Tafuta

Vatican News
Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican. Misa ya Papa Francisko katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican.  (Vatican Media)

Papa amesali ili upendo ukue katika familia.Penye ugumu hakuna roho wa Mungu!

Katika Misa kwenye kikanisa cha Mtakatifu Marta,Papa amesali kwa ajili ya familia ikiwa ni Siku ya kimataifa Duniani.Katika mahubiri yake ametazama duku duku za wakristo wa kwanza na kusema daima katika ukristo kumekuwa na kipindi cha amani,kipindi cha mateso,hata nyakati za tahabu.Penye ugumu hakuna Roho wa Mungu.Kifo na Ufufuko wa Kristo ni zawadi za bure

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko ameadhimisha Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta, Ijumaa tarehe 15 Mei 2020 katika wiki ya tano ya Pasaka. Katika utangulizi wake mawazo yake yamewaendea Familia: Leo hii ni siku ya Kimataifa ya familia: Tuombee familia kwa sababu iweze kukua kwa Roho ya Bwana, Roho ya upendo, ya heshima na uhuru. Katika mahubiri Papa Francisko ametafakari sehemu ya Matendo ya Mitume ( Mdo 5, 22-31) mahali ambapo Paulo na Barnaba walitumwa kwenda wa wapagani waliokuwa wameongoka huko Antiokia, lakini wakiwa na duku duku na kupotoshwa roho zao kutokana na  watu waliokuwa hawajatumwa wajibu huo. Mitume walipeleka barua ambayo ilikuwa inawatia moyo na kufurahi kwa wafuasi wapya hata kwa kuwaeleza wao kwamba wasitishwe mzigo ya bure, bali kujiepusha na vitu vilivyotolewa na sadaka, kwa sanamu na damu na nyama zilizosongolewa na uasherati kama walivyokuwa wanataka baadhi ya wafarisayo waliokuwa wamegeuka wakristo.

Papa Francisko akiendelea na mahaubiri amesema kwamba katika kitabu cha Matendo ya mitume, Kanisa lilikuwa linakua kwa amani, Roho ya Bwana ilikuwa ikienea, kulikuwa hata  na wakati wa mateso… kwa maana hiyo kulikuwa na  kipindi cha amani, kipindi cha mateso na hata nyakati za tahabu. Na ndiyo maana ya somo la kwamza la siku linabainisha juu ya dukuduku hiyo. Je ilikuwa imetokea nini? Wakati walikuwa tayari wameamini katika Kristo na kupokea Ubatizo, kutoka katika upagani na kuingia katika ukristo bila kufanya mchakato wa hatua yoyote, japokuwa  watu wale  walikuwa wakibishi kwamba wasingeweza kufanya hivyo, mpaka kwanza kupitia hatua kwa uyahudi na baadaye wakristo. Hii ilikuwa inaweka mjadala wa ufufuko wa Kristo. Walikuwa ni watu wa mitindo na wagumu.

“Watu hawa ambao walikuwa na itikadi, badala ya maagizo, walikuwa wamepunguza sheria, na kuziweka katika itikadi yaani  kuifanya dini ya maagizo, na kwa hilo waliondoa uhuru wa Roho. Na wafuasi wao walikuwa watu wanyonge ambao hawakujua furaha ya Injili, bali wajua njia ya ugumu tu. Ukamilifu wa barabara ya kumfuata Yesu ulikuwa ni mgumu. Madaktari hawa walidharau dhamiri ya waamini, waliwafanya kuwa wagumu au waliondoka. Papa amebainisha. “Ugumu siyo Roho nzuri. Hili siyo jambo la kizamani amesisitiza Papa. Katika historia imerudiwa. Hata katika nyakati zetu, tumeona mashirika kadhaa ya kitume, yote ni magumu, yote ni sawa. Na baadaye tukajua kuwa ufisadi iliokuwa ndani humo na hata kwa waanzilishi. Mahali ambapo kuna ugumu hakuna Roho wa Mungu. Kifo cha Kristo na Ufufuko ni wa  bure”, Papa Francisko amehimiza.

Aidha Papa Francisko akisisitiza zaidi amesema “Mahali palipo na ugumu hakuna roho ya Mungu kwa sababu Roho ya Mungu ni uhuru. Lakini kuhesabiwa haki ni bure. Kifo na ufufuko wa Kristo ni bure. Haulipwi,  wala haununuliwi: ni zawadi. Roho ya ugumu daima inapelekea dukuduku la kujiuliza je hili nimefanya vizuri hau hapana? Kinyume chake Roho ya huru wa Kiinjili inapelekea furaha kwa maana ndicho alifanya Yesu kutokana na Ufufuko wake, yaani furaha”. Papa Francisko amesema “Uhusiano na Mungu, uhusiano na Yesu haukufanyi useme: 'Mimi nina fanya hiki na Wewe unafanya lile', siyo uhusiano wa kibiashara. Uhusiano wa Yesu na wafuasi wake ni wa bure: “Ninyi ni marafiki zangu. Siwaiti watumwa ninawaita marafiki, kwa maana hamkunichagua mimi bali nimewachagua mimi”, hiyo ndiyo zawadi ya bure, Papa Francisko amesisitiza.

Kwa kuhitimisha ameomba Bwana atusaidie kung’amua matunda ya bure ya kiinjili kutoka katika matunda ya ugumu ambayo siyo ya kiinjili, na atuokoe  kwa kila aina ya dukuduku zinazoingilia imani, kwa wale ambao wanaweka imani chini ya maagizo ya sheria, maagizo ambayo hayana maana na ambayo siyo Amri. Atukoe na roho ya ugumu ambao unaondoa uhuru. Mara baada ya Misa imefuata ibada ya kuabudu na baadaye Papa Francisko abariki kwa Ekaristi. Mwisho wimbo wa Malkia wa Mbingu umeimbwa: Regína caeli laetáre, allelúia. Quia quem merúisti portáre, allelúia. Resurréxit, sicut dixit, allelúia. Ora pro nobis Deum, allelúia.

 

10 May 2020, 10:20
Soma yote >