Tafuta

Vatican News
16.04.2020 Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta 16.04.2020 Misa ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta  (Vatican Media)

Papa amesali kwa ajili ya wafamasia:asante kwa msaada wa wagonjwa!

Katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican,Papa Francisko ameshukuru wafamasia wote wanaofanya kazi katika kipindi hiki cha janga kuwasaidia watu wagonjwa.Katika mahubiri yake anamedhibitisha kwamba nguvu kubwa tuliyo nayo ya kuhubiri Injili ni furaha ya Bwana,furaha ambayo ni tunda la Roho Mtakatifu.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko ameongoza misa ya asubuhi Alhamisi 16 Aprili 2020 katika kikanisa cha mtakatifu Marta mjini Vatican. Wakati wa utangulizi wake, mawazo yake yamewandelea wafamasia wote na kusema: Siku hizi nimekaripiwa kuwa nimewasahau na kuwashukuru kikundi cha watu ambao wanafanya kazi… Nimeshukuru madaktari, wauguzi, watu wa kujitolea…. Lakini wewe umesahau wafamasia: hata wao wanafanya kazi sana, wao pia wanajitahidi kusaidia wagonjwa ili wapone ugonjwa huo.Tuwaombe pia wao.

Katika mahubiri Papa Francisko ametafakari Injili ya siku kutoka Luka 24, 35-48, Yesu mfufuka aliwatoke mitume wake ambao walikuwa na hofu kubwa kwa sababu ya kufikiri wameona kivuli na anawafungua akili ya kutambua Maandiko Matakatifu. Na kwa sababu ya furaha walishindwa hata kuamini. Kujazwa na furaha Papa amesisitiza ni uzoefu wa hali ya juu wa faraja. Ni utimilifu wa uwepo wa Bwana; ni tunda la Roho Mtakatifu, ni neema. Hata hivyo Papa  ametaja juu ya Wosia wa Kitume wa Papa Paulo VI  “ Evangelii nutiandi” ambao unazungumza juu ya wainjilishaji wenye furaha, na kushauri kuusoma kwa siku. Nguvu kubwa tuliyo nayo ya kuhubiri Injili na kwenda mbele kama mashuhuda wa maisha ni furaha ya Bwana na ambayo ni tunda la Roho Mtakatifu amesema Papa.

Papa Francisko akiendelea na mahubiri yake, amekumbusha jinsi gani huko Yerusalem watu walikuwa na hisia nyingi: hofu, mshangao na wasiwasi. Wakati ule kiwete aliponyeshwa waliwakawiza Petro na Yohane na  watu wote, walikuwa na mshangao mkubwa na kujisahau… Kulikuwa na hali ambayo siyo ya utulivu kwa maana kulitokea jambo ambalo hawakujua ni kitu gani. Bwana alikwenda kwa mitume wake. Wao walikuwa wanajua tayari kuwa amefufuka, hata Petro alikuwa anajua kwa sababu alizungumza naye siku ile asubuhi. Wale waliokuwa wamerudi kutoka Emau walikuwa wanajua , lakini Bwana alipowatokea wote walishikwa na hofu. Walijazwa na woga wakifikiri kuona kivuli. Ameongeza kusema Papa,  Uzoefu huo sawa na ule walioupata katika ziwa, wakati Yesu alipowaendea akiwa anatembea juu ya maji. Lakini siku ile Petro akitaka kuwa na ujasiri aliomba Bwana kama ndiye yeye amruhusu atembee naye juu ya maji. Siku hiyo Petro alibaki kimya, alikuwa amezungumza na Bwana asubuhi hiyo na mazungumzo yao hakuna yoyote anayejua ni nini walikuwa wamesemezana. Pamoja na hayo walikuwa namna hiyo wamejazwa na hofu kubwa. Na ndipo Bwana akawauliza kwa nini mmesononeka hivi, Kwa nini wasiwasi unatoka ndani ya mioyo yenu?  Tazemeni mikono na miguu … aliwaonyesha majeraha yake. Tunu ya Yesu iliyo peleka Mbingu ili amwonyesha Baba na kutuombea sisi. “Guseni na mtazame: kivuli hana mwili wala mifupa.

