Tafuta

Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican Papa Francisko aimetolea watawa ambao wako karibu na wagonjwa na maskini Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican Papa Francisko aimetolea watawa ambao wako karibu na wagonjwa na maskini  (Vatican Media)

Papa amesali kwa ajili ya watawa wanaohatarisha maisha wakitoa huduma kwa wagonjwa!

Misa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta,sala yake Papa Francisko imelekezwa kwa watawa ambao wako karibu na wagonjwa na maskini,kwa namna ya pekee anawakumbuka watawa wa Shirika la Mtakatifu Vincenti wa Pauli ambao kwa miaka 98 wanatoa huduma yao mjini Vatican katika kituo cha afya na katika familia zenye kuhitaji msaada duniani kote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko kama ilivyo kwa kipindi hiki maalum ameadhimisha Misa ya Moja kwa moja tarehe 25 Machi 2020 katika Kakanisa cha Mtakatifu Marta Vatican, wakati Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Kupashwa habari Bikira Maria, na kukumbuka Mungu aliyefanyika Mwili. Katika utangulizi wa maadhimisho hayo Papa amesali kwa ajili ya watawa wa Mtakatifu Vincenti wa Pauli ambao wanatoa huduma yao katika kituo cha afya mjini Vatican kwa maskini na kwa ajili ya watawa wote ambao wanahudumia wagonjwa, kwa namna ya pekee katika kipindi hiki chenye tabia ya mlipuko wa virusi vya corona.

Leo hii katika Siku kuu ya Kupashwa habari Bikira Maria watawa wa Mtakatifu Vincenzo de’ Paoli, ambao wanashughulika na kutoa huduma katika kituo cha Afya kwa miaka 98, wanashiriki misa na wnaarudia nadhiri zao pamoja na watawa wengine katika kila pembe ya dunia. Leo ninapenda kuitolea misa hii kwa ajili yao, kwa ajili ya Shirika ambalo linafanya kazi daima kwa wagonjwa, maskini zaidi kama ilivyo hapa kwa miaka 98 na kwa ajili ya watawa wote ambao wanafanya kazi kwa sasa wakiwahudumia wagonjwa na ambao wanahatarisha maisha kwa kutoa maisha yao.

Katika mahubiri Papa Francisko ametoa nafasi  ya Fumbo kubwa la Bwana kufanyika Mwili kwa kurudia kusoma Injili ya Luka ambayo imetolewa katika Siku kuu hii na kusoima kwa taratibu: Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye ju, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake. (Lk 1,26-38).

Hilo ni fumbo! Papa ameongeza kusema na kukaa kimya kwa muda katika tafakari. Papa Francisko amehitimisha maadhimisho kwa kuabudu na kubariki kwa ekaristi akiwaalika waamini wapokee komunio ya tamaa  kwa kusali sala hivi:  Chini ya  miguu yako, Ee Yesu wangu, ninakusujudu na kukupa toba ya moyo wangu ambayo inajificha ndani ya uwepo wako mtakatifu. Ninakuabudu katika sakramenti ya upendo wako, Ekaristi. Natamani kukupokea katika makazi duni ambayo moyo wangu unakupa; kwa kungojea furaha ya muungano wa sakramenti ninataka kukuhifadhi wewe katika roho. Njoo kwangu, oh Yesu wangu, na ili kwamba mimi nije kwako. Mapenzi Yako yaweze kuwasha uzima wangu wote na kwa ajili ya kifo. Ninakuamini ninakutumaia ninakupenda. Basi iwe ndiyo hivyo.

25 March 2020, 10:09
Soma yote >