Tafuta

Vatican News
2020-02-05 Kwa wakristo wanatambua kuwa kipindi cha shida siyo kipindi cha kufanya mabadiliko ni kutulia na kuwa na imani. 2020-02-05 Kwa wakristo wanatambua kuwa kipindi cha shida siyo kipindi cha kufanya mabadiliko ni kutulia na kuwa na imani. 

Papa Francisko:wakati wa shida viongozi waungane kwa ajili ya wema wa watu!

Katika misa ya Papa Francisko kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,Vatican,Mei 2,amesali kwa ajili ya watawala wa nchi wenye majukumu ya kutunza watu.Katika mahubiri amesisitiza kuwa katika kipindi cha shida kuna haja ya kuwa imara na uvumilivu na uthabiti wa imani.Siyo wakati wa kufanya mabadiliko.Bwana atutumie Roho Mtakatifu ili kuwa waaminifu na kutupatia nguvu ya kutouza imani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko, Jumamosi, tarehe 2 Mei 2020, katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican ameongoza Misa Takatifu katika wiki ya tatu ya kipindi cha Pasaka. Katika utangulizi wake Papa mawazo yake yamewageukia watawala: Tusali leo hii kwa wajili ya watala ambao wanawajibu wa kutunza watu wao katika kipindi cha shida yaani  wakuu wa nchi, Marais wa nchi, wanasheria, mameya, wakuu wa mikoa… na ili Bwana aweze kuwasaidia na kuwapa nguvu kwa sababu kazi yao isiyo rahisi. Na kwamba Inapotokea tofauti kati yao, waweze kutambua kuwa katika kipindi cha shida ni lazima waungane sana kwa ajili ya wema wa watu na kwa sababu, umoja una nguvu zaidi kuliko migongano”. Aidha Papa Francisko amesema, @leo hii Jumamosi tarehe 2 Mei, wanaungana na sisi makundi 300 ya sala ambayo yanaitwa “madrugadores”, kwa kisipanyola, maana yake  waamukao asubuhi na mpama. Wao huamka asubuhi sana ili kusali na wanaamka kweli mapema kwa sababu ya kusali. Wao wanaungana pamoja nasi leo hii katika muda huu”.

Akianza mahubiri yake Papa Francisko ametafakari somo la siku kuanzia na sehemu ya Matendo ya Mitume (Mdo 9, 31-42) inayoelezea juu ya Jumuiya ya kwanza ya wakristo ambao walikuwa wakiimarika na kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu na idadi yao kuzidi kuongezeka. Kwa njia hiyo Papa Francisko amekumbusha matukio mawili yanayogusa Petro: kuponyesha kiwete huko Lidda  na ufufuko wa mfuasi aliyekuwa anaitwa Tabità. Kanisa linakua wakati wa kutiwa nguvu lakini hata kuwa na wakati mwingine mgumu wa mateso, katika kipindi cha mgogoro ambacho kinaleta matatizo makubwa kwa waamini. Kama isemavyo Injili ya siku  (Yh6, 60-69), mahali ambapo baada ya mahubiri kuhusu mkate kushuka toka mbinguni, mwili na damu ya Kristo ambayo inatoa maisha ya milele, wafuasi wengi walimuacha Yesu wakisema maneno yake ni magumu", anathibitisha Papa.

Hata hivyo Yesu alikuwa anatambua hayo kuwa wafuasi walikuwa wanalalamika na ndiyo maana katika shida hiyo anakumbusha Yesu kuwa hakuna yoyote anaweza kwenda kwake  isipokuwa anayetuvutwa na Baba yake. Lakini wengine walikwenda mbali, kwa sababu walisikia maneno ya kiajabu. Kama ilivyokuwa mitume wa Emau, ambao walikuwa wakikimbia, au walinzi wa kaburi waliona ukweli lakini wakapendelea kuuza siri yao. Papa Francisko amesisitiza kuwa wakati wa shida ni wakati wa kufanya uchaguzi na maamuzi muhimu. Wote tuna kipindi cha shida, katika familia, kijamii, katika kazi na janga, ni wakati wa kipeo cha kijamii kwa ujumla.

Swali, je ni namna gani ya kufanya? Wafuasi wengi wa Yesu walirudi nyuma. Lakini Yesu akawambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro  kwa mara ya pili akakiri na kumjibu Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu”. Papa ameongeza, Petro anakiri kwa niaba ya thenashara . Hili litusaidie kuishi wakati wa shida. Papa Francisko aidha ametumia msemo wa kiargentina usemao “ usibadili farasi katikati ya mto. Na kwa maana hiyo ameongeza kushauri kuwa katika kipindi cha shida pasifanyike mabadiliko, mtu lazima awe thabiti katika imani.

Ni wakati wa uongofu, mabadiliko kadhaa kwa ajili ya wema. Vipo vipindi vya  amani na shida amesema Papa, na kama Wakristo lazima tujifunze kusimamia na kuwa imara katika nyakati zote mbili”. Shida hiyo ni kama kupitia katika moto ili kugeuka  kuwa na nguvu. Bwana atutumie Roho ili kujua jinsi ya kupinga majaribu wakati wa shida na kuwa waaminifu na tumaini la kuishi wakati wa amani. Tufikirie shida binafsi, za familia na kijamii, na hivyo Bwana atupatie nguvu katika wakati wa shida na siyo kuuza imani, amehitimisha Papa Francisko.

02 May 2020, 09:03
Soma yote >