Tafuta

Vatican News
2020-04-27 Papa Francisko anatoa mwaliko wa kurudia kukumbuka wito wa kwanza na kurudi Galilaya mahali ambapo Yesu alielekeza wanawake baada ya Ufufuko. 2020-04-27 Papa Francisko anatoa mwaliko wa kurudia kukumbuka wito wa kwanza na kurudi Galilaya mahali ambapo Yesu alielekeza wanawake baada ya Ufufuko. 

Papa Francisko awaombea wasanii:Bwana utujalie neema ya ubunifu!

Katika misa ya Jumatatu tarehe 27 Aprili 2020,Papa Francisko amekumbuka wasanii katika njia ya uzoefu na ubunifu ambao unaweza kuwasadia katika kipindi hiki kigumu janga la virusi vya corona.Katika mahubiri amewaalika kuomba neema ya kurudia wito wa kwanza mahali ambapo Yesu alitutazama kwa upendo na kutuita tumfuate.Amekumbusha neno Galilaya mahali ambapo Yesu alianzia na kuelekeza mara baada ya ufufuko wake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko Jumatatu tarehe 27 Aprili 2020 katika kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican ameadhimisha Misa takatifu na katika utangulizi wa misa hiyo, mawazo yake yamewaendea wasanii wote: “ Tusali leo hii kwa ajili ya wasanii wenye uwezo wa ubunifu mkubwa sana na kwa njia ya uzuri huo wanatuelekeza njia ya kufuata. Na Bwana aweze kutujalia wote neema ya ubunifu katika wakati huu”. Akianza mahubiri yake Papa Francisko, kama kawaida yake anakumbuka kwa ujumla hali halisi kwa namna ya pekee ya mgogoro mkubwa uliopo wa janga na baadaye amejikita kutafakari katika Injili ya siku.

Sehemu ya Injili ya siku inaonyesha sura ya hali halisi mara baada ya miujiza ya mikate na samaki. Yesu alikwenda baadaye kusali peke yake na mitume wake wakaondoka kwa chombo chao, naye Yesu baadaye akawafuata wao akiwa anatembea juu ya maji. Lakini watu waliona mtumbwi ukiwa kandoni mwa bahari na kufikiria kuwa Yesu hakuondoka na baadaye wakaanza kumtafuta na kumkuta huko Kapernaum. Papa Francisko amesimulia kuwa “Watu waliokuwa wamemsikiliza Yesu kutwa nzima na baadaye wakapata neema ya wingi wa mikate na waliona uwezo wa Yesu na hivyo walitaka kumfanya awe mfalme”.

Papa Francisko akiendelea amesema, kwa namna hiyo “kwanza walikuwa wanakwenda kwa Yesu ili kusikiliza neno na hata kuomba neema ya uponyweshwaji wa wagonjwa. Lakini walipomwona Yesu anawapa hata chakula, jambo ambalo hawakutegemea, walifikiria: huyo ndiye angekuwa madarakani na angekuwa na uwezo wa kuwakomboa dhidi ya nguvu za kirumi na ili kupeleka mbele Nchi na kwa shauku kubwa walitaka kumchagua awe ndiye mfalme”. Kwa hakika yalikuwa yamejitokeza mabadiliko ya roho ambayo yaliwafanya wasahahu shauku kwamba neno la Yesu lilikuwa limezaliwa katika mioyo yao. Hawa walikuwa wakimtafuta Yesu na wakamkuta Kapernaum na kumuuliza amefika saa ngapi pale. Papa Francisko akiendelea  amesema kuwa, lakini Yesu aliwafanya warudi katika hisia za mwanzo na kuwakaripia kwa kusititiza kuwa wanamtafuta kwa sababu walikula na kusaza na wala siyo kwa sababu ya ishara walizoziona.

Mbele ya unyenyekevu wao, Papa anaongeza, Yesu anawaalika kufanya lolote, lakini si kwa ajili ya chakula ambacho hakidumu bali kutafuta kile kinachodumu milele. Aidha  Papa ameongeza kusema.  Yesu anawakosoa watu hao juu ya tabia zao, umati huo kwa sababu katikati ya mchakato wa safari yao walikuwa wasehamu kumbu kumbu ya faraja ya kwanza ya kiroho na walikuwa wamepoteza njia na kuelekea katika njia ya ya kiulimwengu ambayo siyo ya kiiinjili. Inajitokeza hata kwetu sisi, anaendelea Papa na kwamba katika maisha huanza njia ya kumfuasa Yesu, nyuma ya Yesu na thamani zake za Injili lakini katikati ya njia linakuja wazo jingine ambapo linatufanya twende mbali na kutufananisha na jambo la muda tu, kwa kupenda mali, mambo ya kidunia na tunapoteza kumbukumbu ile ya shauku za kwanza za wito wa Yesu.

 Papa, anabainisha kuwa Bwana, anafanya utambue  daima kurudi katika mkutano wa kwanza, yaani wakati ule alipotutazama na kutufanya ndani mwetu uzaliwe ule utashi wa kumfuata na kwa hali halisi ya kina anafanya hivyo hata baada ya Ufufuko wake,alipowambia wale wanawake waende wakawambie mitume waende Galilaya, mahali ambapo wangemkuta.

Papa amezidi kusisitiza kuwa, Galilaya ni mahali ambapo kulianzia kila kitu na hata sisi sote tunapaswa kurudi pale, katika Galilaya zetu. Kufuatia na hilo, ameomba neema ya kurudi katika wito wetu wa kwanza, wakati wa kwanza kwa maana hapo daima ndipo tutakuwa na kishawishi cha kwenda mbali. Anawaalika waamini kutosahau historia binafsi, wakati ambapo Yesu alinitazama kwa upendo na kuniambia: “hii ndiyo njia yako”. Wakati Yesu alinifanya nitambue ni njia gani ya Injili na siyo njia nyingine kidogo ya kidunia au ya thamani nyingine.

Kati ya mambo ambayo Yesu aliwambia wanawake asubuhi na mapema ya Ufufkoa ni ile ya kwenda “Nendeni kwa wafuasi wangu na wambieni waende huko Galilaya. Hapo wanatanikuta.” Pale palikuwa ni mahali pa kwanza pa mkutano. Kila mmoja anayo Galilaya yake, Papa amesisitiza. Katika maisha inatokea hili ambalo liliwatokea watu hawa wema; inatokea kwamba tunakwenda mbali na tunatafuta thamani nyingine, mambo mengine na kupoteza mambo mapya ya wito wa kwanza.

27 April 2020, 09:53
Soma yote >