Papa Francisko aidha amekumba sentensi moja ambayo inampa faraja na kwa maana hiyo ni sehemu ya Injili moja kati ya  zile anazo zipenda sana na kusema kuwa:kutokana na kwamba walikuwa wanafuraha hawakuweza kuamini… “ na zaidi walikuwa wamejaa mshangao, furaha ambayo iliwazuia kuamini. Ilikuwa ni faraha kubwa ya kusema hii hapana siyo kweli….  Furaha hiyo ilikuwa ikiwazuia wasiamini maana ilikuwa ni kipindi cha furaha kubwa, kwa maana ngingine walikuwa wamegandishwa na furaha kubwa. Furaha ni moja ya matashi mema asemayo Mtakatifu Paulo kwa Waroma “ Na ili Mungu wa matumaini awajaze furaha” yaani furaha kubwa. Ni uzoefu wa faraha kuu ya Bwana anapotufanya kutambua kuwa kufurahia ni jambo chanya na lenye kuangaza.

Hata hivyo Papa Francisko pia kwa kuendelea kufafanua zaidi juu ya furaha amesema kwamba furaha hii ni kielelezo kinachojitokeza mara nyingi kwa mfano ilijitokeza katika Gereza na Petro akaokoa maisha ya wafungwa waliokuwa wanataka kujiua kwa sababu milango ya gereza ilikuwa imefunguka kwa tetemeko na baadaye aliwahubiri Injili, akawabatiza na wafungwa hao katika Bibilia inasema walikuwa wamejazwa na furaha kwa sababu ya kuamini. Furaha hiyo pia ilimtokea mhudumu wa Uchumi wa Candàce wakati Filipo alipombatiza na kutoweka machini pake, yeye aliendelea na safari yake akiwa na furaha kubwa; Vile vile siku ya Kupaa kwa Bwana: Biblia inasema mitume walirudi Yeursalem, wakiwa wamejaa furaha. Huu ni ujazo wa faraja, ujazo wa uwepo wa Bwana. Kwa sababu kama asemavyo Paulo kwa Wagalatia, “ furaha ni tunda la Roho Mtakatifu", siyo matokeo ya hisia ambazo zinaibuka kwa ajili ya kitu cha kushangaza... hapana  hii ni zaidi yake.. Furaha inayotujaza ni tunda la roho Mtakatifu. Bila roho hatuwezi kuwa na furaha. Kupokea furaha ya Roho ni nemaa.

Papa Francisko kadhalikwa  ameijiwa akilini kuhusu kurasa za mwisho wa Wosia wa Evangelii nuntiandi  wa Papa Paolo VI, anapo zungumzia wakristo wenye furaha, wajinjilishaji wenye furaha,na siyo wale ambao wana huzuni. Kufutana na hilo amesema: Leo hii itakuwa vizuri kusoma  yaani kujazwa furaha, kama Biblia inavyosema kwamba kutokana na kujazwa na furaha walishindwa kuamini. Aidha kuna sura nyingine ya kitabu cha Neemia ambacho leo hii kinaweza kusaidia tafakari zaidi juu ya furaha, ameshauri Papa Francisko. Sehemu hiyo ni kuhusu watu waliporudi Yerusalem na kukuta kitabu cha sheria ambacho waligundua kwa sababu walikuwa wanafahamu sheria ya kukarii na kitabu cha sheria hawakuwa nacho. Kwa maana hiyo waliungana kwa pamoja watu wote na kumsikiliza kuhani Esdra aliyekuwa anasoma katika kitabu cha sheria. Kutokana na kushangazwa sana walilia kwa furaha kwa sababu walikuwa wamepta kitabu hasa cha sheria na hivyo walikuwa na furaha hadi kutokwa machozi.

Papa Francisko amesema: Hatimaye kuhani Esdra alipomaliza kusoma, Nehemia akawambia watu “Hakikisha, sasa msilia tena, tunzeni furaha, kwa sababu furaha katika Bwana ndiyo nguvu yenu”. Neno hili kutoka katika kitabu cha Nehemia litatusaidia leo. Nguvu kubwa ambayo tunapaswa kuibadilisha, kuhubiri Injili, ili kwenda mbele kama mashuhuda wa maisha ni furaha ya Bwana ambaye ni tunda la Roho Mtakatifu, na leo tunamuombe atupatie matunda haya. Amehitimisha Papa Francisko mahubiri yake. Mwisho wa maadhimisho yake ya Misa ni pamoja na kuabudu na baraka ya Ekaristi Takatifu, wakati huo akiwaalika waamini kupata komunio ya tamaa. Kabla ya kuacha kikanisa, Papa Fracisko ameimba wimbo wa mwisho wa Malkia wa Mbingu wimbo uimbwao kwa kipindi chote cha Pasaka.

16 April 2020, 10:11
Soma yote >