Tafuta

Vatican News
Watumishi Altareni kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanakutana na Papa Francisko 31 Julai 2018. Watumishi Altareni kutoka sehemu mbali mbali za dunia wanakutana na Papa Francisko 31 Julai 2018. 

Watumishi Altareni wajenzi wa amani wanakutana Roma!

Kuanzia tarehe 30 Juali 2018 hadi tarehe 3 Agosti 2018, Mji wa Roma umefunikwa na watumishi wa Altareni zaidi ya sitini elfu, kutoka sehemu mbali mbali za dunia, walioitikia mwaliko wa “Associazione Internationalis Ministrantium, CIM, yaani Chama cha Kimataifa cha Watumishi Altareni, kinachoongozwa na Askofu Ladislav Nemet.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Familia ni mahali pa kwanza kabisa pa kuwafunda watoto misinngi ya imani, maadili, nidhamu na utu wema. Wazazi wanapaswa kuwaangalia watoto wao kama zawadi kutoka kwa Mungu na kuwaheshimu kama binadamu, walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Wawafundishe kushika Amri za Mungu zinazomwilishwa katika upendo kwa Mungu na jirani. Wazazi wawe ni mashuhuda na vyombo vya: utu wema, heshima, uaminifu, msamaha, upendo na mshikamano wa dhati. Nyumbani pawe ni mahali ambapo watoto wanafundwa fadhila njema, ili waweze kukua na kukomaa: kiakili, kiimani, kimaadili na kiutu!

Mama Kanisa anaendelea kuwekeza katika malezi, makuzi na majiundo ya watoto, ambao kimsingi ni matumaini ya Kanisa na Jamii ya leo na kesho iliyo bora zaidi. Kuanzia tarehe 30 Julai 2018 hadi tarehe 3 Agosti 2018, Mji wa Roma umefunikwa na watumishi wa Altareni zaidi ya sabini elfu, kutoka sehemu mbali mbali za dunia, walioitikia mwaliko wa “Associazione Internationalis Ministrantium", CIM, yaani Chama cha Kimataifa cha Watumishi Altareni, kinachoongozwa na Askofu Ladislav Nemet. Watumishi wa Altareni kutoka Ujerumaini, wanaongoza kuwa kuwa na idadi ya vijana wengi zaidi.

Hija ya Watumishi wa Altareni kwa mwaka huu inaongozwa na kauli mbiu “Utafute amani ukaifuatie". Hiki ni kilio, furaha na shukrani ya maskini mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa huruma, wema na upendo mkuu aliomtendea na kwamba, anaona wajibu wa kushirikishana furaha na jirani zake. Vijana hawa kutoka sehemu mbali mbali za dunia, wanataka kujiaminisha tena kwa Kristo Yesu na Kanisa lake kwamba, wanataka kumtumikia bila ya kujibakiza, huku wakichuchumilia amani na utulivu. Huu ni muda wa hija kuzunguka maeneo ya kihistoria, kipindi cha sala na tafakari pamoja na vijana kufurahia maisha ya ujana wao kwa kukutana na vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia kama njia ya ujenzi wa madaraja na utamaduni wa watu kukutana.

Hija ya vijana hawa vijana siku ya Jumanne, jioni tarehe 31 Julai 2018 inapambwa kwa namna ya pekee, kwa uwepo na ushiriki wa Baba Mtakatifu Francisko, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Tukio hili litatanguliwa na shuhuda, muziki na tafakari. Mtakatifu Tarcisio, kijana aliueuwawa kikatili, wakati akiwapelekea Ekaristi Takatifu wagonjwa waliokuwa wamefungwa gerezani ndiye msimamizi wao.

Sikiliza kwa raha zako mwenyewe!

 

30 July 2018, 15:04