Tafuta

Vatican News
Papa Francisko wakati wa Misa tarehe 24 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican amebainisha kuwa wivu unapelekea vita japokuwa  daima ni kama povu la sabuni. Papa Francisko wakati wa Misa tarehe 24 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican amebainisha kuwa wivu unapelekea vita japokuwa daima ni kama povu la sabuni. 

Papa Francisko:wivu unapelekea vita japokuwa ni povu la sabuni!

Katika mahubiri ya Misa Takatifu,Ijumaa tarehe 24 Januari 2020 amekuwa na mtazamo dhidi ya wivu unaopelekea vita, wivu unapelekea kuwahukumu vibaya wengine na masengenyo ambayo yanaua mwingine lakini ni kama povu la sabuni.Maombi ya Papa ni kwamba,Bwana atupatie neema ya kutambua hayo kama ilivyokuwa Sauli aliyetaka kumuua Daudi.

Na Sr. Angela – Vatican

Tunajaribiwa mara nyingi na wivu sana ambao unatupelekea kuwahukumu wengine vibaya na kuleta migongano ndani ya familia, mitaani na katika nafasi za kazi. Hii ni mbegu ya vita, masengenyo, ambayo awali ya yote yanaua nayetoa hata kwa wengine. Lakini ukifikiria vizuri mambo hayo yanaishia vibaya kama povu la sabuni. Ndivyo Papa Francisko ametoa tafakari katika Misa Takatifu ya Ijumaa tarehe 24 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta, Vatican ambao mada kuu ya wivu imetokana na Mfalme Sauli kutaka kumuua Daudi.

Wivu ni uhalifu

Papa Francisko amekumbusha kuwa wivu wa mfalme kama ulivyojieleza katika kitabu cha Kwanza cha Nabii Samweli, inazaliwa kutokana na ushindi wa kijana, ambapo Sauli aliuwa maadui elfu moja na Daudi elfu kumi.  Kwa maana hiyo Sauli alitoka na jeshi lake ili kwenda kumuua Daudi. Wivu ni uhalifu mkubwa ambao unatafuta daima kuua wengine anasema Papa. Je ni nani anasema ndiyo mimi ni mwenye wivu lakini siyo muaji? Lakini kumbuka kuwa ukiendelea kuwa na wivu utaishia vibaya na unaweza kufikia kuua tena kwa urahisi kwa njia ya mdomo na masengenyo. Wivu unakuwa kwa kuzungumza mambo mengi ya uongo dhidi ya wengine, na hayo yote yanafunga masho hadi kukosa kuona ukweli, badala yake ni. Sali kwa njia hiyo  alikuwa na  wivu sana hadi kumfia katika kutaka kumuua Daudi aliye fikiria ni adui wake. Hata sisi tunaposhikwa na wivu na chuki, lazima tujiulize ni kwa nini na hatimaye kuomba Neema ya Mungu ili  aweze kutuepusha na ugonjwa huo.

Wokovu wa sauli

Wokovu wa Sauli ulitokana na upendo wa Mungu amekumbusha Papa na ambaye alikuwa amemwambia kama hatatii angemwondolea Ufalme, lakini alikuwa anampenda. Na kwa maana hiyo alimpatia neema. Hii yote Papa amesimulia ni kwa jinsi gani Sauli aliingia ndani ya pango kujificha mahali ambapo Daudi tayari alikuwa humo ndani. Maaskari wenzake walimwambia Daudi atumie nafasi hiyo kumuua Mfalme, lakini yeye alikataa kuwa ataweza kudhuru kamwe aliye na Mpako wa Bwana. Hii kwa hakika inaonesha umakini na utambuzi wa Daudi kulinganisha na mwenye wivu na muuaji Sauli. Na kwa ukimya alikata kipande kidogo cha joo lake la kifalme na kuondoka nacho. Daudi mara baada ya kutoka nje alimwita Sauli “ Ewe Bwana wangu hata kama unataka kuniua. Daudi anamwambia kwanini anapenda kusikiliza sauti ambazo zinasema Daudi anakutakia mabaya? Kwa uhakika alimfanya atazame kile kipande na kumweleza kwamba angemuua, lakini hakifanya hivyo.

Sauli alijitambua wivu wake baada ya kuyeyuka kama povu la sabuni

Papa aanaendelea kubainisha kuwa hii ni kuonesha jinsi gani  povu la wivu kama sabuni lililoyeyuka la Saulo na kutambua wakati huo kuwa Daudi ni mwanae na kurudia hali halisi akisema: Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya”. Hii ni neema anasema Papa ikiwa mwenye wivu anajikuta mbele ya hali halisi na kulia kwa sababu  ya wivu wake Papa Francisko kwa maana hiyo anawaalika waamini kutazama ndani mwao binafsi. Kama kuna mdudu wa wivu ambaye anakua ndani ya moyo. Ni lazima kulinda mioyo yetu dhidi ya ugojwa huu mbaya na ambao unafanya kukua kwa povu la sabuni tu na lisilokuwa na mshiko, kwa maana hatima yake utaishi pabaya. Hata mtu mwingine akisema mabaya dhidi yako lazima kumfanya atambue kuwa ni vema kuzungumza kwa utulivu tu na kwa njia ya wema. Ni lazima kuasha chauku za kuoneana wivu.

Tuombe Bwana atuepushe na kutupatia neema ya kuwa na moyo wazi kama wa Daudi

Tuwe makini Papa anasema iwapo tunahisi ndani ya kuwa ni wivu na kujiulize kwa nini tunahisi hivyo? Tuepukane na masengenyo na kufikiria vibaya wengine. Tuombe Bwana neema ya kuwa na moyo ulio wazi kama ule wa Daudi, moyo wazi ambao unatafuta haki tu, unaotafuta amani. Moyo wa upendo, moyo ambao hautaki kuua yoyote kwa sababu ya chuki na wivu ambao unaua.

24 January 2020, 12:53
Soma yote >