Tafuta

Misa ya Papa Francisko tarehe 13 Mei 2020 amekazia muungano wa dhati katika Kristo. Misa ya Papa Francisko tarehe 13 Mei 2020 amekazia muungano wa dhati katika Kristo.  (Vatican Media)

Papa amesali kwa ajili ya wanafunzi.Maisha ya kweli ya kikristo ni katika kubaki ndani ya Yesu!

Katika Misa ya Papa Francisko kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,amesali kwa Bwana ili awajalie ujasiri wanafunzi na walimu wa kwenda mbele katika janga hili.Mahubiri yake amesisitiza juu ya ujasiri wa maisha ya kikristo kwamba ni wa kubaki ndani yake na Yeye kuwa ndani mwetu maana bila Yesu hatuwezi kufanya lolote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumatano tarehe 13 Mei 2020 Papa Francisko ameadhimisha Ibada ya Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican ikiwa ni wiki ya tano ya Pasaka na ambayo Mama Kanisa anaadhimsha Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Fatima. Katika utangulizi wake mawazo yamewaendea wanafunzi na walimu na kusema “Tusali leo hii kwa ajili ya wanafunzi, vijana ambao wanasoma na walimu ambao lazima watafute mitindo mipya ya kuweza kwenda mbele katika mafundisho. Bwana awasaidie katika safari hiyo na kuwajalia ujasiri na hata mafanikio mema”.

Katika mahuburi, Papa ametafakari Injili ya siku kutoka Yohane 15,1-8 mahali ambapo Yesu anawambia mitume wake “Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima.  Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa.  Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote.  Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote.  Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.  Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu".

Matawi na matunda vinategemeana

Papa Francisko amesema maisha ya kikristo ni kubaki katika Yesu. Bwana anatumia picha ya mzabibu. Kubaki siyo suala la kubaki bila kazi au kulala katika Bwana. Ni tendo la kubaki hata kwa upamoja. Hata Yeye anabaki ndani mwetu, ni fumbo la maisha, ni fumbo zuri sana. Matawi bila uhai hayawezi kufanya lolote kwa maana yanahitaji kiini ili kukua na kutoa matunda, lakini hata uhai unahitaji matawi. Ni mahitaji yanayotegemeana ili kutoa matunda. Papa Francisko amebanisha kuwa “Haya ndiyo maisha ya kikristo,  ni kutimiza amri, yaani katika kuishi kwa heri na kutumiza kazi ya huruma, japokuwa kile cha muhimu ni kutegemeana. Bila Yesu hatuwezi kufanya lolote. Ameongeza kusema Papa Utafikiri kwamba hata bila ya sisi, na kama  kama mnaniruhusu kusema Bwana huyo, Yesu hawezi kufanya lolote.  Kwa maana ni ule undani wenye matunda”.

Mahitaji ya Maisha ni kuzaa matunda

Mahitaji ya maisha ni kuzaa matunda. Mahitaji ya Yesu ni ushuhuda wetu. Na mahitaji ya Yesu ni kwamba sisi tuoneshe ushuhuda wa jina lake, kwa sababu ndiyo unakuza Kanisa kwa ushuhuda. Na fumbo la “kubaki” kwa kutegemeana”.  Kwa maana hiyo Papa ameshauri kuwa “Itakuwa ni vema leo kufikiria hili. Sisi kubaki ndani mwa Yesu na Yesu kubaki ndani mwetu”.

Tunayo zawadi ya bure ili tuwe na wokovu

Ili sisi tuweze kuwa na wokovu, Papa anasema tunayo zawadi ya bure na Yesu aweze kubaki ndani mwetu ili  kutupatia nguvu za kushuhudia ambapo Kanisa linakua. Tunatakiwa kuwa na uhusiano wa ndani, na kufanya ibada ya kina, bila maneno.  Aidha amebainisha kuwa “Siyo tu kwa watu wa ibada ya kina  bali ni kwa ajili yetu sisi pia”.  “Bwana nipatie nguvu na nitafanya kile unachoniamuru”. Papa Francisko ameshauri kuwa na mazungumzo ya kina na Bwana. Na kwa kuhitimisha amesistiza kuwa ni uhusiano wa kina, ibada ya kina, bila maneno. Siyo tu kwa wale wenye ibada ya kina bali ni kwa ajili ya sisi sote. Sala ya Papa: “Bwana atusaidie kutambua hili na kuishi ibada hii ya kina ya kubaki”. Kwa kuhitimisha ibada ya Misa imefuata kuabudu na baraka ya Ekaristi. Kabla ya kuondoka katika kikanisa ameshiriki wimbo wa mwisho wa Bikira Maria aliye watokea watoto watatu huko Cova ya Ria, Fatima nchini Ureno.

“Salamu, Salamu, Salamu Maria”....

 

13 May 2020, 09:03
Soma yote >