Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican  (ANSA)

Papa anasahuri usikubali kutawaliwa na tamaa

Msikubali kutawaliwa na tamaa na msisubiri uongofu wa moyo,bali mwongokee Mungu.Ndiyo wazo la mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko alhamisi tarehe 28 Februari 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican.Anamwalika kila mmoja kutafakari dhamiri kwa kipimo cha matendo binafsi hakuna uhakika kwa jinsi gani maisha yataishia

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni muhimu kusimama na kutafakari ndani ya dhamiri na kujishinda binafsi kwa utambuzi ya kwamba siku ya mwisho inaweza kufika punde bila kuchelewa,siyo kuishi unarudia kusema ipo huruma ya  Mungu isiyo na kikomo, kwa maana huo ni uthibitisho wa kuendelea kuishi unavyotaka bila mabadiliko ya ndani. Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Februria 2019 kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican ameongozwa na ushauri kutoka somo la Yoshua Bin Sira na kuwashauri wabadilishe  mioyo katika uongofu kwa Bwana.

Tamaa inatawala,hivyo itawale wewe

Kuwa na hekima ni jambo la kila siku na linazaliwa katika tafakari ya maisha katika kusimama na kufikiri kwa jinsi gani ya kuishi. Ni kwa kusikiliza Neno la Mungu ndipo pia unapata ushauri kutoka kitabu cha Yoshua bin Sira ambacho kinafanishwa na maelekezo ya baba akimshauri mwanae au babu na mjukuu wake, Baba Mtakatifu anathibitisha. Akiendelea na mahubiri anasema, usifuate hisia zako, nguvu zako kwa kukubaliana na tamaa ya moyo wako. Kwa maana wote tunazo tama; badala yake ni lazima kuwa makini na kuzitawala hizo tamaa. Ziwe mikononi mwako maana tamaa wakati mwingine siyo mambo mabaya, kwa maana zipo ndani ya damu lakini kwa ajili ya kupeleka mambo mengi mema mbele. Japokuwa, iwapo hutuna uwezo wa kuzitawala, tamaa hizo zitakutawala wewe binafsi, kwa maana hiyo simama na uzitawale.

Usisubiri uongofu wako bali ongoka!

Baba Mtakatifu akiendelea kujikita katika maisha ya kila siku anataja sehemu ya zaburi isemayo “Jana nimepitia na kumwona mtu:leo hii nimerudi lakini hayupo  tena. Mtu siyo wa wa milele, anabainisha Baba Mtakatifu, huwezi kufikiria kufanya kile unachotaka kwa kutegemea huruma isiyo na kikikomo ya Mungu. Usiwe hivyo, na hofu kwa kuamini kuwa “peke yako utaweza kwa maana ya kujidanganya kwamba: hadi sasa umeweza hivyo utaendelea kujitosheleza. Hapana, kwa maana uliweza wakati ule, lakini kuanzia sasa huwezi kujua … ni bora kutosema hivyo, Baba Mtakatifu anatoa angalisho. Halikadhalika kwa kufikiria kuwa huruma ya Mungu ni kubwa atanisamehe dhambi zangu nyingi, hivyo nitandelea mbele kufanya kile ninachotaka. Husisema hivyo. Na ushauri wa mwisho wa baba huyo na babu huyo unasema: usisubiri Bwana atoe uongofu wako, usisubiri uongofu,  bali ubadili maisha, ondoa yale magugu mabaya, kwa maana wote tunayo, lakini yatoe mwenyewe… isisubiri kumwongokea Bwana na kusubiri siku hadi siku, kwa maana bila kujua hasira ya Bwana itapasuka!

Dakika tano kwa ajili ya uongofu wa moyo

Usisubiri ongoka,ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu kwamba, hakuna kusubiri kubadilisha maisha binafsi, kugusa kwa mkono wako kufilizika, kutofaulu na usiogope, bali uwe na uwezo wa kutawala kile kinacho sababisha kuwa na tamaa. Ni vema kutafakari ndani ya dhamiri kila siku angalau kwa dakika tano ili kuweza kumwongokea Bwana. Mwisho wa siku nzima, katika  dakika hizo zikusaidia kufikiri, bila kusubiri tena  madiliko ya moyo na kumwongokea Bwana.  Na  Bwana atufundishe kuwa na hekima yake  ili kuelekea katika njia hii.

28 February 2019, 14:15
Soma yote >