Tafuta

Vatican News
Misa ya Papa Francisko  katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican tarehe 14 Mei 2020 Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican tarehe 14 Mei 2020 

Papa Francisko:tuungane ndugu wote kusali kwa Mungu asitishe janga!

Katika Misa ya asubuhi kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican,Papa Francisko amekumbuka Siku ya Maombi iliyoandaliwa na Kamati Kuu kwa ajili ya Udugu wa Kibinadamu ili kuomba Bwana asimamishe janga la covid-19.Katika mahubri amekumbusha kuwa,licha ya uwepo wa janga la sasa,lakini bado kuna majanga mengine yanayosababisha vufo vya milioni ya watu kama vile janga la njaa,la vita na watoto ambao hawawezi kwenda shule.Amewaalika wote kuomba Mungu na atubariki na kutuhurumia.

Papa Francisko Alhamisi tarehe 14 Mei 2020 amedhimisha Ibada ya Misa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, Vatican katika siku ambayo Kanisa linaadhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Matia Mtume. Katika utangulizi wake amekumbuka siku hii iliyotolewa kwa ajili ya maombi, kufunga, toba na kufanya matendo ya hisani iliyoandaliwa na Tume Kuu ya Udugu wa Kibinadamu na kuwatia moyo wote waungane  kama ndugu ili kuomba Mungu wokovu dhidi ya ubaya huu. Katika maneno yake Papa amesema: Tume Kuu kwa ajili ya Udugu wa Kibindamu, ilitangaza leo hii kuwa Siku ya sala, kufunga na kuomba Mungu huruma na rehema katika kipindi hiki cha kutisha cha janga. Sisi sote ni ndugu. kama  Mtakatifu Francis wa Assisi alivyokuwa akisema “sisi sote ni ndugu”. Na kwa maana hiyo wanaume na wanawake wa kila dhehebu ya kidini  leo hii tuungane katika sala na katika kufunga kwa ajili ya kuomba neema ya kuponyeshwa na janga hili.

Nabii Yona aliyetumwa na Mungu

Katika mahubiri Papa Francisko ametafakari juu ya somo la kwanza lililosomwa kutoka kitabu cha Yona, Nabii aliyetumwa kuwaalika watu wa mji wa Ninawi waongoke ili wasije pata pigo la uharibifu wa mji wao. Mji wa Ninawi uliongoka na  ukaokolewa na janga, na labda amebainisha Papa “lilikuwa ni janga la kimaadili”. Leo hii amesisitiza Papa kuwa sisi sote, kaka na dada wa kila tamaduni ya kidini  tuombe. Siku ya sala na kufunga, siku ya toba, iliyotishwa na Tume Kuu ya Udugu wa Kibinadamu. Kila mmoja asali, Jumuiya zisali kwa Mungu, ndugu wote,  kwa kuungana kidugu unaotuunganisha katika kipindi hiki cha uchungu na balaa. Papa aidha amesema “ hakuna aliyekuwa anasubiri balaa hili limekuja bila sisi kutegemea, lakini sasa lipo. Watu wengi wanakufa. Na watu wengi wanakufa wakiwa peke yao, watu wengi wanakufa bila hata kufanya lolote. Lakini Papa amesema: “Mara nyingi inawezeka kuijiwa na wazo kuwa“ kwangu mimi hailinigusi, ninamshukuru Mungu nimeokoka”. Lakini fikiria wengine! Fikiria balaa na matokeo yake ya kiuchumi, matokeo kuhusu elimu na yale ambayo yatakuja baadaye. “Kwa njia hiyo Papa amesisitiza leo hii kaka na dada, wa kila dhehebu la dini tusali kwa Mungu”.

