Cerca

Vatican News
Barua ya Papa Francisko kwa Stephen Walford na kitabu chake Barua ya Papa Francisko kwa Stephen Walford na kitabu chake 

Barua ya Papa kwa Walford:Wosia wa Amoris Laetitia usomwe wote!

Kitabu cha Stephen Walford chenye kichwa cha Papa Francisko, familia na talaka. Utetezi wa Ukweli na Huruma, kinajikita kufafanua Wosia wa Amoris Laetitia, mahali ambapo Gazeti la Civilta’ Cattolica , limetoa barua kamili ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Bwana Waldford akimpongeza kwa kazi hiyo ambayo ni tunda la sala na tafakari

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Franciko amemwandikia barua Stephen Walford Mtaalimungu , ambaye ni  baba wa Familia kama shukrani utunzi wake wa  kitabu  ambacho kinahusu Amoris Laetitia yaani Furaha ya Upendo ndani ya Familia. “Wosia wa Kitume, unatokana na shauku ya nguvu ya kutafuta mapenzi ya Mungu kwa ajili ya kuhudumia Kanisa , kwa maana hiyo ni bora kuusoma waraka huo wote”, anabainisha Baba Mtakatifu.

Barua ya Papa kwaWalford:Wosia wa Amoris Laetitia usomwe wote

Kichwa cha kitabu cha mtaalimungu  Bwana Stephen Waldford  katika lugha ya kingereza  “Pope Francis, the family and divorce. In Defense of Truth and Mercy”,  kwa maana ya “Papa Francisko, familia na talaka.Utetezi wa  Ukweli na Huruma”, kinajikita kufafanua Wosia wa Amoris Laetitia, mahali ambapo Gazeti la Civilta’ Cattolica , limetoa barua kamili ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Bwana Waldford.

Ni barua uliyotumwa na Baba Mtakatifu mnamo Mosi Agosti mwaka jana, ambayo kwa namna ya pekee imesaidia kuboresha kitabu hicho kwa ufasaha zaidi. Hiyo ni kwasababu, Papa Francisko anamwelekea akisema: si tu mtaalimungu kama mwandishi wa kitabu hicho katika mafundisho ya muziki, lakini pia kama baba na kusititiza jinsi gani, matatizo mengi leo hii yanayokumba familia, yanaweza kukabiliwa katika Wosia wa Kitume, lakini akisisitizia umuhimu wa kuusoma wosia  wote.  Katika barua yake pia, Baba Mtakatifu anakumbuka kwa upendo mkuu wa ziara mwandishi wa kitabau mjini Vatican mwaka jana alipotembelea akiwa na familia yake, na kuelezea kama udhati kwamba ni  kielelzeo cha Amoris Laetitia. Kadhalika anaonesha mayaba mambo kadhaa yaliyomo katika wosia ambao unajulikana na kama tunda la sala inayojikita katika huduma.

Kutafuta namna ya kuhudumia

Baba Mtakatifu anaandika katika Wosia wa Amaros Laetitia kwambani tunda la mchakato wa muda mrefu wa Kanisa ambalo limejihusisha na Sinodi mbili na matokeo ufafanuzi na mchango mkubwa  kutoka katika Makanisa mahalia duniani  kwa njia ya mabaraza ya maaskofu. Kadhalika hata kwa ushirikiano wa taasisi taasisi mbalimbali za maisha ya kitawa na taasisi nyingine kama vile Vyuo Vikuu Katoliki na vyama mbalimbali vya kilei. Anathibitisha ya kwamba, Kanisa zima limesali, limetafakari na kwa urahisi likaweza kutoa mchango wa dhati kwa namna nyingi. Na  hivyo anathibitisha ya kuwa Sinodi zote mbili ziliwakilisha hitimisho lao.

“Moja ya mambo ambayo yalinigusa katika mchakato wote ni ile shuuku ya kutafuta mapenzi ya Mungu kwa ajili ya kuhudumia vema Kanisa”.  Anarudia kusisitiza: “Kutafuta kuhudumia”! kwa maana hiyo Wosia huo umetokana na njia ya tafakari, kubadilishana mitazamo na maono, kusali na kung’amua. Lakini pamoja na hayo anaendelea bila kuficha ya kuwa , kumekuwapo hata vishawishi wakati wa mchakato huo, japokuwa  Roho njema imeongoza na imeonekana; na kutokana na ushuhuda, umeweza kuonesha furaha ya kiroho.

Kusoma wosia wote bila kuumega vipande vipande

Zaidi katika barua yake Baba Mtakatifu anasisitiza juu ya fursa nzuri ya kuusoma wosia wa Amoris Laetitia kuanzia mwanzo hadi mwisho kwani, kila kitu ndani ya wosia kinafuata mfululizo na haiwezekani kuusoma vipande vipande.  Hiyo ina maana kwamba ndani ya Wosia kuna maendeleo, iwe kwa upande tafakari ya kitaalimungu na katika mtindo ambao unakabiliana na matatizo. Iwapo Wosia hautasomwa wote  kamili jinsi ulivyo na mpangilio wa tema zake, itakuwa vigumu kuutambua vema  au ipo hatari ya kuupindisha na kuuondoa maana yake kamili.

Udhati wa Kanisa

Baba Mtakatifu anathibitisha, kwa hakika, kitabu cha Waldford kinaweza kuwa muhimu katika familia nyingi kwasababu kinakabiliana na matatizo yanayo wakumba familia nyingi kwa udhati wake wa kina  na chini ya mantiki za dhati kama ilivyo Wosia wa Amoris Laetitia inayotazama hata hali tofauti zinazohusu maadili, kwa kutafuta hata mtindo wa mafundisho ya Mtakatifu Tommaso d’Aquino.

Katika mchakato wa Wosia huo, Baba Mtakatifu ameonesha  matatizo ya sasa na ya kweli, kama vile familia duniani leo hii, elimu ya watoto, maandalizi ya ndoa, familia na matatizo yake  na mengine mengi. Tema hizi zimegusiwa kwa ustadi kabisa katika Wosia wa Amoris Laetitia na kwa udhati wa Mafundisho ya Kanisa, ambayo daima itaendelea bila kumegeka pamoja na kwamba daima inajikita katika mchakato wa hija ya ukomavu!

Barua ya Baba Mtakatifu inahitimishwa na salam kwa mke wake na watoto wa Stephen Walford na kushukuru kwa ajili ya ushuhuda wao wa maisha na zaidi ya hayo bila kusahau tabia yake kuomba nao wasali kwa ajili yake!

24 August 2018, 10:55