Tafuta

Vatican News
Bwana atusaidie kutambua ubaya wa dhambi ya ulegevu. Bwana atusaidie kutambua ubaya wa dhambi ya ulegevu.   (ANSA)

Virusi vya Corona,COVID-19:Papa Francisko amesali kwa ajili ya madaktari na mapadre waliokufa!

Katika misa ya asubuhi tarehe 24 Machi 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican,Papa amewashukuru madaktari,wauguzi na makuhani ambao wanajikita katika kusaidia wagonjwa wa covid 19.Ni mfano wa kishujaa. Katika mahubiri ameonya juu ya dhambi ya ulegevu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika siku hizi wamepoteza maisha madaktari, makuhani na wauguzi. Wameambukizwa kwa sababu walikuwa katika huduma ya wagonjwa. Tusali kwa ajili ya familia zao. Ni karibia wahudumu elfu tano wa afya ambao wameambukizwa. Na karibia mapadre 50 wamekufa kwa sababu ya mlipuko huu wa Covid-19. Ninamshuru Mungu kwa kuwa na mifano ya kishujaa ambayo wametuonyesha katika kuuguza wagonjwa.  Ndiyo maneno ya Papa Francisko wakati wa utangulizi wake wa misa ya asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican tarehe 24 Machi 2020.

Kwa kutafakari Neno la Injili ya Yohane 5,1-16 ambapo Yesu anamponyesha mgonjwa katika kisima  amesisitizia juu ya hatari ya dhambi kwa namna ya pekee ulegevu. Papa Francisko amebaninisha kuwa katika liturujia ya siku inatufanya kutafakari maji, kwa kufikiria Gharika kuu la Nuhuu, lakini katika masomo ya ya siku  maji ni kama ishara ya wokovu.

Katika somo la kwaza Maji ambayo yanaleta maisha, yanasafisha bahari , ni maji mapya ambayo yanasafisha. Na katika Injili kisima kile mahali ambapo walikuwa wanakwenda wagonjwa wote kulikuwa kumejaa maji ili kutakasa na kila mara maji hayo yalikuwa yakitikiswa kama vile ya mto maana Injili inasema malaika alikuwa akishuka toka juu na wa kwanza kuingi ndani ya maji hayo alikuwa anapona. Ni wagonjwa wengi sana kama vile vipofu, wiwete walikuwa wanasubiri palei li waweze kuponywa.  Miongoni mwao kulikuwa na mtu ambaye kwa muda wa miaka 38 aalikuwa bado anasubiri aponyeshwe. Jambo hili linakufanya ufikirie kidogo amesema Papa je ni kwa nini?

Mbele ya mgonjwa, Yesu alimuuliza kama anataka kuponywa, lakini jibu la huyo ni la kushangaza kwa maana siyo la moja kwa moja, badala yake analalamika.  Ni mtu ambaye daima ufika akiwa amechelewa na kwa hakika alikuwa ameugua moyo, alikuwa ameugua roho,  alikuwa ameugua ugumu, alikuwa mgonjwa na tamaa mbaya, alikuwa mgonjwa na huzuni, na uvivu: analalamika juu ya wengine na hakufanya lolote  ili aweze kupona, Papa Francisko amesisitiza.

Hali hiyo Papa amesema , inamfanya afikiriwe  watu wengi kama sisi, wakristo wengi ambao wanaishi katika hali hii ulegeve: “inanifanya nifikirie wengi wetu, Wakristo wengi ambao wanaishi hali hii ya uvivu, hawawezi kufanya chochote lakini wanalalamika juu ya kila kitu na  kuwa  na sumu, au ukungu ambao unazungukia roho na haufanyi kuishi pia ni kama dawa ya kulevya kwa sababu ikiwa unaonja  ladha mara nyingi unapenda na unaishia kuwa mfanyakazi mwenye huzuni”.

Papa Francisko amedha mesema kuwa tujifikire hata sisi ikiwa tupo katika kuangukia kwenye mtego huo wa dhambi hiyo. Ni dhambi ambayo shetani anaweza kuitumia katika maisha yetu ya kiroho hata katika maisha ya watu.

Itakuwa ni vizuri anashuri Papa kusoma sura ya tano ya Yohane ili kujia ni jinsi gani magonjwa haya yanaweza kutuangukia hata sisi. Maji ni kwa ajili ya kutuokoa. Na Bwana atusaidie kutambua ubaya dhambi hiyo. Hatimaya mara baada ya misa takatifu ameendelea na ibada ya kuabudu na kuhitimisha kwa baraka ya Ekaristi.

24 March 2020, 12:44
Soma yote >