Kila mmoja asali ajuavyo kwa mujibu wa tamaduni yake

Aidha kwa kusisitiza zaidi amesema, mwingine anaweza kusema, “Lakini huu ni uhusiano wa kidini na hauwezi kufanywa”.  Je ni kwanini huwezi fanya, kusali kwa Baba wa wote? Papa anauliza na kusema, kila mmoja asali anavyojua, na kama iwezekanavyo kwa mujibu wa utamaduni wake. “Sisi hatusali dhidi ya kila mmoja, utumaduni huu wa kidini dhidi ya mwingine hapana! Sisi sote tunaunganika kama wanadamu, tukiwa ndugu, tunamwomba Mungu, kulingana na tamaduni zetu, kulingana na mila zetu, kulingana na imani zetu, lakini tukiwa ndugu na tunaomba kwa Mungu na hii   ndiyo muhimu”. Kwa kufunga, tuombe msamaha kwa Mungu kwa ajili ya dhambi zetu, kwa sababu Bwana atuhurumie, ili Bwana atusamehe, na ili Bwana asimamishe janga hili”. Papa Francisko ameongeza kusema “ leo hii ni siku ya Udugu, kwa kutazama Baba mmoja, ndugu na ubaba. Siku ya sala”. Janga hili limekuja kama gharika kuu, limekuja kwa pigo moja, na sasa ndipo tunazinduka kidogo, Papa amebanisha. Lakini kuna hata majanga mengine ambayo yanafanya watu kufa na sisi bila kutambua hilo, na kutazama sehemu nyingine. Sisi kidogo tunapoteza fahamu mbele ya mikasa  ambayo inajitokeza hivi sasa ulimwenguni”.

Twakwimu za vifo kuhusu njaa ulimwenguni

Papa Francisko ametaja takwimu rasmi ambazo hazizungumzi juu ya janga la virusi vya corona, bali jingine na kusema:“Katika miezi ya mwanzo wa mwaka huu ni vifo vya watu milioni 3,700 kwa sababu ya njaa. Kuna janga la njaa. Katika miezi minne  ni karibu watu milioni 4. Sala ya siku ya leo ambayo ni kuomba Bwana asimamishe janga, itufanye tufikirie majanga mengine ya ulimwengu”. Papa anaongeza, “yapo mengi! Janga la vita, la njaa na mengine mengi. Lakini la muhimu ni kwamba leo hii na shukrani kwa ujasiri walioupata Tume Kuu hii kwa ajili ya Udugu wa kibindamu na kufanya siku ya toba kwa kufungwa na hata kwa ajili ya upendo ili kutoa msaada kwa ajili ya wengine. Hili ni muhimu. Katika kitabu cha Yona tulichosikia kuwa Bwana alipowatazama watu walivyokuwa wamefanya, yaani wakaongoka, Bwana alisimamisha na kuwanusuru kwa kile alichokuwa anataka kufanya”,Papa amesema.

Bwana asimamisha balaa hili

Sala ya Papa Francisko ni kwamba “ Bwana aweze kusimamisha balaa hili, asimamishe janga hili. Mungu aturehemu na azuie magonjwa mengine mabaya: ile ya njaa, ile ya vita, ile ya watoto wasio na elimu. Na tuombe kama ndugu, wote kwa pamoja. Mungu atubariki wote na utuhurumie”. Mara baada ya madhimisho ya misa imefuata kuabudu na baraka ya Ekaristi. Papa Francisko kabla ya kuondoka altareni amemshukuru Tommaso Pallottino, fundi mitambo ya matangazo ya moja kwa moja ambaye leo hii, ilikuwa ni siku yake ya mwisho kazini kabla ya kustaafu:"Bwana aweze kumbariki na kumsindikiza katika hatua mpya ya maisha", ameomba Papa. Wimbo wa kipindi cha Pasaka wa Malkia wa Mbingu kwa lugha ya kilatino umeimbwa wakati Papa amesimama mbele ya picha ya Mama Maria.

Regína caeli laetáre, allelúia.

Quia quem merúisti portáre, allelúia.

Resurréxit, sicut dixit, allelúia.

Ora pro nobis Deum, allelúia.

14 May 2020, 09:44
Soma yote >