Tafuta

Misa ya Papa Francisko Jumapili ya Tano ya Pasaka ameombea umoja wa Ulaya ukue na udugu katika utofauti. Misa ya Papa Francisko Jumapili ya Tano ya Pasaka ameombea umoja wa Ulaya ukue na udugu katika utofauti. 

Papa Francisko:umoja na udugu ukue na kusali ni mapambano na Mungu!

Katika Misa ya Papa Francisko Jumapili asubuhi katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican,amekumbuka matukio mawili ya karibuni:Sikukuu ya Ulaya na kumbu kumbu ya mwisho wa vita ya Pili ya Dunia katika bara la kizamani huku akiombea Ulaya iweze kukua katika utofauti wake.Katika mahubiri amesisitiza kuwa sala ni kama ufunguo wa kwenda kwa Bwana.Ni lazima kuwa na ujasiri wa kusali na kuamini nguvu ya sala.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumapili tarehe 10 Mei 2020  Papa Francisko ameongoza Ibada ya Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican, ikiwa ni Dominika ya V ya Pasaka. Wakati wa utangulizi wake, mawazo yake  kwa mara nyingine tena yametazama bara la Ulaya na kusema: “Siku mbili zilizopita kumekuwapo na kumbu kumbu mbili:kwanza Miaka 70 tangu Tamko la Robert Schuman na ukawa ndiyo mwanzo wa Umoja wa Ulaya na hata Kumbu kumbu la mwisho wa vita. Leo hii tuombe Bwana kwa ajili ya Ulaya hii,  ili umoja huu ukue katika umoja wa kidugu ambao unafanya kukua watu wote katika umoja wa utofauti”. Wakati wa kuanza mahuhubiri yake Papa Francisko yamejikita katika sala, huku  akitafakari Injili ya siku (Yh 14, 1-12) ambapo Yesu anawambia mitume wake kuwa kila amwaminiye, kazi azifanyazo yeye,  atafanya kuwa kubwa zaidi,  kwa kuwa yeye anakwenda kwa Baba. Yesu anasema “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.”

Tamko rasmi la kwenda kwa Baba

Papa Francisko ameongeza kusema kuwa tunaweza  kuona kwamba sehemu hii ya Injili ya Yohane ni tamko la kwenda kwa Baba. Baba daima amekuwapo katika maisha ya Yesu na Yesu alikuwa akisema kuwa Baba anatutunza kwa kuwa ni viumbe vyake. Wakati mitume waliomba awafundishe namna ya kusali, Yesu aliwafandisha sala ya “Baba Yetu.” Yesu daima anakwenda kwa Baba kwa maana hiyo  sehemu hiyo ina nguvu sana kwa sababu ni kama vile inafungua mlango wa nguvu ya sala, kwa maana yeye anasema “Mimi niko na Baba: niombeni nami nitafanya kila kitu”Lakini kwa nini Baba anafanya hivyo? Imani hii katika Bwana ni uwezo wa kufanya kila kitu. Ujasiri huo wa kusali ndiyo ujasiri  sawa sawa na wa  kuhubiri unaohitajika.

Papa Francisko katika kusisitiza hilo amekumbusha ujasiri wa Ibrahimu aliyekuwa anapambana, alikuwa na ujasiri wa kupambana katika sala, kwa maana amebainisha kuwa  kusali ni mapambano na Mungu. Vile vile ni kama ujasiri wa sala ya Musa ambaye alidiriki hata kusema hapana kwa Bwana. Kusali kwa ujasiri kidogo ni kama kukosa heshima Papa amesema. Kusali ni kwenda na Yesu kwa Baba ambaye anatatupatia kila kitu.

