kizazi na nafasi maalum kwa upande wa babu na bibi katika kudumisha mahusiano ya familia na kuonesha tunu ya imani.

Baba Mtakatifu katika hili amesema: ni vigumu kutamka, lakini ni bora kulisema, kwa maana utafikiri wazee wanasumbua. Katika utamaduni wa ubaguzi, babu na bibi wanabaguliwa na kuwekwa pembezoni. Lakini wazee ni hekima, pia ni kumbukumbu ya watu, kumbukumbu ya familia! Wazee lazima waoneshe kumbukumbu kwa vikujuu vyao. Vijana na watoto lazima wazungumze na babu zao ili kupeleka historia mbele. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ameomba tafadhali wasibaguliwe wazee, lazima wawe karibu na watoto wao na wajukuu zao!

Madhabahu ya Bikira Maria huko Nock

Siku ya Jumapili, Baba Mtakatifu anasema, alivyo fanya ziara yake katika Madhabahu ya Bikira Maria wa Knock, ambayo inapendwa na watu wa Ireland. Katika Kikanisa cha matokeo ya Bikira Maria, amekabidhi familia zote chini ya ulinzi wake mama Maria kwa namna ya pekee nchi ya Ireland. Lakini pamoja na kwamba katika ziara yake, haikuwapo ratiba ya kwenda Ireland Kaskazini, alipendelea kutoa salam za upendo kwa watu hao na kuwatia moyo uli mchakato wa mapatano, amani, urafiki na ushirikiano wa kiekuemene uweze kufanikiwa.

Ushiriki wa mateso kwa ajili ya wathirika

Ziara hiyo ya kutembelea Ireland, licha ya furaha, Baba Mtakatifu amesema, alikuwa pia aweze kushiriki kubeba uchungu na hasira za mateso yaliyosabishwa katika nchi hiyo na baadhi ya mitindo mbalimbali ya manyanyaso, hata kwa upande wa wahusika wa Kanisa. Tukio hilo lilitokana na kwamba, kwa upande wa Kanisa katika nyakati zilizopita hawakutambua kukabiliana uhalifu huo vya kutosha. Ishara ya kina ambayo imefanyika katika mkutano huo, ni ile ya kukutana na waathirika hali nane, ambao yeye binafsi ameowaomba msamaha kwa Bwana kwa dhambi hizi na kashfa na kwa maana ya kusali kwa ajili ya yote waliyotendewa. Maaskofu wa Ireland wameanza kwa dhati mchakato wa uongofu na mapatano na wale ambao wwalio athirika na manyanyaso hayo na kwa msaada wa vyombo vya taifa, wameweka sheria kali ili kuhakikisha usalama wa vijana.

Mkutano wa maaskofu wa Ireland na kuwatia moyo

Na katika mkutano na Maaskofu, Baba Mtakatifu anathibitisha, aliwatia moyo katika juhudi za kuondoa kule kushindwa kwa wakati uliopita kwa ukarimu na ujasiri, wakikabidhi yote katika ahadi ya Bwana na kuhesabu juu ya imani ya kina ya watu wa Ireland katika matarajio ya kuona kipindi cha upyaisho wa Kanisa la Ireland. Mkutano wa Familia duniani mjini Dublin kwa dhati umekuwa ni uzoefu wa kinabii, uliotiwa nguvu na familia nyingi ambazo zijanajikita katika njia ya ndoa ya kiinjili, ya maisha ya familia; familia kama wafuasi, umisonari chachu ya wema, utakatifu, haki na amani

Onyo na ushauri

Sisi tunasahau familia nyingi tena nyingi! Ambazo zinapeleka mbele watoto, kwa imani wakiomba msamaha inapojitokeza matatizo. Tunasahau kwasababu leo hii ni mtindo katika magazeti au majarida, kuongea hivi: huyo amepata talaka na Yule yuko hivi… ni talaka… Lakini tafadhali, Baba Mtakatifu ameonya: haya maneno ni mbaya: ni kweli kuwa iwapo mimi ninaheshimu mmoja, lazima kuwaheshimu watu, lakini wazo siyo talaka, wazo siyo kuachana, wazo siyo uharibifu wa familia. Wazo ni familia iliyoungana. Na ndiyo wazo la kuendeleza mbele na ndiyo wazo Baba Mtakatifu amehimiza.

Mkutano wa Familia duniani 2021

Mwisho wa katekesi yake amehitimisha akigusia juu ya Mkutano wa famila dunia ambao utafanyika Roma mwaka 2021. Kwa maana hiyo amesema kukabidhi yote kwa ulinzi wa Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu kwasababu katika nyumba zao, parokia na jumuiya wanaweza kuwa kweli furaha ya ulimwengu.

29 August 2018, 14:15