Tafuta

Vatican News
Tarehe 13 Februari 2014 Papa Francisko katika tafakari ya siku amefafanua juu ya Mfalme Somoni alivyoingia kwenye mtego wa dhambi Tarehe 13 Februari 2014 Papa Francisko katika tafakari ya siku amefafanua juu ya Mfalme Somoni alivyoingia kwenye mtego wa dhambi  (Vatican Media)

Papa Francisko:tuombe neema ya kutoteleza katika dhambi!

Katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 13 Februari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican anatoa onyo ili kutoteleza taratibu katika dhambi akifafanua kuhusu historia ya Solomoni.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa mahubiri ya Papa Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, amebainisha juu ya hatari ya utelezi kwa taratibu katika dhambi hasa kwa kuacha ufanye  majadiliano na ibilisi kama vile ya  pesa, ubatiri na kiburi. Ametafakari hayo kwa kuongozwa na Somo la Kwanza la Siku kutoka katika Kitabu cha kwanza cha Wafalme 11,4-13. Somo linalosimulia juu kuteleza kwa Solomoni aliyekosa kuwa mwaminifu kwa Bwana  hadi mwisho. Papa amaesema , alipokuwa mzee, wake zake, walimfanya abadilishe moyo wake na kufuata miungu mingine. 

Tangu mwanzo Solomoni alikuwa ni kijana mzuri ambapo alikuwa amemwomba Bwana hekima na Mungu akamjalia awe na hekima mpaka ya kumfanya asifike kila mahali hadi Malkia wa Saba kutoka Afrika akaja na zawadi zake nyingi kwa maana alikuwa alisikia alivyokuwa na hekima. Francisko amebainisha kwamba inaonekana kuwa mwanamke huyo kidogo alikuwa ni mwanafalsafa kwa maana alimuuliza maswali magumu lakini Solomoni aliweza kuyajibu yote kwa ushindi na alikuwa anatambua vizuri kujibu.

Katika nyakati zile  Papa amefafanua kuwa kulikuwa na uwezo wa  kuwa na wanawake wengi lakini ambapo hakuwa na maana kuhalalisha kufanya utakavyo. Moyo wa Solomoni lakini ulianza kuwa mdhaifu na siyo kwa sababu ya kuoa wanawake wengi hao bali kwa sababu alikuwa amechagua katika watu wengine ambao walikuwa wanaabudu miungu.  Kutokanna na hiyo Solomoni akaanguka katika mtego hasa mwanamke alipokuwa akimwambia aende kuabudu Camos au Moloc. Na kwa maana hiyo alifanya hivyo kwa wanawake wengine wote ambao walikuwa wanatolea miungu dhabìhu. Kwa kifupi aliacha kuabudu Mungu mmoja wa kweli. Moyo wake ukawa dhaifu kwa sababu ya kupenda sana wanawake na kuingia katika upagani wa maisha yake.

Kwa kufafanua zaidi na mifano Papa amesema, kijana mbaye alikuwa anasali vizuri na kuomba kwa hekim, akaanguka hadi kufikia kumkana Bwana. Huo siyo mchakato wa safari ya siku moja, bali ulikuwa ni mchakato wa safari ya taratibu. Hata Mfalme Daudi, baba yake alikuwa na dhambi kubwa  hata mara mbili, lakini aliungamana na kuomba msamaha na kubaki mwaminifu kwa Bwana ambaye alimlinda hadi mwisho.  Daudi alilia sana kwa dhambi na kwa ajili ya mtoto wake alipopata taarifa za kifo chake, na wakati alipomkimbia kwa sababu yake alijinyenyekeza sana hasa alipokuwa akifikira dhambi yake na zaidi watu walipokuwa wakimdhihaki. Kwa hakika alikuwa ni mkatifu, amesema Papa. Solomoni si mtakatifu Bwana alikuwa amempatia zawadi nyingi lakini yeye alizitumia zote na kuacha kudhoofisha moyo wake, hivyo dhambi hiyo siyo ya mara moja tu ni kuteleza taratibu taratibu

Lakini Je ni mara ngapi tunasahau Bwana na kuanza majadiliano na miungu mingine kama vile ya  pesa, ubatiri na kiburi?, ni swali la Papa na kuongeza kusema mambo haya yanakuja taratibu kama hakuna neema ya Mungu, unaweza kupoteza kila kitu. Papa pa  ametaja mfano mwingine wa mke wa Uria aliye danganywa… Inabidi kuwa makini dhidi ya kuteleza katika maisha ya kidunia. Na maneno ya kidunia yanafanya upoteze maana ya Injili, maana ya Neno la Mungu na kupoteza ile tabia ya  kuogopa Mungu ambaye ametoa maisha kwa ajili yetu . Na hii ni kwamba haiwezekani kukaa na Mungu na kukaa na ibilisi, ina maana ya kupoteza umaninifu.

Papa Francisko amehitmisha kwa kuomba neema ya Bwana ili kutambua kila hila za ibilisi. Kwa kufikiria dhambi ya Solomoni, kufikia namna alivyo anguka, yeye aliyekuwa mwenye hekima, aliyekuwa amebarikiwa na Bwana, akawa na urithi wote wa mfalme Daudi, baba yake, kwa jinsi alivyo teleza taratibu katika kuabudu miungu katika hali ya kidunia na baadaye kunyang’anywa ufalme. Tuombe Bwana neema ya kujua hasa moyo unapoanza kudhoofika na kuteleza, ili ausimamishe. Itakuwa ni neema ya upendo wake kusimamisha iwapo sisi tunamwomba!

13 February 2020, 14:52
Soma yote >