Manung'uniko ya wakristo wa mwanzo ni kama mwendelezo wa tabia

Papa Francisko akitafakari somo la Kwanza kutoka Matendo ya Mitume mahali ambapo wanaelezea juu ya migogoro ya nyakati za mwanzo wa Kanisa, kwa sababu wakristo waliokuwa asili ya Kigiriki walikuwa na manung’uniko na hivyo ameongeza Papa kuwa  “tayari katika kipindi hicho kulikuwa na manung’uniko kama hayo. Hii inaonesha kuwa ni tabia ya Kanisa”… “hawa walikuwa wanang’uniko kwa sababu ya wajane na watoto yatima wao hawakuwa na ulinzi mzuri; mitume hawakuwa na muda. Ndipo Petro kwa kuangazwa na Roho Mtakatifu, akavumbua suala la ushemasi. Watu wenye imani ili waweze kujikita katika huduma kwa namna ya kwamba, wale watu waliokuwa na sababu ya kulalamika waweze kuhudumiwa katika mahitaji yao. Petro alichukua uamuzi huo ili mitume wajikite katika sala na kutangaza Neno, Papa amefafanua.

Kazi ya Askofu kusali na kuhubiri

Hii ndiyo kazi ya Askofu kusali na kuhubiri. Kwa nguvu hizo ambazo zimesikika katika Injili. Askofu ndiye wa kwanza kwenda kwa Baba kwa imani aliyopewa na Yesu na kwa ujasiri wa sala katika kupambania watu wake. Aidha Papa amekumbuka kuhani mmoja, paroko mwema alipokuwa kikutana na askofu alikuwa anamuuliza swali lile lile kuwa  Mhashamu mara ngapi unasali kila siku? Askofu alikuwa kimjibu kwamba anasali daima. “ Hii ndiyo kazi ya kwanza ya kusali kwa sababu sala ni kiongozi mkuu wa jumuiya, kuomba kwa Baba ili alinde watu wake”. Sala ya Askofu ndiyo kazi ya kwanza kusali. Na watu wakiona askofu anasali na wao wanajifunza kusali. Kwani Roho Mtakatifu anatufundisha kuwa Mungu anafanya hivyo. Sisi tufanye angalu kidogo lakini ni yeye anayefanya mambo  ya Kanisa na kusali ni kupeleka mbele Kanisa, Papa anashuri. Na ndiyo kazi ya kwanza ambayo maaskofu wanapaswa kupeleka mbele kwa sala.

Neno la Petro: mashemasi wafanye yote maaskofu wasali na kutangaza Neno

Neno lile la Petro ni la kinabii anasema Papa kuwa “mashemasi wafanye yote hayo na watu waweze kutunzwa na kulindwa na kusuluhisha matatizo na mahitaji yao. Lakini sisi maaskofu, sala na kutangaza Neno”. Vile vile Papa amesema “ni huzuni kuona maaskofu wema, lakini wanao jishughulisha na mambo mengi ya kiuchumi au ya hapa na pale … Lakini sala ndiyo yenye nafasi ya kwanza, mambo mengine yanafuata baadaye. Ikiwa mambo mengi yanaondoa nafasi ya sala, kuna jambo ambalo halifanyi kazi. Na sala ndiyo yenye nguvu. Yesu alisema “mimi ninakwenda kwa Baba, lolote mtakalo omba kwa jina la Baba yangu mimi nitafanya ili Baba yangu aweze kutukuzwa”.

Kwa kuhitimisha:Kanisa linaendelea mbele kwa sala

Kwa huhitimisha Papa anasema na ndiyo hivyo Kanisa linakwenda mbele, kwa sala, kwa ujasiri wa sala kwa sababu Kanisa bila hilo hakuna kwenda kwa Baba na haliwezi kuishi. Papa Francisko amehitimisha maadhimisho yake kwa kuabudu na baraka ya ekaristi. Kabla ya kuacha kikanisa  hicho ameshiriki wimbo wa mwisho wa Malkia wa Mbingu kwa lugha ya kilatino: Regína caeli laetáre, allelúia.

Quia quem merúisti portáre, allelúia.
Resurréxit, sicut dixit, allelúia.
Ora pro nobis Deum, allelúia.

Malkia wa Mbingu: Malkia wa mbingu, furahi, aleluya. Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya. Amefufuka alivyosema, Aleluya. Utuombee kwa Mungu, Aleluya. Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya. Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya

10 May 2020, 10:55
Soma yote >