Tafuta

Vatican News
2020-04-28 Papa Francisko amesali kwa Bwana ili watu wake wake na busara katika kipindi hiki cha janga. 2020-04-28 Papa Francisko amesali kwa Bwana ili watu wake wake na busara katika kipindi hiki cha janga.  (Vatican Media)

Papa Francisko amesali ili watu wawe na neema ya busara mbele ya janga !

Katika Misa ya Papa Francisko tarehe 28 Aprili 2020 amesali ili watu wa Mungu waweze kutii sheria zilizowekwa kwa ajili ya karantini ili janga lisiweze kulipuka tena.Katika mahubiri yake anawaalika waamini wasiangukie katika maneno meneno ya hukumu ndogo za kila siku ambazo husababisha chochezi za hukumu za uwongo kwa watu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko kama kawaida yake, ameadhimisha misa takatifu katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican Jumanne tarehe 28 Aprili 2020 tukiwa katika wiki ya tatu ya kipindi cha Pasaka. Akianza utangulizi wake, amefikiria juu ya tabia ya watu wa Mungu mbele ya kukabiliana na mwisho wa karantini na kusema: “ katika kipindi hiki ambacho kinaanza kuwa na nafasi za kuweza kutoka nje ya karantini, tusali kwa Bwana ili awapatie watu wake, sisi sote neema ya kuwa na busara na utiii  wa sheria zilizowekwa ili janga lisiweze kurudia tena.

Akianza mahubiri yake Papa Francisko ametafakari juu ya somo la siku kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume (Mdo7,51-8,1), mahali ambapo Mtakatifu Stefano anazungumza kwa ujasiri kwa watu, wazee na waandishi ambao wanamhukumu kwa ushuhuda wa uongo, wanamkamata na kumburuza nje ya mji na kumpiga mawe bila huruma. Papa Francisko amebainisha kuwa hata kwa upande wa Yesu walifanya hivyo hivyo kwa kutafuta kuwaaminisha watu kuwa alikuwa na tuhuma ya kukashifu. Ulikuwa ni unyama kuanzia na ushuhuda wa uongo wa kutaka kufanya haki. Uongo, masengenyo ambayo yalichochea watu ili kumhukumu ndiyo kweli maoni ya tuhuma hizo.

Habari za uwongo, kejeli, ambazo zinawashawishi watu kufanya haki ya kuhukumu, Papa Francisko amesisitiza kuwa ni hukumu mbaya. Ndivyo walivyofanya na Stefano, wakitumia watu ambao walidanganywa. Hivi ndivyo inavyotokea  hata leo na mashuhuda wa uongo, kama wafia dini wa sasa, aidha amekumbuka Asia Bibi, ambaye amekuwa gerezani kwa miaka mingi, alihukumiwa kwa sababu ya tuhuma za maneno ya uongo. Mbele ya maporomoko ya  habari za uwongo zinazounda maoni, wakati mwingine hakuna kinachoweza kufanyika Papa Francisko amesema. Kufuatia hilo aidha amewaza mauaji ya kimbari ya wayahudi na kwamba maoni yaliundwa dhidi ya watu  hao ili kuwaondoa.

Kadhalika Papa Francisko amebainisha kuwa kuna hata hukumu ndogo ndozo zinazofanyika kila siku katika kutafuta kuunda sifa mbaya dhidi ya watu , masengenyo na maoni ya kulaani watu. Ukweli kwa upande,  uko wazi na wazi, ni ushuhuda wa ukweli, wa kile tunachoamini. Tufikirie juu ya lugha zetu: mara nyingi na maoni yetu tunaanza hukumu hizo. Hata katika taasisi zetu za Kikristo tumeona malalamiko mengi ya kila siku ambayo yanatokea kwenye gumzo. Tuombe kwa Bwana atusaidie kuwa wenye haki katika hukumu zetu na kuanza kufuata hukumu hii kubwa inayosababishwa na maneno mengi. Papa Francisko amehitimisha misa yake kwa kuabudu na baraka ya ekaristi Takatifu, akiwaalika hata waamini kufanya Komunio ya tamaa.

 

28 April 2020, 11:05
Soma yote >