Tafuta

Vatican News
Papa amewaombea wale wote wanao teseka na kipeo cha uchumi kilicho sababishwa na mlipuko wa virusi vya corona na kuzuia shughuli nyingi za kazi. Papa amewaombea wale wote wanao teseka na kipeo cha uchumi kilicho sababishwa na mlipuko wa virusi vya corona na kuzuia shughuli nyingi za kazi. 

Virusi vya Corona,COVID-19:Papa Francisko amesali kwa ajili ya matatizo ya kiuchumi sababu ya virusi!

Katika misa takatifu ya asubuhi 23 Machi 2020,Papa Francisko amefikiria kipeo cha uchumi ambacho kinaendelea kuathiri nchi kufuatiana mlipuko wa virusi na mawazo yake ameyaelekeza kwa familia zenye matatizo kutokana na kutoweza kufanya kazi.Katika mahubiri Papa anawalika kujikita kwa kina katika maombi kwenye kipindi hiki kusali kwa imani,bila kuchoka na ujasiri.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Misa ya moja kwa moja katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, tarehe 23 Machi 2020, maneno ya kwanza ya Papa Francisko yalikuwa ni kuhusu imani. Ni maneno yaliyotokana na wimbo wa mwanzo, usemao “ninakutumainia ee Bwana. Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako, Kwa kuwa umeyaona mateso yangu. Umeijua nafsi yangu taabuni,.Wala hukunitia mikononi mwa adui; Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi. Kwa maana hiyo amewaombea wale wote wanao teseka na kipeo  cha uchumi kilicho sababishwa na mlipuko wa virusi vya corona na kuzuia shughuli nyingi za kazi. Papa mesema: tusali leo hii kwa ajili ya watu ambao kwa sababu ya virusi wameanza kuhisi matatizo ya kiuchumi, kwa sababu hawawezi kufanya kazi na kila kitu kinaangukia juu ya familia. Tuombe kwa ajili ya watu wenye matatizo.

Akianza kutoa mahubiri yake kwa kuongozwa na Injili ya Yohane( Yh 4,43-54) kuhusu uponywaji wa  mtoto wa diwani, Papa Francisko amewaalikA wasali kwa imani, bila kuchoka na ujasiri hasa katika kipindi hiki. Diwani aliombea mwanaye afya. Bwana anakaripia lakini kwa wote, lakini hata Yeye. Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa. Yule diwani badala ya kunyamaza akaendelea mbele na kumwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Papa Francisko akiendelea kueleza umuhimu wa sala amesema:Kuna mambo matatu yanayohitajika  ili sala iweze kuwa ya kweli. Kwani ni imani: ikiwa hamna imani… na mara nyingi katika sala zinakua za mazungumzo ya mdomo tu, lakini siyo kwa imani ya moyo au imani ni dhaifu… Kwa kutoa mifano zaidi amesema: Tufikirie baba mwingine mwenye mtoto aliyekuwa amepagawa na pepo, Yesu alipo mjibu kwamba “kila kitu kinawezekana kwa yule anayeamini. Kiukweli baba alito alijibu “ninaamini” lakini niongezee imani”.

Imani katika sala. Papa Francisko ameendelea kusema kuwa kusali kwa imani hata ikiwa tunasali nje hata ndani ya Kanisa na Bwana yupo hapo.  Jambo la kujiuliza  je nina imani au ni mazoea? Lazima tuwe makini katika sala. Tusiangukie katika mazoea ya sala  na dhamiri kwamba Bwana yupo, ya kwamba niko nazungumza na Bwana  a yeye ana uwezo wa kutatua matatizo. Na kumbe hali ya kwanza inayohitajika kwa ajili ya sala ya kweli ni imani. Akiendelea kufafanua zaidi amesema: Hali ya pili ambayo Yesu mwenyewe anatufundisha ni uvumilivu. Baadhi wanaomba neema, lakini hawapati, kwa sababu hawana uvumilivu, au chini chini awahitaji au hawana imani. Na Yesu mwenyewe anatufundisha katika msemo wa bwana yule aliyekwenda karibu kuomba  mkate usiku wa manane. Uvumilivu wa kubisha mlango… au yule mwanamke mjane na hakimu hasiyejali. Yeye alisisitiza na kusisitiza, ndiyo huo uvumilivu. Imani na uvumilivu vinakwenda pamoja, kwa sababu wewe ukiwa na imani una uhakika kuwa Bwana atakupatia kile unachokiomba.

Ikiwa Bwana anatakufanya usubiri, wewe bisha, bisha, bisha na mwishowe Bwana atakupatia neema. Lakini Bwana hafanyi hivyo kwa ajili ya kukuridhisha kwamba anataka au  kusema subiri hapana. Yeye anafanya hivyo kwa ajili ya wema wako na ili kuweza kuwa makini zaidi. Kuwa makini katika sala na siyo kama kasuku  mwenye maneno tu ya bla bla bla bila kitu zaidi….  Yesu mwenyewe anatukaripia. “Msiwe kama watu wa mataifa ambao wanaamini wamesali kwa maneno mengi”. Hapana inahitaji uvumilivu na ni imani.

Hali ya tatu ambayo Papa Fancisko ameielezea na ambayo Mungu anapenda katika sala ni ujasiri. Papa amesema:Mwingine anaweza kujiuliza hivi inahitaji ujasiri katika sala kukaa mbale ya Bwana? Inahitajika! Ujasiri wa kukaaa na kuomba na kwenda mbele na zaidi, siyo kukana, bali ni kama vile kumtishia Bwana. Ujasiri  wa Musa mbele ya Mungu alipokuwa anataka kuharibu watu na kuwapatia kiongozi wa watu wengine. Anasema, hapana mimi na watu wangu, hivyo ni ujasiri. Ujasiri wa Ibarahim alipokuwa anabishana na kutetea wokovu wa Sodoma. Yeye alisema ikiwa ni 30 , ikiwa ni 25 , ikiwa ni 20… huo ndiyo ujasiri. Fadhila ya ujasiri inahitajika sana. Siyo kwa ajili ya matendo ya utume lakini hata kwa ajili ya sala.

Papa Francisko akiendelea kusitiza zaidi amesema: Imani, uvumilivu na ijasiri. Katika siku hizi ni lazima kusali, kusali zaidi, tufikirie ikiwa sisi tunasali namna hii kwa imani ambayo Bwana naweza kuingilia kati kwa uvumilivu na ujasiri. Bwana hakatishi tamaa kamwe. Itakuwa vizuri kuwa na subira na kuwa na muda lakini haikatishi tamaa. Imani, uvumilivu na ujasiri.

Hatimaye Papa Francisko amehitimisha maadhimisho ya misa kwa kuabudu ekaristi takatifu na baraka ya ekaristi, na kuwaalika waamini wapokee kumunio rohoni mwao kwa kusali sala  hii: Chini ya  miguu yako, Ee Yesu wangu, ninakusujudu na kukupa toba ya moyo wangu ambayo inajificha ndani ya uwepo wako mtakatifu. Ninakuabudu katika sakramenti ya upendo wako, Ekaristi. Natamani kukupokea katika makazi duni ambayo moyo wangu unakupa; kwa kungojea furaha ya muungano wa sakramenti ninataka kukuhifadhi wewe katika roho. Njoo kwangu, oh Yesu wangu, na ili kwamba mimi nije kwako. Mapenzi Yako yaweze kuwasha uzima wangu wote na kwa ajili ya kifo. Ninakuamini ninakutumaia ninakupenda. Basi iwe ndiyo hivyo.

 

23 March 2020, 12:09
Soma yote >